Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Very Goood! Hapo umenena Mkuu, Mama Mhe. Rais aachwe, apewe moyo ili aweze kufanya kazi zake kwa kujiamini na hapo atafanya kwa ufanisi
 
Mleta mada unataka umoja upi na umoja na nani? Tatizo ni maneno mengi mnayotumia lakini mnachomaanisha ni interests zenu ziangaliwe. Tusiwe akina pangu pakavu. Kila mtu analazimisha mchuzi uwekwe kwake kwanza. Muacheni Rais aongoze nchi.
 
Toka Rais SSH ameapishwa rasmi kuongoza nchi yetu ni muda wa kama mwezi mmoja tu umepita. Hapo achilia mbali siku za maombolezo na shughuli za mazishi ya Rais aliyetangulia.

Kwa hiyo basi katika hali ya kawaida ya kiutendaji, muda huu ni mfupi mno kuanza kufanya tathimini juu uongozi wake. Nafikiri hata kupitia "rule of thumb" utendaji wa viongozi wapya wa nchi huanza kuangaliwa kwa jicho la shahuku ktk siku 100 za mwanzo za uongozi wao.

Rais SSH hata bado ajakabidhiwa rasmi uenyekiti wa CCM kitaifa. Tuzidi tu kuwa wavumilivu na kuzidi kumtia moyo na kumpa ushirikiano wakati anapojipanga zaidi na kupanga safu ya wasaidizi wake ili aweze kuiongoza vyema nchi yetu.
 
Katiba mpya ndio itaibadilisha hii nchi
Katiba mpya ni muhimu lakini si kwa hili bunge linalocheza (kudemka) na ngoma za mitandao I. La mwanzo na muhimu ni kuwa na tume huru na ya haki itakayotupa wabunge ambao ni wawakilishi waliyopata ridhaa ya wananchi ili waweze kuisimamia upitishaji wa katiba mpya.
 
Too early to pass judgement on Samia Leadership! Tumpe muda angalau hta siku mia moja za mwanzo ni bora zaidi kuliko mwezi mmoja wakati hata muundo wa serikali yake haujakamilika!
Naona kama anatembea kwa kunyata (anakanyaga kwa kunyata). Anakwenda kwa mwendo wa kukiogopa chama chake. Ndani ya CCM waliowengi hawataki kusikia kwamba mama anatenda tofauti na mwendazake. Yaani mawazo yao ni kwamba Samia Suluhu "amefundishwa kazi" na JPM, hivyo atafanya kama JPM. Hili jambo la kifo cha JPM halijawaingia akilini kabisa. Mama ameamua kutumia hizo lugha ili kuwaridhisha wapambe wa mwendazake na wao kwa jinsi walivyochanganyikiwa, wameamini kwamba John na Samia ni kitu kimoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani tathimini yako siyo sawa. Kuna mengi ameongea na yamefanyika na mengine bado yanafanyiwa kazi.

Hivi mnataka Rais afanye kila kitu kwa siku moja? Tumpe nafasi na ushirikiano.

Ina maana wewe hujaona watu wamefunguliwa account zao zilizoshikiliwa kwa miaka zaidi ya mitatu.
 
Mama yupo vizuri sana,mwendo anaoenda wazee wa fursa (zile gangs)wana weweseka sana.
Mama kamua twende.Endeleza mema tu!!
Safari iendelee
 
Huo ni ukweli ulio bayana.

Ukiangalia na kusikia ya hapa na pale ndani ya muda ambao Rais Samia amechukua madaraka hakika magomvi, dharau na kutuhumiana waziwazi kwenye kada mbalimbali kumetamalaki.

Mfano ni katika Idara mbalimbali za Serikali Viongozi wengi kwa muda mfupi baada ya kifo cha Magufuli waziwazi ama wanatishana kuuana kwa sababu ya maslahi ama wanadharauliana na kuchongeana ili tu mmoja wao aonekane bora dhidi ya mwingine.

Kinachosikitisha hayupo yeyote anayewakemea ama kuwaadhibu. Mamlaka za wagomvi wale zipo kimya jambo ambalo katika Utawala uliopita kamwe wajinga wale wasingevumiliwa.

Kwa muktadha huo naliona mapema sana anguko la Samia.
 
Timu Magu kazini.

Ujue kuna muda wakuzibua watu vibao washtue mzee alishafariki na lazima kukubali utawala mpya.

Hayo ulosema yapo tangu muda tuu sema wakati umelewa mvinyo wa maneno ya Magu ulikuwa huyaoni.. Alafu ule ulikuwa sio uongozi ila ni ubabe.. Mlipendelewa nyie timu kuabudu alafu wengine wakiumia . Sa hivi kibano kimegeuka mnalia.
 
Ni kweli mama Ana uwezo mdogo lakini kama wasaidizi wake wakiwa wazuri Basi hamna shida.

Siku zote wanawake huwa Wana uwezo mdogo ndo maana 99.999% ya manabii Ni wanaume...walioacha legacy Wengi Ni wanaume
Hapo ampe nguvu majaliwa , atamsaidia Sana asimbeze jamaa anaweza , vinginevyo mambo yatamharibikia , nchi ni ngumu kuiongoza .... Yeye abaki Tu kusimamia na kurekebisha mana yeye ndo final and high command, Ila asiwe mbishi na asiye jali raia kama alivyokuwa Jiwe....kwenye usimamizi nilikuwa pamoja na Jiwe, Ila kwenye matumizi tulitofautiana vibaya Sana na jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…