Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Hana lolote huyu Samia Suluhu. Tunapoteza muda. Híi nchi ni complex. Hana uwezo wa kuiongoza. Nilisahau kuisikiliza spichi yake ya Mei Dei. Nasikia ilisheheni makosa mengi.
Haya,tumsikie atawaambia nini Wabunge wa Kenya leo. Mangi-meza tupo wengi tunaisubiri spichi yake.

 
Anaogopa kusemwa mpaka afe kama JPM,anataka sifa tu, sasa ataona wakina mama wakifia kwenye mawodi
 



Nashangaa sana hadi natamani kuzimia nikisikia baadhi ya watu wanasifia eti hotuba tamu. Tamu!??? Imekuwa choroko hiyo!??? Watu hawajui kwamba hata panya au mbu akitaka kukufaidi damu huwa ANAPULIZA ndipo ANANG'ATA.
 
Magufuli kiongozi akilalamikiwa na wananchi,anamwita pale pale, anafanya naye mental sparring pale pale kwenye halaiki.
Pale pale kwenye halaiki anampiga knockout anamwambia,"kazi basi"
 
Kwenye utilianaji saini mikataba ya kiuwekezaji Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni muhimu ahusishwe, sasa kwanini hatujamuona Profesa Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali? Mnaficha nini?

Au tuamini mafisadi wameanza kuivamia nchi sisi wazalendo and the entire Afrika tunahoji usiri huo lakini kumbuka wewe umengia kwa utaratibu fuata utaratibu hatutakubali kuchezewa kwa rasilimali zetu na kikundi cha watu wachache.
 
Yawezekana waziri asiwepo lakini utaratibu ukafuatwa
Na waziri anaweza kuwepo na utaratibu usifuatwe vilevile


Kwani huo mkataba wenyewe unasemaje🤔🤔
Heri kuona mambo waziwazi kuliko kuota ndoto!
 
Kilicho sainiwa KENYA sio mkataba.. Kilicho sainiwa ni Makubaliano ya kuelekea katika kufanikisha huo mradi wa Bomba la gesi..

MEMORANDUM OF UNDERSTANDING (MOU) ndo kitu kilichosainiwa, hii inamaanisha mazungumzo zaidi yanafuatia kuelekea katika kusaini mkataba wenyewe.

Tuwe tunafuatilia kabla ya kutoa taarifa zetu.
 
Tulikuwa na maisha mazuri na ya furaha wakati unaowaita mafisadi wanatawala Tanzania kuliko hao wazalendo wako wa kuchonga akina Magufuli. Kama uzalendo ndiyo yale Mwendazake alikuwa anafanya, basi uzalendo ni UHANITHI

Mafisadi waendelee kwa maisha bora ya Watanzania
 
Huna lolote we sukuma gang. Kwa huyo Maghufuli mikataba imewahi kuwa wazi ?!. Ni lini iliwahi kuwekwa wazi mikataba ?! Wapinzani Cdm wamekuwa wakidai miaka yote mikataba ipitishwe bungeni kwa kujiridhisha lakini Ccm na serikali haijawahi kuwa tayari.

Mwacheni Mama afanye kazi yake. Na daima hawezi kuongoza sawa na huyo Maghufuli wako. Maghufuli mwenyewe kasoro zilikuwa kibao
 
Yule hakuwa na kasoro isipokuwa alikuwa dikteta kabisa
 
Good
 
KUMBUKIZI za Mikataba.
Hii inanikumbusha ule mkataba wa MUUNGANO WA TANZANIA 1964.
Mwanasheria mkuu wa Zanzibar (Welfong Dorado) hakuwepo kwenye maandikiano yale.
Hivi Kutilianasaid kule Ulikuw Memorundum of Understanding tuu? Hukuwa Mkataba Kamili?



 
Inawezekana kuna watu hawali wala kulala wanawaza utendaji kazi wa mama tu. Jamani, muacheni mama afanye kazi, ujue mtaanza kumpanikisha alafu ataanza kuwa defensive alafu ndio atawaumiza zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…