Tutegemee mambo mengi toka kwa Rais Samia Suluhu. Mojawapo ni tabia nyingi za aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne Ndugu Jakaya Kikwete.
Safari zitakuwepo nyingi sana na majambazi yatampangia safari nyingi ili yabaki yakiiba pesa za umma. Kuna uwezekano mkubwa sana wa Nchi kusimama.
Lakini faida ni yeye katika kutaka kuwafurahisha watu kwa furaha za muda mfupi huku nchi baadaye ikiingia kwenye majanga
Wauzaji wa madawa ya kulevya na biashara haramu wanaanza kurudi wakiamini sasa watakuwana nafasi ya kuja haribu tena maisha ya watanzania. Mtandao wao unafahamika ulikuwa mkubwa mpaka ndani ya Serikali kuu.
Sijui yeye atakuwa na mtizamo gani katika hilo. Lakini tutegemee maisha yale mazuri ya kipindi cha kikwete katika awamu hii. Ya kila mbuzi kula kutokana na urefu wa kamba yake.
Tofauti na kikwete labda ni kuwa Speeches za huyu mama anaongea kwa utulivu na anakuwa amejipanga. Kikwete hakuwa na mvuto wa kuongea au kusikilizika. Tofauti ya kikwete na magufuli ni kuwa magufuli alikuwa na maneno makali but kikwete maneno yasiyo na maana.
Kama tunapenda speeches nzuri basi tutaendelea kuzipata kila mara. Hizi mama atajitahidi kuendelea kuwa nazo. Na kwa kuwa tulizimiss kila baada ya speech tutampongeza sana kwa kutufariji. Na ni kweli watanzania wanapenda maneno ya faraja. Tuendelee kupata.
Mnaweza kidogo mkachanganyikiwa kwa nlichoandika. But ndani kwenye threads mnaweza pata some points.mengine achana nayo