Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kwani wakati wa Magufuli Huyo Kabudi mzee wa Jalalani alifanya nini cha maana?

Acheni kumpa Prof wa majalalani sifa asizostahili
 
Yawezekana waziri asiwepo lakini utaratibu ukafuatwa
Na waziri anaweza kuwepo na utaratibu usifuatwe vilevile


Kwani huo mkataba wenyewe unasemaje🤔🤔
Si mnakumbuka Waziri huyu si ndio alikuwepo, wakati wa ule kutia saini mkataba wa kampuni feki ya kununua korosho toka Kenya na akapiga na selfie, akionyesha mkataba na kutuhakikishia kwamba mambo ni safi, lakini matokeo yake kila mtu anajua kilichotokea yakawa maumivu....kazi iendelee.
 
Hauna cha kumfanya Mama utaishia kuandika humu humu JF[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
yes, ni kama kilichofanyika kuhusu bandari ya bagamoyo enzi za mkwere......


majadiliano yalifanywa chini ya magufuli
 
Hakuna profesa wa sheria muongo kama Kabudi.
 
Yawezekana waziri asiwepo lakini utaratibu ukafuatwa
Na waziri anaweza kuwepo na utaratibu usifuatwe vilevile


Kwani huo mkataba wenyewe unasemaje🤔🤔
Hata AG asiwepo? Si ndo Chenge alipokuwa akiwapigia hapo?
 
Kenge wewe, nenda kamshauri JIWE uko alipo, anabebeshwa viroba vya korosho mwanzo mwisho, we si kutwa unamtukana rais wetu, sasa huo ushauri unampa wa nini, we Musiba lazima uende jela awamu hii
 
Kama mnaona hamfuati magufuli si mumfuate mwenda zake mkaongozwe ki magufuli ?
 
Kwa taarifa yako hakuna mkataba unatiwa saini na nchi bila kupitia kwa mwanasheria mkuu wa serikali
 
Mikataba daima haisainiwi na Bunge. Labda tujianzishie utaratibu mpya
 
Mikataba daima haisainiwi na Bunge. Labda tujianzishie utaratibu mpya
Sasa uwazi mnautaka kwenye mikataba mtaupatia wapi ?!. Chombo cha wananchi ni Bunge . Vinginevyo usiri serikalini utaendelea na kwa sababu pia huwa wanaapa kutunza siri .
 
Nonsense!

Kila siku unaanzisha post zenye maudhui negative juu ya mama yetu. Why?

Tuachie mama yetu. Kitabu cha baba yako Jiwe kimeshafungwa!
 
Mkuu usipende kuendekeza rushwa. Sisi tunaolipa kodi hatufurahii kuona nchi haisongi mbele. Mimi nataka hata posho za Wabunge zishuke.
 
Yawezekana waziri asiwepo lakini utaratibu ukafuatwa
Na waziri anaweza kuwepo na utaratibu usifuatwe vilevile


Kwani huo mkataba wenyewe unasemaje🤔🤔
Upo sahihi kabisa, pia yawezekana walishiriki kikamilifu katika maandalizi yake, na wameenda wasaidizi wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…