Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Baadhi ya kauli ambazo tumezisikia kutoka kwa Mama Samia na viongozi wengine fulani waliohudumu chini ya JPM zinaonesha kwamba hao viongozi walikuwa wanahubiri na kusimamia wasichokiamini. Kitendo hicho cha kuhubiri na kusimamia wasichokiamini kilikuwa unafiki na utovu mkubwa wa nidhamu kwa wapigakura wa nchi hii. Hili limenikumbusha hata ule utovu wa nidhamu ambao VP na PM waliuonesha wiki nne zilizopita kwa kuwapa wapigakura salaam hewa kutoka kwa Hayati JPM ilhali wakijua JPM alikuwa mahututi ndani ya ICU.

Katika utumishi, sio kitu cha ajabu kuwa na tofauti za kimtazamo juu ya jambo fulani. Hata hivyo, inapotokea kwamba VP au waziri anaamini tofauti za kimtazamo zilizopo kati yake na Rais, juu ya jambo hilo, ni kubwa sana na hazivumiliki endapo Rais atakataa ushauri wake, basi ni bora akajitenga na msimamo wa Rais kwa kujiuzulu.

VP au Waziri akishindwa kujitenga na kitu ambacho anaamini kinaumiza maslahi ya taifa, VP au waziri huyo anakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi. Kiongozi lazima awe na ujasiri wa kusimama upande wa haki hata kama kufanya hivyo maana yake ni kupoteza kazi. Vinginevyo, huyo hafai kabisa kushika dhamana kubwa kama hiyo.

Needless to say, VP au Waziri anayehubiri na kusimamia asichokiamini hawezi hata kuweka kiasi sahihi cha juhudi inayohitajika kufikia malengo yaliyotarajiwa. Kwa maneno mengine, yeye anageuka kuwa VP au waziri mzigo.

Mama Samia ameonesha udhaifu wa kiwango cha PhD na amekuwa mfano mbaya kabisa kwa mawaziri wake. Bila shaka, Rais anawaambia mawaziri na taifa zima kwamba unafiki katika Serikali unakubalika. Yumukini mfano wa unafiki aliouonesha ni silaha ambayo wateule wake hawatasita kuitumia dhidi yake. Inasikitisha, to say the least!
Wtz hatjui tunataka nn, kwhyo unataka mama akopi njia za hayati..
Fanya we ukiona bi mkubwa anakosea ebooo ....
Ukizingua tutazinguana , nasema uongo ndugu zangu
 
Huyu mama ataongoza kama kiongozi wa kawaida.

Sidhani kama ana vision.

ie anataka kutupeleka wapi katika levo za kiuchumi.

Hatutaki kwenda huo Uchumi wa Juu wa kinafiki ambao taarifa yake inaishia kwenye Makaratasi na sio hali halisi ya Wananchi.
 
Mkuu watu ni wajinga sana..hawajui wananchi wanahitaji nini na mama nae kafuata huo huo mkumbo..sio kwa zile hotuba zake yaan hata kuziskiliza ni kero..anataka turudi enzi za kina jk.kuchekeana chekeana.. hatutaki uswahili kwenye masuala ya kulipa kodi kwenye masuala ya rasilimali za nchi..
Time will tell..JPM will never be forgoten.
Unavyosema uswahili unamaanisha nini? Inmaana sisi waswahili waswahili hatustahili kuongoza hii nchi? Au hatuna akili?

Uhuru wa nchi hii umeletwa na hao unaowaita waswahili wakati babu zako hawajui Dar ipo upande gani.
 
Huyu mama ataongoza kama kiongozi wa kawaida.

Sidhani kama ana vision.

ie anataka kutupeleka wapi katika levo za kiuchumi.
Mkuu mimi nadhani wewe ndio huna vision sio mama mnazungumzia level za uchumi wa kwenye makaratasi wakati umasikini umekua Kama ngozi na damu haviachani...
 
Hao ndio ccm....unafiki, uongo na kila aina ya uovu.... Kwa nini hukuandika kirahisi tu kuwa samia ni mbobezi mwenzako na magufuli waliohitimu kwa unafiki?! Kwa sababu...magufuli akiwa waziri alisimamia kipi alichokiamini?!
 
Mtaweweseka sana

Bisha kwa hoja! Ni uamuzi gani mgumu hawa wengine wamewahi kufanya?

Hata 2015 NEC meeting kwa ajili ya nomination ya CCM presidential candidate tu JKM ilimshinda mpaka BWM akalazimika kuokoa jahazi!
 
Acha unafiki wewe. Yaan JK imshinde kuchagua. We hujui nguvu ya mwenyekiti wa CCM. RAIS SAMIA ATAKUWA KIONGOZI BORA KULIKO YULE MAREHEMU.
 
Hahahahaaahaha ila Polepole alisema CCM itatawala zaidi ya miaka 100
Unafiki wake nini, mbona hayati nae alikuwa hivo hivo wakati anamuambia JK asafir tu ili alete mahela, alivoingia unakumbuka akasemaje na akatendaje?

Mtateseka sana, nchi imechukuliwa na CDM kiulaini bila hata push up yani.
 
Sio kweli amejifunua bayana kwamba hakukubaliana na nmna alivyokuwa anawaongoza ila haijulikani ni kwanini hakujiuzulu kujenga heshima iliyo bora kuliko kumsema vibaya marehemu ambaye kwa sasa hana kauli ya kujitetea kutokana na kile anachokiagiza sasa hivi kufanyika. Amesikika akisema ataunda tume kufanya utafiti kama wakubali au kukataa kupokea chanjo ya UVIKO wakati akijua kabisa hayati alishaunda tume hiyo tayari kufanya utafiti huo na majibu wayawakilishe kwenye mamlaka husika kwa hatua kama sio kudhoofisha urithi (undermining legacy) huo ni nini ambao na yeye alikuwa sehemu yake?

Je, walikuwa na uadui baridi wakiviziana kwa muda mrefu ili tujue na yeye ashauri kuwa makini na washauri wa karibu ndio humpoteza kiongozi?
Mwendazake amemaliza mwendo wake, wengi mnaumia kwani vile mlivyozoea sio tena hivyo, kuna umuhimu wa kukubali hali halisi na kusonga mbele kwa kujenga nchi yetu kwa kuitekeleza ilani!!! Kulia lia hakuwezi kumrudisha mwendazake, siku 21 za kuomboleza zimekwisha sasa upende usipende kijiti kimepokewa na Rais Samia ndio anaongoza jamhuri ya Tanzania.
 
Bila kukinga bakuli kwa mabeberu, huyu hana ujanja wa kuendesha hii nchi. Kwa hiyo, atalazimika kufuata masharti yote ya mabeberu!
 
Baadhi ya kauli ambazo tumezisikia kutoka kwa Mama Samia na viongozi wengine fulani waliohudumu chini ya JPM zinaonesha kwamba hao viongozi walikuwa wanahubiri na kusimamia wasichokiamini. Kitendo hicho cha kuhubiri na kusimamia wasichokiamini kilikuwa unafiki na utovu mkubwa wa nidhamu kwa wapigakura wa nchi hii. Hili limenikumbusha hata ule utovu wa nidhamu ambao VP na PM waliuonesha wiki nne zilizopita kwa kuwapa wapigakura salaam hewa kutoka kwa Hayati JPM ilhali wakijua JPM alikuwa mahututi ndani ya ICU.

Katika utumishi, sio kitu cha ajabu kuwa na tofauti za kimtazamo juu ya jambo fulani. Hata hivyo, inapotokea kwamba VP au waziri anaamini tofauti za kimtazamo zilizopo kati yake na Rais, juu ya jambo hilo, ni kubwa sana na hazivumiliki endapo Rais atakataa ushauri wake, basi ni bora akajitenga na msimamo wa Rais kwa kujiuzulu.

VP au Waziri akishindwa kujitenga na kitu ambacho anaamini kinaumiza maslahi ya taifa, VP au waziri huyo anakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi. Kiongozi lazima awe na ujasiri wa kusimama upande wa haki hata kama kufanya hivyo maana yake ni kupoteza kazi. Vinginevyo, huyo hafai kabisa kushika dhamana kubwa kama hiyo.

Needless to say, VP au Waziri anayehubiri na kusimamia asichokiamini hawezi hata kuweka kiasi sahihi cha juhudi inayohitajika kufikia malengo yaliyotarajiwa. Kwa maneno mengine, yeye anageuka kuwa VP au waziri mzigo.

Mama Samia ameonesha udhaifu wa kiwango cha PhD na amekuwa mfano mbaya kabisa kwa mawaziri wake. Bila shaka, Rais anawaambia mawaziri na taifa zima kwamba unafiki katika Serikali unakubalika. Yumukini mfano wa unafiki aliouonesha ni silaha ambayo wateule wake hawatasita kuitumia dhidi yake. Inasikitisha, to say the least!

Huna unachokijua, Utamlaumu vipi ilhali yeye hakuwa kwenye power? Kama kutakuwa na cha kumlaumu ni wakati huu ambapo yeye ndio top,nadhan mama apewe muda.,

Wakati wa mwendazake sio mama tu alikuwa kimya ata hao kina kigwangala hali ilikuwa hairuhusu

Kama unataka kumpima mama ni kwa hii miaka minne kabla uchaguzi mkuu
 
Ushauri kwa mama apunguze mishe za kuonekana kwenye midia mara kwa mara.... Itamjengea heshima sana.
 
Nchi hii ni mkusanyiko wa watu wa aina zote. Wanafiki, wabaguzi waongo na hata washirikina.

Lakini Rais hastahili kukatisgwa tamaa na watu hawa. Asimame katika haki na ukweli, hawa wasiojitambua wataabika.

Nchi yetu ni lazima ibadilike. Ienende katika uchumi wa kisasa na utawala wa kistaarabu. Hii ninkarne ya watu waliostaarabika, siyo ya watu wanaoswagwa kama ng'ombe. Tulipe kodi, tuhoji, tukosoe, tujadiliane - lakini katika yote tuongozwe na ustaarabu wa kuheshimu utu ja ubinadaku wetu.

Najua fursa za kukwepa kodi na kupiga dili ndiyo aina ya ustaarabu mnayopigania!
 
Huna unachokijua, Utamlaumu vipi ilhali yeye hakuwa kwenye power? Kama kutakuwa na cha kumlaumu ni wakati huu ambapo yeye ndio top,nadhan mama apewe muda.,

Wakati wa mwendazake sio mama tu alikuwa kimya ata hao kina kigwangala hali ilikuwa hairuhusu

Kama unataka kumpima mama ni kwa hii miaka minne kabla uchaguzi mkuu

Kiongozi asiyeweza kusimamia anachokiamini hatufai, kwa sababu “ana tabia ya kimalaya malaya; ananunulika”!
 
Mwendazake amemaliza mwendo wake, wengi mnaumia kwani vile mlivyozoea sio tena hivyo, kuna umuhimu wa kukubali hali halisi na kusonga mbele kwa kujenga nchi yetu kwa kuitekeleza ilani!!! Kulia lia hakuwezi kumrudisha mwendazake, siku 21 za kuomboleza zimekwisha sasa upende usipende kijiti kimepokewa na Rais Samia ndio anaongoza jamhuri ya Tanzania.
Hakuna namna...Tanzania yetu
 
Back
Top Bottom