Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

[
Nyinyi mlitaka mle peke yenu na magenge ya wahuni task force....Nani alikwambia ujambazi au madawa ya kulevya yatarudi? Haujaona tani za sembe zimekamatwa juzi juzi? Wahalifu hawaepukiki ila majambazi dawa yao ni kula vyuma tu na wenyewe wanajua kwamba kwasasa polisi hawataki utani na ujambazi ukizingua na ujambazi wako unakula chuma tu.

Enzi za jiwe ,wapiga pambio na wahuni task force walikuwa na maisha mazuri,sasa ujio wa ssh wanaona wamenyang'anywa tonge mdomoni hivyo wanataka na wengine waendelee kunyanyasika kama enzi za jiwe wakati mama kashakataa fedha za dhuluma.
 
Nadhani hii ni premature conclusion. Mama anafanya safari zenye economic gain na pia kurudisha mahusiano dhabiti ya kimataifa aliyoharibu jpm (rip) na Kabudi
 
Tutegemee mambo mengi toka kwa Rais Samia Suluhu. Mojawapo ni tabia nyingi za aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne Ndugu Jakaya Kikwete.

Safari zitakuwepo nyingi sana na majambazi yatampangia safari nyingi ili yabaki yakiiba pesa za umma. Kuna uwezekano mkubwa sana wa Nchi kusimama.

Lakini faida ni yeye katika kutaka kuwafurahisha watu kwa furaha za muda mfupi huku nchi baadaye ikiingia kwenye majanga

Wauzaji wa madawa ya kulevya na biashara haramu wanaanza kurudi wakiamini sasa watakuwana nafasi ya kuja haribu tena maisha ya watanzania. Mtandao wao unafahamika ulikuwa mkubwa mpaka ndani ya Serikali kuu.

Sijui yeye atakuwa na mtizamo gani katika hilo. Lakini tutegemee maisha yale mazuri ya kipindi cha kikwete katika awamu hii. Ya kila mbuzi kula kutokana na urefu wa kamba yake.

Tofauti na kikwete labda ni kuwa Speeches za huyu mama anaongea kwa utulivu na anakuwa amejipanga. Kikwete hakuwa na mvuto wa kuongea au kusikilizika. Tofauti ya kikwete na magufuli ni kuwa magufuli alikuwa na maneno makali but kikwete maneno yasiyo na maana.

Kama tunapenda speeches nzuri basi tutaendelea kuzipata kila mara. Hizi mama atajitahidi kuendelea kuwa nazo. Na kwa kuwa tulizimiss kila baada ya speech tutampongeza sana kwa kutufariji. Na ni kweli watanzania wanapenda maneno ya faraja. Tuendelee kupata.

Mnaweza kidogo mkachanganyikiwa kwa nlichoandika. But ndani kwenye threads mnaweza pata some points.mengine achana nayo
huyo aliyekuwa hasafiri kasaidia Nini zaidi ya kutuachia Uchumi ulikuwa kwa asilimia 4

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Iliimarika kwenye sekta ipi KWA mfano??

Ufisadi mbona ulikuwa pale pale?deni la Taifa mbona limezid Mara dufu,hali ya maisha mbona ulizid kuwa mbaya zaid??

Biashara na uchumi mbona umedorora, mwendazake bora ametanguliaaa
Bila shaka wewe utakuwa mpinzani mmefumbishwa macho kabisa msione mema yaliyofanyika.Miundombinu iliyojengwa hauioni mkuu? Ndege? SGR? Terminal 3?,stendi mbalimbali?,shule na hospitali zilizojengwa? maboresho huduma ya afya? maboresho sekta ya madini? hayo yote huyaoni? mapato TRA kuongezeka? uchumi kupanda mpaka nafasi ya kati? hauoni? Nidhamu kazini? kupinga uzembe na ufisadi bila kuonea mtu haya? mama aliyepo kule kijijini ndiye anaweza kuona ubora wa maisha kwa kusogezewa huduma ya maji! ila wewe uliyepo mjini ukiishi kwa kupiga dili lazima hali ya maisha utaona ngumu!
 
Mungu anisamehe...hayati Magufuli amefanya mengi mazuri lakini sikuwahi kufurahia utawala wake kamwe.....sitakuja kuutamani naomba Mungu anisaidie katika maisha yangu yoote yalisalia nisipitie utawala kama ule
Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila Jambo.
Niliposikia Magu katutoka, nilihuzunika lkn nilimshukuru Mungu kwani mapenzi yake yalitimizwa.

Usiombe kila Kona na kila wakati Kuna watu wanalia kwa machungu unayowapatia
 
Mwisho wa siku kumpa matumaini makubwa sana Rais ni kujiumiza mwenyewe, atafanya kiasi chake mengine atawaachia wengine mbona wale maadui watatu bado tunao mpaka leo miaka 60 baada ya uhuru.
 
Wagalatia mmeshaanza chuki zenu, muachen mama afanye kazi,kwann mnateseka??yeye hakumchukua jiwe,jiwe limeondoka KWA kudra za mungu,kama hamkubali mwambien Gwajima akamfufue aje aendeleze alipoishia, hamuwez basi tulieni,kelele zenu hazina mashiko
Ukikuta mtu anajiita Mkristo aafu anabagua watu wa dini, dhehebu, kabila,au mtu wa rangi ingine basi jua huyo si Mkristo ni muhuni km walivyo wahuni wengine. Kwa Mungu sote tunaitika km watoto wake. We nani hata umbagua mtu ambaye hujamuumba na duniani tumekutana tu?

Dini ni njia ya kutafuta na kumjua Mungu na dini haibadilishi ubinadamu wetu. Ni wajinga wachache ndio wamezifanya dini ziwe msingi wa kubaguana,kusemana vibaya na hata kupigana.
 
Tutegemee mambo mengi toka kwa Rais Samia Suluhu. Mojawapo ni tabia nyingi za aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne Ndugu Jakaya Kikwete.

Safari zitakuwepo nyingi sana na majambazi yatampangia safari nyingi ili yabaki yakiiba pesa za umma. Kuna uwezekano mkubwa sana wa Nchi kusimama.

Lakini faida ni yeye katika kutaka kuwafurahisha watu kwa furaha za muda mfupi huku nchi baadaye ikiingia kwenye majanga

Wauzaji wa madawa ya kulevya na biashara haramu wanaanza kurudi wakiamini sasa watakuwana nafasi ya kuja haribu tena maisha ya watanzania. Mtandao wao unafahamika ulikuwa mkubwa mpaka ndani ya Serikali kuu.

Sijui yeye atakuwa na mtizamo gani katika hilo. Lakini tutegemee maisha yale mazuri ya kipindi cha kikwete katika awamu hii. Ya kila mbuzi kula kutokana na urefu wa kamba yake.

Tofauti na kikwete labda ni kuwa Speeches za huyu mama anaongea kwa utulivu na anakuwa amejipanga. Kikwete hakuwa na mvuto wa kuongea au kusikilizika. Tofauti ya kikwete na magufuli ni kuwa magufuli alikuwa na maneno makali but kikwete maneno yasiyo na maana.

Kama tunapenda speeches nzuri basi tutaendelea kuzipata kila mara. Hizi mama atajitahidi kuendelea kuwa nazo. Na kwa kuwa tulizimiss kila baada ya speech tutampongeza sana kwa kutufariji. Na ni kweli watanzania wanapenda maneno ya faraja. Tuendelee kupata.

Mnaweza kidogo mkachanganyikiwa kwa nlichoandika. But ndani kwenye threads mnaweza pata some points.mengine achana nayo
Muacheni Mama tuenjoy maisha
 
Huyu mama anavitu vingi vya kurekebisha. Mwendazake hakupaswa kupata kile cheo cha urais, ameua sekta binafsi ambayo ndio walipaji wakuu wa kodi.. NGO nyingi alifunga.
Mwendazake alijiconnect na BOT anashinda anachungulia accounts za makampuni na watu binafsi.. Akitoka hapo ni kukwapua hela za watu.
Hatujawahi kupata kituko cha namna hii hata wawekezaji ilikuwa shida kuja kuwekeza kwenye nchi hii.. Mwacheni mama atafute connection na uwekezaji ili angalau hata mzunguko wa hela urudi
 
Kwani kila awamu ya uongozi lazma uzi wa kuuliza kama huu uwepo?? Mama anatupeleka pazuri sana na tunamwamini.
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Anafuta legacy Mbaya ya mwendazake
 
au mkuu una
Bila shaka wewe utakuwa mpinzani mmefumbishwa macho kabisa msione mema yaliyofanyika.Miundombinu iliyojengwa hauioni mkuu? Ndege? SGR? Terminal 3?,stendi mbalimbali?,shule na hospitali zilizojengwa? maboresho huduma ya afya? maboresho sekta ya madini? hayo yote huyaoni? mapato TRA kuongezeka? uchumi kupanda mpaka nafasi ya kati? hauoni? Nidhamu kazini? kupinga uzembe na ufisadi bila kuonea mtu haya? mama aliyepo kule kijijini ndiye anaweza kuona ubora wa maisha kwa kusogezewa huduma ya maji! ila wewe uliyepo mjini ukiishi kwa kupiga dili lazima hali ya maisha utaona ngumu!
mkuu mbona hujazungumzia ile faida ya bilioni 28 za ATCL zilizopatikana mwezi mmoja tu baada ya kununua ndege (km sijakosea)?!!!!
 
Labda unapotea mwenyewe na wenzio wachache msio elewa ,Samia anatupeleka pazuri , wewe ulitaka atupeleke jela?
 
Back
Top Bottom