Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

ataenda kuzifanyia chato basi, ili amuenzi mungu wenu
Dodoma gharama nyingi zimeisha tumika pale bila kujali mwendazake alifanya alaka au la no way tunaweza tusiendelee mbele ,vinginevyo itakua nikuchezea akili za walipa kodi
 
Mama katutoa kuzimu anatupeleka kaanani
Mitano tena kwa mama,kituo kinachofata Ally Hapi
 
... nitajie hoteli yoyote Dodoma yenye hadhi ya kufikia mkuu wa nchi ya kigeni na msafara wake! Hebu ongeeni kwa facts badala ya kuwaza kwa akili za marehemu!
Hebu acha utani na fikra potofu ,kwamba kama wageni walifikia Chato,enzi za mwendazake ,iweje sema Dodoma hakuna hotel ambayo mkuu wa Nchi awezi fikia , ilihali Dodoma ni jiji na chato ni wilaya acha madhalau mkuu
 
Hebu acha utani na fikra potofu ,kwamba kama wageni walifikia Chato,enzi za mwendazake ,iweje sema Dodoma hakuna hotel ambayo mkuu wa Nchi awezi fikia , ilihali Dodoma ni jiji na chato ni wilaya acha madhalau mkuu
... acha stori nyingi kijana; taja hoteli. Chato walikuwa hawalali zaidi ya kufika na kuondoka.
 
ACHA kudhalilisha jiji la Dodoma,
... labda baadaye sana ila kwa sasa hamna jiji pale zaidi ya siasa. Prince Mohamed bin Salman, the de facto ruler of the Kingdom of Saudi Arabia anaweza kufikia Dodoma? Huwa akiingia mjini anachukua hoteli zote za nyota tano kwa ajili yake na ujumbe wake. Sasa lodge za Dodoma; dah!
 

image.png

Na Nkwazi Mhango​

Si nadra siku hizi kusikia watu–––hasa wateule wake au wale aliowabakiza kwenye ulaji–––wakimwita rais Samia Suluhu Hassan ‘mama yetu’ ili kumfurahisha na kulinda ulaji wao. Kama tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu, je kweli SSH ni mama yetu? Kwangu mimi, SSH ni rais wa JMT basi. Kwanini ninafikiri hivi? Nina sababu zifuatazo:

Mosi, Samia si mama yetu bali rais wetu hasa ikizingatiwa kuwa umama wa taifa haupewi mtu kwa sababu ni rais bali kutokana na mchango wake kama upo. Je tukilinganisha mchango wa SSH na akina Maria Nyerere, mjane wa baba wa taifa au Bi Titi Mohamed, mama aliyepigania uhuru wetu hadi kuathirika kifamilia kwa kuachika na kufungwa tena kwa kusingiziwa kweli tunaweza kusema kwa haki na heshima kuwa SSH ni mama yetu?

Pili, kama ni umama utokanao na urais, inakuwaje watangulizi wake kuanzia Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na Hayati Dkt John Magufuli hawakuitwa baba zetu? Hapa kuna nini au ni ule udhalilishaji wa mfume dume kama siyo tabia ya kujikomba ambayo ilianza kuota mizizi kwenye awamu ya tano tokana na ukali wa Magufuli? Tulizoea kusikia mke wa Magufuli, mama Janet, akiitwa na walipoende kujipendekeza kwa mumewe wakimwiti ‘mama yetu kipenzi’ sifa ambayo imepotea ghafla baada ya mumewe kufariki na kutokuwa madarakani. Je ni kweli mama Janet alikuwa kipenzi au madaraka ya mumewe? Mbona siku hizi tunasikia akiitwa mjane wa Magufuli bila sifa ya kipenzi kuendelea kutajwa kama kweli alikuwa akipendwa kweli? Je kwanini SSH, ghafla amegeuka mama wa kila mmoja wakati alipokuwa makamu wa rais aliitwa jina lake la SSH? Kunani hapa?

Hata hivyo, hili linahitaji wenye kuona mbali na ndani zaidi. Je hawa wanaomwita SSH mama yetu wanamaanisha hivyo au kujikomba na kumzuga aendelee kuwabakisha kwenye ulaji? Je––kama tutafuata vigezo––SSH anastahiki heshima ya mama yetu ambayo kwa maana nyingine ni mama wa taifa wakati mataifa karibu yote–––tokana na mfumo dume–––huwa hayana mama wa taifa isipokuwa baba wa taifa?

Kwa kujua tabia ya kujikomba inayoendana na madaraka, namshauri rais SSH akemee utapeli huu usiokuwa na sababu yoyote bali kujikomba na kumpumbaza na kumdanganya adhani wanampenda wakati si kweli. Hebu fikiria. Alipokuwa madarakani, Dkt Magufuli alikuwa akisema kila jambo na kuungwa mkono huku waliomzunguka wakimsifia na kujichekesha ilhali walikuwa wanalenga kumtumia na kumfurahisha ili wanusurike. Ukiangalia kwa sasa ambapo wale waliokuwa wakijifanya watu wake walivyomgeuka na kuanza kubomoa mema yake, utajua ninachomaanisha.

Mfano wa karibu ni ile hali ya baadhi ya waliokuwa karibu naye kuanza kutetea bila aibu mambo ya aibu ana ajabu kama vile mradi mbovu wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo Hayati Magufuli alipiga kalam una kutamka wazi kuwa hata mwendawazimu asingeweza kuuruhusu. Mbali na hiyo, rejea kubadilika kwa ghafla kwa wapiganaji wa miamvuli waliotuaminisha kuwa taifa letu lilikuwa hali corona na lilikuwa likilindwa na Mungu kiasi cha kutovaa mabarakoa kwa vile Hayati Magufuli aliyapinga wanavyovaa mabarakoa. Je huu si ushahidi wa unafiki na imani za woga?

Sina ugomvi na kuwepo kwa corona. Je kwanini mliokuwa mmezunguka Hayati Magufuli hamkumshauri au kuachia ngazi pale alipokuwa ameshikilia msimamo kuwa tulihitaji kinga ya Mungu na si barakoa na chanjo?

Taifa letu ni ajabu kidogo. Ilifikia mahali watu wanajua kabisa kuwa walikuwa wakihatarisha afya zao na wengine ilmradi waendelee kuwa madarakani wasijue wangeweza kufa na kuyaacha. Kwa kuzingatia tabia hii ya ajabu na hovyo, namshauri rais SSH asikubali kuitwa mama yetu wakati wanaomuita hivyo wapo wanawake wenye umri mkubwa kuliko yeye ukiachia mbali wanaume wanaoweza kumzaa. Nisisitize. Tuwe wakweli kwa nafsi zetu badala ya kuendekeza njaa na unafiki. Tunawapotosha viongozi na wananchi wetu.

Tokana tabia hii ya kinyonga, nachelea kuwa baadhi ya mambo aliyokataza Hayati Magufuli yanaweza kurejea taratibu kama vile safari za hasara na hovyo za maafisa wa serikali nje, matumizi mabaya, wizi, uzembe na mengine mengi. Rejea kadhia ya hivi karibuni ambapo wadau wa bandari walivyosikika kwenye mitandao wakilalamika kuwa bandari imerejea ujahiri wa awali ukiachia mbali wizi hata ujambazi kuanza kuibuka hata kabla ya Hayati Magufuli hajaoza.

Biblia ina maneno ya busara yasemayo ajikwezaye atashushwa. Pia tuongezee kuwa akubalie kukwezwa asipostahili atashushwa na wale wale wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa au kumtwisha kiremba cha ukoko. Namshauri rais SSH ajikumbushe kisa cha Yesu siku ya matawi alipoingia Jerusalem akiwa amepandishwa kwenye mgongo wa punda huku wanawake wakitandika khanga zao na wengine matawi ili apite. Je alipokamatwa, watu wale wale walisema? Walisema “asulubiwe” hata bila makosa. Kumbuka.

Kabla––kwa mujibu wa biblia––Yesu aliweza kulisha umati pale alipobadili samaki sita na vipande vya mikate watu wakala na kusaza. Ajabu, baada ya hapo, ni wanufaika wale wale walisema bila aibu wala woga asulubiwe.

Mfano mwingine ni wa Musa. Alipowatoa wana wa Israeli Misri alishangiliwa sana. Cha ajabu, akiwa jangwani njiani kuelekea Kanani, walimgeuka wakakufuru wakisema walikuwa wamechoshwa na mana na pia walitaka wamuone Mungu vinginevyo wangemuua Musa. Mfano mwingine ni wa baba wa taifa. Alipokuwa kitini walimwimbia mapambio, ngonjera na nyimbo zote za sifa. Alipostaafu walimwita ‘Baba aambiliki” wakati walikuwa wakigwaya kumwambia zaidi ya kumsifu hadi wakaja na kile kilichoitwa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM. Je zilidumu au zimeishia wapi baada ya yeye kuishia? Hawa ndiyo wanadamu. Hawana tofauti na ndege kwenye mti wenye matunda. Yakiishia, nao wanaishia bila hata kugeuka nyuma kama ambavyo kwa sasa naona wakimpa kichogo Hayati Magufuli ambaye amebakiza wanyonge wake tu ila siyo wale walioshiba mikononi mwake.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa ukiwa na madaraka, ulaji au utajiri na nguvu watakusifia. Zana hizi zikishakutoka waliokuwa wakijifanya kukupenda wanakuponda. Waliokuwa wakikweza wanakushusha na kukushua. Jifunzeni toka kwa Hayati Magufuli na yanayoendelea. Leo sisemi mengi zaidi ya kuuliza tena.

Je kweli SSH ni mama yetu au rais wetu? Je anahitaji sifa hii kweli? Namshauri SSH akatae unafiki na unywanywa wa kutaka kuingizwa mkenge na wasaka tonge na wachumia tumbo ambao wako tayari kucheza ngoma yoyote ilmradi tonge liende kinywani.
NAUNGA MKONO HOJA KWA 100% MKUU.
Hapa mleta hoja umeweka ukweli tupu bila kupepesa macho kabisa!

UNAFIKI ni janga la kitaifa kwa sasa!
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Nadhani ni jambo ambalo halihitaji kutumia akili nyingi. Dodoma hakuna international airport so mgeni anatua Dar na ni mji wa kibiashara na tuna ikulu pia kwa nini ashuke dar then aanze safari ya Dodoma tena hata kama ni kwa kuunganisha local flight? Hii sio sawa.

Ndio maana wageni wa kimataifa wanaokuja kwenye ishu za UN wanatua KIA then Arusha fasta, solution ni kujenga international airport pale Dodoma itakuwa easy wao kuja straight Dodoma.

Lakini pia jamani Dar pazuri bwana kushinda Dodoma wacha waishie mjini kwakweli, kule kwa Ndugai bado shamba aisee wacha tufiche kaumasikini .
 
Hela ya kumalizia bwawa la umeme unaona sio jambo la msingi maana ametoa zaidi ya bilioni 580, hela ya Daraja la busisi, hela ya kujenga phase 3 ya reli ya SGR? Hela alizopeleka Halmashauri? Hela alizoidhinisha za kununua madawa? Tuwe makini basi.
Hela za serikali huidhinishwa na Bunge, halafu rais ni masimamizi tu. Kazi ya rais na serikali yake ni kupeleka maombi bungeni wakati wa bajeti, bunge likishapitisha basi anabaki kuzisimamia tu zisitumike vibaya; ni kweli angeweza kuzitumia vibaya kwa kuzipeleka kusikohusika lakini sidhani ingekuwa ni busara kwake kwa sababu tayari miradi ilishapewa popularity sana na fedha zilzokuwa zimeidhinishwa kwenye miradi hiyo zilikuwa documented vizuri. Ni hela zinatokana na bajeti ya mwaka jana; tusubiri sasa bajeti ya mwaka huu iidhinishwe ndipo tuone kaomba kiasi gani kwa ajili ya miradi hiyo kwa mwaka unaofuata na miradi itasimiwaje.
 
So kwa akili yako miradi ya Chato nayo ataendeleza? Hata daraja la Busisi tunapiga chini kwanza
Nakerwa Sana na watu wanaodharau umuhimu wa daraja la Busisi. Daraja hili Ni kiungo kati ya Mwanza na mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma. Ndio unaifungua Mwanza na kuiunganisha na Nchi za Congo, Rwanda na Burundi kwa njia ya mkato au rahisi bila kuvuka maji na pantoni. Wakati ule Mimi nakaa kahama, nilipita njia Ile mara Moja tu lakini amini nakuambia tulitumia masaa matatu kusubiria kuvuka kwa pantoni umbali wa kilomita 3 tu . Hebu shika ramani uangalie jinsi gari kutoka Kigoma zinavozunguka kutokea nyakanazi kupita kahama, Shinyanga ndo wafike Mwanza. Gari zingine kwa kuchagizwa na lami wanapita, Tabora, Nzega, Shinyanga. Kwa kweli Ni mpumbavu tu au asiyejua jiografia hii ndio atahoji umuhimu wa hili Daraja, tusiwaamini Sana wanasiasa... WANATUINGIZA CHAKA SANA.
 
Ww unaempinga mama, labda tukuulize maovu aliyotufanyia jiwe hukuyaona? Unasema cheap popularity, kuna mtu alikua anapenda cheap popularity na masifa ya kijinga kama jiwe? Ebu jaman tuwe na kaaibu basi. Saiv ni muda wetu kutesa kwa zamu. Mlitunanga, mkatutukana na kutupiga na kutuumiza mkimtetea dikteta wenu, sasa kafa mmebaki wenyewe kama digidig hamjui mwende wapi.

Tulianza na Bashiru, polepole baadae Sabaya, na sasa Chalaila. Next point ni Happy na mwigulu. Tumempa li wizara gumu ili aboronge tumchomoe kama samaki bwawani mpaka wapambe uchwara wa dikteta wote waishe. Shenzi sana nyie.

Mama apige kazi wala asiwe na shaka, sisi tuko tunamlinda kwa wivu mkubwa sana. Hata tusipokua na hela ila angalau kuna uhuru wa kuongea na kazikazi zinapatikana mtaani kuliko kipindi kile kazi zinapayikana chato u na ndugu zake wakawa ndo wanufaika.
 
Utilize majibu yako wazi.
Anatuondolea wale wa mwenda kwa malaika aka OLE Saa Mbaya Mzee wa viboko shuleni na wengine wanakuja tulizana utaelewa.!
 
8. Anajenga reli SGR kipande Cha Isaka - Mwanza (keshatoa zaidi yaBill. 350)
9. Anapandisha madaraja watumishi 92,000 mchakato unaendelea.
10.Ameshatoa fedha kujenga barabara za kimkakati zinazounganisha mikoa zaidi ya kilometer 1,500 (hizi zilikwama)
11.Ameshatangaza ajira mpya zaidi ya 42,000. Elfu kumi tayari vibali vimeshatolewa
12.Ameondoa faida Kandamizi ya Bodi ya mikopo (Retention fee) ya asilimia sita kila Mwaka katika Deni la la mkopo wa kusoma chuo.
13.Ameondoa faini ya Bodi ya mikopo ya 10% ukichelewa kurejesha.
14. Anamalizia SGR kipande Cha Dar- Moro. Ujenzi unaendelea.
15. Anajenga SGR kipande Cha Dodoma Makutopola Ujenzi unaendelea.
16. Ameanzisha mradi wa kufua umeme mto Malagalasi tayarizaidi ya bill.100 zimeshatolewa.
17. Anaendeleza Ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa JK Nyerere Rufiji.
18. Anarudisha nidhamu ya utendaji unaozingatia sheria kwa viongozi wa umma (Wapuuzi,waigizaji,commedian na chawa wawili wameshaondolewa na mmojawao yupo mahakamani)
19. Anarejesha mahusiano ya kidiplomasia,kiuchumi na mataifa ya nje. Tayari mahindi,maharage,pamba nk yameanza kupanda bei.
Afadhali ww umetusaidia kuorodhesha maana hawa pushgang wanataka kutumaliza na ujinga wao.
 
Hela ya kumalizia bwawa la umeme unaona sio jambo la msingi maana ametoa zaidi ya bilioni 580, hela ya Daraja la busisi, hela ya kujenga phase 3 ya reli ya SGR? Hela alizopeleka Halmashauri? Hela alizoidhinisha za kununua madawa? Tuwe makini basi.
Mtanzania anachojua ni kukosoa tu, kuonyesha kasoro zipo wapi. Huwa hana kabisa shukrani.

Kumlaumu Rais Samia ni wajibu wa kila mtu, ila akifanya jema utasikia anatimiza wajibu wake!!. Poor mindset.
 
Hii awamu kweli ni ya sita sio ya tano kama wengine walivyofikiri kwa kua kura ni za mpendwa wao magufuli.
Watu hazina kuona hakuna magufuli wamepiga hela kwa mwezi mmoja mabilioni kama sherehe. Waziri mkuu majaliwa kaishia kufoka hatuoni hatua yoyote kuengua fisadi hadi sasa.

Tumesikia waziri wa fedha akiwasilisha bajeti huku akitoa pambio kumsifu mama eti ana kadi rangi zote. Jpm alitembeza kadi nyekundu kwa wezi na wabadhirifu maana hawa hawahitaji kadi tofauti. Hii kitu ilileta tija na nidhamu.

Sasa mama yetu hazina hela zinaliwa ovyo pale hutoi kadi nyekundu huku mtu karopoka kama kawaida yake ndio unamtimua kupata nafasi kupanga line yako ya watu.

Magufulists tupo hatuendi popote kuona nini mama anafanya.
 
Mama mwepesi hana jipya yeye na msoga wake,dotto james,dk bashiru,dk mchembe,kakonko,mfugale hawa ni majambazi sugu wa pesa za watanzania.

Wako wanadunda mtaani tu na magari ya serikali..jicho nyanya hamudu hicho kiti ni katiba imembeba tu,anachoweza ni kushona nguo mpya kila siku
 
Back
Top Bottom