Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Usikonde mkuu. Kumwunga mkono mtu hakuna maana ya kuwa chawa.

Nilimwunga mkono na wengi tulimwunga mkono lakini hatukuwa vyawa wake (aione hii taslimu bwana Jumbe Brown Mzanzibara wa pale Mkunazini).


Mama Samia kabadilika baada ya zile sifa za siku 100. Akapandisha mabega na kuona kumbe yeye alifaa zaidi kuwa ndiye mnene mwenyewe hata enzi za uwepo wa mwendazake. Kwamba kumbe mwendazake alipaswa kuwa kidampa tu 😂😂😂😂😂!

Hiiiiii bagosha
John Pambalu ndio ameianza safari ya kuwepo rumande. Mdude Nyagali yuko nje mkuu wangu.

Mimi ni "mbara" sina tone la damu la huko MKUNAZINI kaka 🤣

Mama SSH ana nia njema ya kuwatumikia watanzania kwa moyo mweupeee.....tatizo liko kwenu na siasa zenu za "tug of war"!!

Yashilaga guukuu!
 
Kanda ya ziwa hadi wazee hawataki hata kumsikia huyo Samia..hawamwelewi kabisaaaaaa
 
Ujinga ni wako mwenyewe

Bado hujajitambua

Mh. SSH ni rais wetu, jukumu lake la kwanza ni KUILINDA TANZANIA DHIDI YA MACHAFUKO, VURUGU, UGAIDI NA UASI.

Tunaojitambua TULIMUUNGA MKONO SIKU ZAKE ZA MWANZO.

Tunaendelea kumuunga mkono.

Akigombea 2025 tutampigia kampeni in shaa Allah na TUTAKWENDA VITUONI KUMCHAGUA KWA KURA ZA SUNAMI.

ENDELEA kuishi kwa KUOTA NDOTO ZA ALINACHA!

#KaziInaendelea
#NchiKwanza
#JMTMilele
 
Kawaida yenu kukurupuka

Wakuu,

Kama mtaniita mzee wa kukurupuka ni sawa tu maana niliyataka mwenyewe. Nilimuunga mkono Rais Samia bila kufanya uchunguzi wa kina, kiukweli kiongozi yeyote anaetumia uongozi wake kuumiza wengine kwa namna yeyote ile mimi hua sipo upande wake na kamwe simuungi mkono.

Nilifanya hivo kwa mwendazake na kwa huyu ni hivo hivo kwahiyo najitokeza hadharani kusema kua kwa matendo machache tu na yanayoumiza watu aliyofanya toka kaingia madarakani nasema mimi sipo upande wake kabisa hivo waliodhani vinginevo hapana nimeshtuka nimeshtuka nae ni walewale tu.
 
John Pambalu ndio ameianza safari ya kuwepo rumande....Mdude Nyagali yuko nje mkuu wangu.....

Mimi ni "mbara" sina tone la damu la huko MKUNAZINI kaka 🤣

Mama SSH ana nia njema ya kuwatumikia watanzania kwa moyo mweupeee.....tatizo liko kwenu na siasa zenu za "tug of war"!!

Yashilaga guukuu!
John Pambalu ndio ameianza safari ya kuwepo rumande....Mdude Nyagali yuko nje mkuu wangu.....

Mimi ni "mbara" sina tone la damu la huko MKUNAZINI kaka 🤣

Mama SSH ana nia njema ya kuwatumikia watanzania kwa moyo mweupeee.....tatizo liko kwenu na siasa zenu za "tug of war"!!

Yashilaga guukuu!

Mbona kujishuku? Nimekutambua sahihi kabisa kama Mzanzibara (parejee kujiridhisha).

Nisiache kukunong'oneza - "Mama Samia katukwaza sana kwenye hili la kubambikiziana kesi." Mjini wanasema katu kata stimu kabisa," wengi tuliokuwa tukimwunga mkono.

Kulikuwa na misukumo ya kudai kuendelezea sasa rais wa JMT - Mzanzibari tosha!

Nini kimebadilika?

Nisiache kukwambia ewe chawa wake kuwa "hili amelikoroga kweli kweli!"

Mkipenda mmwambie kama anataka kulimaliza kama vipi:

"Amwone JK haraka sana ili kupata maujanja ya haraka haraka. Muelekeo sahihi ukiwa - kuwaachia makamanda wote mara moja na bila ya masharti yoyote. Hiyo kama hatua ya mwanzo kwenye kujisafisha kwa mwenyewe kwa brush ya waya."

Asiache kuwapata Mbagusiro wake wawili watatu wa kubebesha jumba bovu kuwa yeye hakuwatuma.

Mkipenda endeleeni kujidanganya.

Uamuzi ni wenu.
 
Anatupeleka uchumi wa kati na kazi inaendelea kama mwanzo.Si ndiyo ndugu zangu?!
 
Heshima sana wanajamvi,

Miezi minne iliyopita tulisajili kiungo mshambuliaji ambaye alionyesha uwezo mkubwa wa kufunga magoli,kukaba na kutoa pasi za uhakika.Kifupi kiungo mshumbuliaji kakamilika kila idara ukipenda waweza kusema pasipo shaka anaupiga MWINGI.Team kadhaa kubwa zilijaribu kumnasa kwa ahadi luluki na nono.Kiungo Mshambulia aliweza kufunga magoli ya mbali na kutoa pasi zenye macho ambazo zilisababisha magoli heka heka nyingi langoni mwa team pinzani.

Sijui nini kimemsibu kiungo mshambuliaji kimemsibu,mara kadhaa kabaki yeye na kipa anapaiza mipira juzi ndio ilikuwa balaa yaani kabaki peke yake golikipa kaanguka goli lipo wazi hakuna beki wala nini kapaiza mpira juu ya lango!.Tatizo nini au sifa zilizidi tumebaki tunashangaa na kujiuliza maswali mengi pasipo jibu hata kiduchu.
 
Amegundua kuwa alikuwa anapiga square na back passes nyingi sana, sasa ameamua apeleke moto kwa wapinzani kwa kupiga final penetrating passes
 
Huku nyuma niliwahi kusema, Mama Samia is a breathe of fresh air!

Lakini sasa hili sakata la Mbowe limeleta uvundo wenye harufu ya Mwendazake.

Nikiri, mimi ni mwana CCM, siwafagilii wapinzani, lakini nchi hii ni ya vyama vingi, katiba hsijabadilika.

Kuna yale wapinzani wanayasema yana ukweli wa kuyafanyia kazi.

Narudia, sajata la Mbowe mama litakuadhiri na kukuvunia heshima iliyoanza kujengeka.
 
heshima ya mama iko palepale huwezi kuendesha nchi kwa kuangalia upepo yaani chadema wakisema hivi unafanya cuf wakisema hivi unafanya mwisho watasema tuishe ytuongoze nchi yani hapo ndiyo panatakiwa akaze uzi kabisa mpaka waseme poo
 
heshima ya mama iko palepale huwezi kuendesha nchi kwa kuangalia upepo yaani chadema wakisema hivi unafanya cuf wakisema hivi unafanya mwisho watasema tuishe ytuongoze nchi yani hapo ndiyo panatakiwa akaze uzi kabisa mpaka waseme poo
Hivyo vyama havifuati sheria?Huo upepo mnaujua?
Muogopeni Mungu
 
Back
Top Bottom