Hapa nazungumzia PM na VP ambaye amekuwa Rais. Kwenye siasa akili ni kuchagua wasaidizi wa karibu ambao ni Loyal(wafuasi wazuri) na si wenye weledi (competent). Lengo ni kupata watu utaoweza kuwaelekeza mambo na wakafuata.
Na mara nyingi watu competent huwa siyo wafuasi wazuri. Watu wanaoweza kufikiri wenyewe huwa siyo wafuasi wazuri. Hivyo basi, viongozi wakubwa, hasa wale wanaoongoza kibabe huwa na na wasaidizi dhaifu ila loyal sana.
Kwa mantiki hii, Rais Magufuli kama Rais katuachia uongozi mbovu. Na hata CCM alikokuwa mwenyekiti, pale juu aliacha uongozi dhaifu automatically.