Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Lengo kuu ni kukuza uchumi kupitia uwekezaji kwenye sekta binafsi
Kushirikiana na sekta binafsi kufanya miradi (PPP)
Sekta binafsi itakuza ajira na kuongeza makusanyo ya kodi

Kikwazo kikubwa kwa Samia ni hii miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli bila step
 
mimi sioni mzee , kwangu sifa ya uchumi ni watu kuwa na pesa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi , hasa sioni chochote kinachobadilika ,zaidi naona mfumuko tu wa bei, kila aliye kwenye nafasi kuniomba rushwa ninapofanya biashara zangu na wateja kulalamika hali ngumu walizinazo
Dah! kumbe umekuja na majibu yako mfukoni
 
Lengo kuu ni kukuza uchumi kupitia uwekezaji
Wewe kwa imani yako unaamini taarifa za TIC kuwa saizi wawekezaji wengi? Mtu gani mjinga anaweza akawekeza kwenye nchi ambayo umeme na system umejaa ufisadi!?
Unaowasikia hao wengi ni wawekezaji uchwara!
Hakuna kiwanda hata kimoja kilichoanzishwa wala kutangaza chini ya utawala wa awamu ya sita!
 
Samia anaendesha nchi Kama "serikali ya mpito"

Hana vision Wala malengo yoyote. Yeye kaweka watu wake sehemu za Kula na Wanasiasa wapiga kelele kawapa ulaji, Basi.

Na too bad, Hana agenda.

Mwanzoni wakati anaingia madarakani alianzisha siasa za Jinsia ( Ikawa ni wanawake, wanawake, ) naona watu hawazielewi.

Akaja na siasa na Machief, kelele nyingi watu hawazielewi.

Sasa hivi, anazungumzia 4R hata mwenyewe sidhani Kama anajua ni Nini. Ila kwa mtazamo wa haraka haraka naona, ni siasa za kuziba nyufa. Kila anayepiga kelele, mtupie kipande Cha mkate.
Wewe ndio umeshindwa kuiona vision
Halafu mada inauliza kuhusu malengo ya kiuchumi, wewe umeongelea siasa
 
Wewe kwa imani yako unaamini taarifa za TIC kuwa saizi wawekezaji wengi? Mtu gani mjinga anaweza akawekeza kwenye nchi ambayo umeme na system umejaa ufisadi!?
Unaowasikia hao wengi ni wawekezaji uchwara!
Hakuna kiwanda hata kimoja kilichoanzishwa wala kutangaza chini ya utawala wa awamu ya sita!
Okay, wewe unayepinga ungekuja na takwimu mbadala ambazo zipo verifiable
 
Lengo kuu ni kukuza uchumi kupitia uwekezaji kwenye sekta binafsi
Kushirikiana na sekta binafsi kufanya miradi (PPP)
Sekta binafsi itakuza ajira na kuongeza makusanyo ya kodi

Kikwazo kikubwa kwa Samia ni hii miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli bila step
Mkuu hebu taja mradi ambao Magufuli aliuanzisha bila step.
 
Wewe ndio umeshindwa kuiona vision
Halafu mada inauliza kuhusu malengo ya kiuchumi, wewe umeongelea siasa
Hakuna malengo ya kiuchimi mkuu! Tuendelee kufarijiana tu!
Lini Samia umemsikia akisisitiza mambo ya viwanda kama mwenzie alivokuwa akifanya ?
Alteast uliona kabisa ujenzi wa viwanda kama Bagamoyo Sugar na vinginevyo!
Ila huyu yeye anachojua ni kukopa sio yeye ila ni tabia ta wanawake ndio maana hata vikoba vinawatesa sana!
 
Viwanda havijengwi kwa kupiga makelele jukwaani, bali ni mikakati n sera rafiki

Kiwanda cha Bagamoyo sio cha kwanza Bakhressa kujenga, alijenga viwanda vingi kipindi cha Kikwete, kwani ni kwa kupiga kelele au sera?
 
Kelele ndio nini? Unajua viwanda vingi vilivilo jengwa huko Pwani? Bila kuwaeleza watu na kiwa na vision unafikiri watakuja tu?
Mbona juzi Mama Samia kafanya Royal tour lengi si kupiga kelele uonekane?
Acha visingizio there is no fucking Vision on her!
 
Hali ngumu unayo wewe tu, wengine hela tunazo na mambo yanaenda, kwani lini uliona uchumi unaenda vizuri?
wewe una hela ! hebu sema kitu kimoja ambacho umekifanya kinaonyesha una pesa , kwa mfano mimi pamoja na kutokuwa na pesa na hali yangu kuwa mbaya nipo najenga hostel eneo la airport - mbeya, lengo ni wanafunzi wa vyuo vya TIA, TEKU na SAUT walale hapo, sasa wewe tajili sema mradi wako mmoja ambao unatambulika tu kwenye jamiii na location ulipo ili tuone una hela
 
Kelele ndio nini? Unajua viwanda vingi vilivilo jengwa huko Pwani? Bila kuwaeleza watu na kiwa na vision unafikiri watakuja tu?
Mbona juzi Mama Samia kafanya Royal tour lengi si kupiga kelele uonekane?
Acha visingizio there is no fucking Vision on her!
Royal Tour ndio mikakati sasa, action bila makelele,
Yule alikuwa akipiga makelele viwanda, viwanda, viwanda, baadae yakamshinda akadai cherehani 4 ni kiwanda
 
Niyo Royal tour ndi inaiona ya maana? Wewe una chuki zako tu za kijinga huna lolote!
 
Ningekupa matokeo ya Royal Tour kwenye utalii ila tatizo ukipewa takwimu unasema ni za kupika

Sasa wewe kumkosoa Samia unaona ni sawa ila kumkosoa Magufuli unaona ni chuki?
 
Mnaojua lengo hasa la samia kwenye uchumi wa Tanzania, njooni mtuambie hapa, mimi sielwei elewi kabisa naona hakuna kinachoendelea.
,Hilo jibu aje nalo Madelu Mburundi wa Singida, 'They are running a minority economy with excess self enrichment'
 
Mnaojua lengo hasa la samia kwenye uchumi wa Tanzania, njooni mtuambie hapa, mimi sielwei elewi kabisa naona hakuna kinachoendelea.
Kwa kifupi Bibi hana vision,kashachemka ila kwasababu anaongoza taifa la wanafiki ndiyo maana anadunda Ikulu mpaka sasa.
 
Malengo ya kiuchumi yaatokana na vision ya uongozi wake unaotokana na siasa zake.
siasa ni jinsi ya kufanya aongoze kirahisi, kupunguza resistance

Mikakati ya uchumi ataitekeleza vizuri baada ya kupunguza resistance,

Ambapo hadi sasa amefanikiwa kuongoza kirahisi kuliko mtangulizi wake
 
Back
Top Bottom