Habari za jumapili.
Niko busy kidogo kwenye ujenzi wa taifa uku Mwanza, ila shughuri zangu zinanifanya nisafiri sana mikoa ya hapa kanda ya ziwa.
Uku kipindi cha nyuma, Samia angalau raia walikuwa wanamnena kwa mazuri.
Sasahivi hali imebadirika sana, sijui ni uku au hata uko kwenu wakuu hali ipo hivyo? Yaani kitaa watu sahivi hawamuelewi Samia, yaani hawamuelewi ata kidogo. Kisa eti anauza mali za Tanganyika kwa waarabu.
2025 Samia ana kazi kubwa sana kuvuna kura mikoa ya; Mwanza,Kagera,Mara,Geita,Shinyanga na Simiyu.
Mimi binafsi, nilikuwa miongoni mwa waliokuwa wakimpongeza Rais Samia katika mambo mengi lakini kwenye hili la bandari, kwa kweli amenikwaza sana, na siyo pekee yangu. Kwa watu wale ambao nina uwezo wa kuwafikia, sijaona hata mmoja anayemwunga mkono kwenye hilo.
Ndiyo hivyo, ule msemo wa Kiswahili kuwa kamba hukatikia pembamba, swala la kuruhusu uporwaji wa bandari, ndiyo wembamba wa kamba ya Rais Samia. Kama ulikuwa ni uamuzi na mapenzi yake binafsi kuikomoa Tanganyika, hawezi kujutia, ila kama alishauriwa na watu wengine, bandari hataisahau maisha yake yote.
Sula la bandari limewafanya watu kujiuliza maswali mengi:
1) Kwenye kitu ambacho nchi haina faida nacho, anataka kifanyike kwaajili ya faida yake binafsi au faida ya watu gani?
2) Je, ina maana hata pale alipokuwa akiwaonesha watu kuwa ana upendo nao, ilikuwa ni hadaa tu, lakini hakuwa na upendo wowote kwa Tanganyika na Watanganyika?
3) Je, anaichukia sana Tanganyika, kiasi cha kuona aikomeshe kwa kuiweka chini ya Waarabu wa Dubai?
4) Je, kuna mpango wa muda mrefu ambao una lengo eneo lote la pwani lichukuliwe na Waarabu? Ikumbukwe kuna kiongozi wa SMZ alikwishawahi kutamka kuwa maeneo yote kuanzia pwani ya bahari, kuingia kilometa 20 ndani ya ardhi ni mali ya Zanzibar kwa sababu hapo zamani maeneo hayo, pamoja na kisiwa cha Kilwa, yalikuwa yanatawaliwa na sultani wa Oman ambaye makao yake makuu yalikuwa Zanzibar.
5) Je, anataka kuitumia Tanganyima kuwatajirisha Wazanzibari? Ikiwa na maana kuwa kuuzwa kwa rasilimali hizi za Tanganyika, malipo yake yanaenda kwa Wazanzibari, ndiyo maana wahusika wote wakuu kwenye syndicate hii ni watu wa Zanzibar. Yaani Wazanzibari wanaiona Tanganyika kama 'kubwa jinga', ambayo wanaiweza kuitumia kuchuma utajiri.