Anayesema Moshi pagumu kwa wageni, ugumu wake ni nini?

@YEHODAYA una CHUKI kubwa sana na wachagga kuanzia na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kumbe hata chuki yako na Chadema ni safu ya chama pale juu kuwa ni ya wacchaga ikiongozwa na Mbowe
 
Una chuki binafsi. Hawaendi Christmas tu wanaenda vipindi vingine vya mwaka sababu sk hizi barabara zimetengenezwa na watu wengi wana magari si kama zamani.
Zile nyumba zinarithishwa kwa hiyo vizazi na vizazi vinaendekea kuishi kwenye makazi bora, sio kunywa supu mjini ukirudi kijijini kwenu unaenda kunya vichakani.
 
Umepanic mkuu take a glass of cold water and relax for a bit,we waenda wizarani kutafuta data za land owners in Tanzania,mie nalog in na kukupa hizo data😂👊🏼🙏
 
moshi ndio mkoa pekeee nyumba za msajili huwezi kukuta wamelundikana wahindi kama mikoa mingine kupata duka la muhindi moshi ni sawa na kukuta mhindi bariadi
Wapo wahindi wenye maduka Moshi mjini nenda double road,kina panjwan and the like unasemaje?sio kila aliye if haifahamu Moshi joh,jipange
 
moshi ndio mkoa pekeee nyumba za msajili huwezi kukuta wamelundikana wahindi kama mikoa mingine kupata duka la muhindi moshi ni sawa na kukuta mhindi bariadi
Kijana labda Kama Kuna Moshi nyingine sio hii.

Wap wahindi kibao hapa double road na maeneo mengine ya mjini kati
 
Kijana labda Kama Kuna Moshi nyingine sio hii.

Wap wahindi kibao hapa double road na maeneo mengine ya mjini kati
sio kama hawapo wapo ila sio wengi kama mikoa mingine broo niko moshi pia
 
Watuache na Moshi yetu. Pumbavu hawa watu, wanasumbulia na chuki
 
Mkuu umeeleza kinaga ubaga na umeeleweka kabisa. Kumbe inaweza kua nisababu pia ya wachaga kutapakaa nchini si ajabu moshi ingekua kama arusha labda wangejikalia zao huko kula mema ya huko kwao.
 
Btw nimezaliwa na kukulia Moshi mjini Soweto pale na tuna bonge la mji plus shamba pale,sitishwina ndezi Kama wewe.Afu ni wakuja tu,sikuzote wanajikomba niwe mchaga Kama wait,nawajibu Noh mie mtu wa mbeya baba🙏
 
Ardhi waipate wapi. Ni maskini wa kutupwa hao
 
Mkuu umeeleza kinaga ubaga na umeeleweka kabisa. Kumbe inaweza kua nisababu pia ya wachaga kutapakaa nchini si ajabu moshi ingekua kama arusha labda wangejikalia zao huko kula mema ya huko kwao.
uhaba wa ardhi ulipelekea wachaga wengi kuhama toka kilimanjaro. wakati wa utawala wa mwalimu nyerere kuna wachaga walihamishiwa maeneo ya morogoro na kutokana na uhaba wa ardhi kilimanjaro.

miaka ya 70 na 80 kulitokea changamoto ktk kilimo cha zao la kahawa na hiyo ikasababisha wachaga wengi kukimbilia mijini. jamii ya kwanza kufanya umachinga dar es salaam, kwa mfano, kushona na kupiga rangi viatu, kukaanga chips, na gereji bubu, ni wachaga na hiyo ilikuwa miaka ya 80. ilipofika miaka ya 90 ndipo wakaja wamachinga toka mikoa ya kusini ambao walijishughulisha zaidi na uuzaji wa nguo.

hivi majuzi mbunge wa vunjo dr.kimei aliiomba serikali ifikirie kuwapatia wapigakura wake maeneo ya kulima sehemu mbalimbali za tanzania. sasa inabidi watu wajiulize ni mbunge gani mwingine amewahi kutoa ombi la namna hiyo kwa serikali? mchango huo wa mbunge ni kielelezo cha tatizo kubwa la ardhi na ukosefu wa fursa unaowakabili wananchi wa kilimanjaro.

moshi ingekuwa na fursa mpya kama arusha tusingewaona wachaga wengi maeneo mengine ya tanzania. pia wasingekuwa na tatizo la ardhi wasingetapakaa tanzania nzima. na wasingebahatika kupata elimu wasingehamia maeneo mengine kikazi na kuweza kuziona fursa zilizoko nje ya uchagani.

mwisho, wachaga wanapaswa kuwekeza ktk mji wao wa moshi ambao kwa sasa hivi umedumaa. wako wengi wenye mitaji mikubwa ambao wangeweza kuichangamsha moshi kwa kuwekeza kwenye viwanda. hii habari ya kujisifia kujenga majumba ya kifahari migombani naamini imepitwa na wakati. wachaga wa karne ya 21 wanatakiwa wajisifu kwa kuwekeza ktk viwanda ktk mkoa wa kilimanjaro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…