Anayofanya Christina Shusho ni matokeo ya Wanaume wengi kuoa Wanawake Watumwa wasio huru. Siku wakipata Uhuru wao hayo ndio hutokeaga

Mbona hilo lipo wazi! Binafsi nafurahi kuona baadhi ya watu wanaona ukweli wa mambo nje ya mihemko. Ukweli ambao hauhitaji democracy kuthibitika kuwa ni ukweli. Hii inaonesha kuwa there's hope in our society.

Badala ya kumlaumu Tina, ingependeza kuchukua key take-aways kwenye hili saga, especially from mzee shusho na wazazi wa Tina.

Mwanamke anapaswa kuolewa akiwa anajitambua na ameridhia. Kinyume na hapo ni biashara ya utumwa.
Ke yupi aliwahi kuridhika tangu kuumbwa kwa ulimwengu? Unadhani una akili sana kuliko aliyeumba Ke na kuagiza Me waishi nao kwa akili?

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Ke yupi aliwahi kuridhika tangu kuumbwa kwa ulimwengu? Unadhani una akili sana kuliko aliyemuumba Ke na kuagiza Me waishi nao kwa akili?

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.

Kwani ni mwanaume gani kwenye hii dunia aliwahi kuridhika?
Nikupe takwimu ya matukio tuliyoyafanya wanaume kwa kutokuridhika?

Elewa Mwanamke na mwanaume wote ni binadamu.
 
Ukweli mtupu japo huu ni mkuki moyoni kwa wanaume, ndoa nyingi ni za mme na mtumwa tu.....
Utumwa unaofichwa kwa mwamvuli wa upendo na utii na bla bla nyingi.

Namna bora ya kuondoa haya ni kuwapa Watu elimu ya kweli. Ili kila mtu awe huru.

Huoni humu wanaume hawataki na wanaogopa wanawake waliosoma na wenye kazi? Sababu kubwa ni kuwa wanataka Wanawake Watumwa na sio Wake.

Mwanaume hataki kubishiwa jambo ilhali ukiangalia kakosea huoni hapo kuna tatizo.
 
Leo unakataa wanaume kuwa na wake wengi wakati huko nyuma umewahi kuandika kuwa wanaume kuwa na wake wengi ni jambo sahihi. Siyo contradiction hiyo?.
Jambo kuwa kiasili haimaanishi ni HAKI.
Niliwahi andika hivyo lakini haimaanishi nililiunga mkono.

Unapozungumza Umri una maana kuwa mabinti wenye miaka 18 wasiolewe au?.

Mwanamke aolewe katika umri ambao kwa hiyari yake anataka kuolewa.
 
Kwani ni mwanaume gani kwenye hii dunia aliwahi kuridhika?
Nikupe takwimu ya matukio tuliyoyafanya wanaume kwa kutokuridhika?

Elewa Mwanamke na mwanaume wote ni binadamu.
Me walioridhika.

1. Yusufu.

2. Enock.

3. Ayubu.

4. Mimi.

Ke wasioridhika.

1. Ever.

2. Delilah.

3. Mary.

4. Yezebeli.

5. Mke wa Mfalme Potifa aliyetaka kumbaka Yusufu.

6........
 
NDOA Si uwanja wa vita.

Ikiwa mume na mke ni mwili mmoja,

Hizo harakati za kudai Uhuru wa mke zinatoka wapi kama Si Kwa shetani?
 
ANAYOFANYA CHRISTINA SHUSHO NI MATOKEO YA WANAUME WENGI KUOA WANAWAKE WATUMWA "WASIOHURU. SIKU WAKIPATA UHURU WAO HAYO NDIO HUTOKEAGA.

Anaandika Robert Heriel
Mtibeli

Huwezi mfanya Mwanamke mtumwa alafu ukamuita Mkeo.
Unajua Watu wengi wamechukua wanawake na kuwageuza watumwa wa kingono na vijakazi wao alafu hujinasibu kuwa Wameoa. Hakuna ndoa ya hivyo. Sema umemnunua Mwanamke na kumgeuza mtumwa wa ngôno na kijakazi wako hapo sisi Watibeli tutakuelewa.

Mfano, kwenye ndoa hakunaga ndoa ya Wake wengi. Ila kwenye utumwa wanaume huruhusiwa kuchukua wanawake watumwa wengi na kuwaita Wake zao ilhali sio kweli na sio Haki.

Kama ilivyo kwa sisi wanaume tusivyoweza kukubali kuwa na Mwanamke mwenye mahusiano na wanaume wawili. Ndivyo hivyohivyo kwa wanawake.

Wanaume wengi hupenda kuishi na Wanawake watumwa kuliko kuoa Mke. Sio ajabu wanaume wengi hujiamini na kutaka Mwanamke mwenye kipato duni au asiyefanya kazi, na wengi huenda mbali kwa kuchukua vibinti vidogo ili wavitumikishe kitumwa.

Kimantiki huwezi pata kitu kinachoitwa heshima kwa mtumwa. Mtumwa hawezi kukupa heshima. Heshima hutolewa na Watu Huru.
Kupewa heshima na mtu asiyehuru au mtumwa huitwa nidhamu ya woga, unafiki na ulaghai.

Kuoa Mwanamke mdogo kiumri ambaye hana maamuzi sio tuu ukatili bali pia ni dhulma ambayo baadaye lazima iligharimu.

Mimi kama Mtibeli halisi nasema, hasa kwa vijana. Ikiwa unahitaji kuishi na mwanaume ambaye utamuita mke basi yakupasa ûtafute mwanamke aliyehuru.
Namaanisha huru kiakili, kihisia, kimwili na kiroho.

Christina Shusho NI kielelezo cha wanawake wengi walioolewa pasipo uhuru wao kuheshimiwa na kuthaminiwa.

Nilieleza pia, Mke hatolewi Mahari. Ila watumwa hutolewa mahari.
Mwanamke aliyehuru hawezi kukubali kutolewa mahari kwa sababu mahari msingi wake mkuu ni kumdunisha Mwanamke na kumdhalilisha ingawaje kwa umbo la nje waliolianzisha walilifanya kama kumheshimisha.

Mwanaume ni bora ikiwa atajua kusimamia Haki. Na Mwanamke atakuwa bora kama mwanaume ikiwa atajua haki zake na nani wa kuzisimamia.

Usioe Mwanamke asiyehuru(tegemezi) na kama utamuoa basi hakikisha unampatia uhuru wake. Ajitegemee.

Usimuozeshe binti yako kama bado hayupo huru. Huko ni kumkosea binti yako.

Usioe Mwanamke asiyefanyakazi, na kama umemuoa akiwa hana kazi basi hakikisha unampa kazi au anasimamia kazi na miradi ya familia. Nazungumzia kazi za kuzalisha kipato sio kazi za nyumbani. Kazi za nyumbani zitafanywa na mtu yeyote au machine. Baba au mume uwe kiongozi alafu mke au mama awe msaidizi. Hiyo ndio tafsiri ya ndoa kama hamtaki iwe ndoani.

Usioe Mwanamke ambaye hakupendi(moyo wake haupo huru na wewe). Atakusumbua na wewe utamsumbua.

Usimlazimishe Mwanamke kuwa na wewe hata kama mmeishi miaka mingi.
Usiingilie uhuru wa mtu mwingine wa kuchagua na kuutendea mwili wake. Kama ameku-cheat na anataka mwanaume mwingine muache aende.

Elewa, Mwanamke aliyehuru hadanganywi ila anafanya kwa Makusudi.
Ila watumwa hudanganywa kwa sababu wapo kwenye harakati za kutafuta uhuru wao.

Usioe mwanamke asiyeweza kujitunza mwenyewe, wala kujitafutia kipato. Huyo sio mke, huyo ni mtumwa.

Mke mchapakazi haimaanishi kazi za nyumbani pekee bali kazi za uzalishaji mali. Hata siku usipokuwepo unajua kabisa ile ndoto ya familia uitakayo itatimizwa na mkeo. Na sio ukifa basi watoto wako ndio habari imeisha.

Oa Mwanamke anayejua Haki zake kwani mtu kujua haki zake ni tafsiri ya kujua haki zako pia.
Mtu asiyejua haki zake hawezi kujua haki zako.

Elewa, mwanamke anayekubali kuonewa jua naye kuna sehemu ànakuonea au upo wakati unaokuja atakuonea tuu. Kwa sababu hiyo ni HAKI.

Ukijiona wewe ni mwanaume na unathamani kwenye ndoa kuliko Mwanamke elewa hata mwanamke atajiona anathamani kuliko wewe. Haitakuwa ndoa bali ndoano full kuumizana.
Lakini ukijitoa kwa mwenzako naye atajitoa. Ukimtañguliza mwenzako naye atakutanguliza.

Heshima yako kama mwanaume haipo kwa kumfanya Mwanamke mtumwa wako. Ila ipo kwa kumfanya Mwanamke kuwa Mtu na kulinda utu wake.
Yale yote unayotaka kufanyiwa basi mfanyie mwenzako. Na yale yote isiyotaka kufanyiwa basi usimfanyie mwenzako.

Kuwa mwanaume sio tafsiri ya tiketi ya kufanya dhulma na uhalifu wa kijinsia kwa Mwanamke.
Kama nilivyoandikaga, kuwa mzazi sio kigezo cha kufanya dhulma kwa watoto wako kisa uliwazaa.

Ni ruhusa na Haki yako kumuacha(kutoa talaka) Mwanamke ambaye ulimpenda, na ukafanya kila jitihada na kuheshimu na kulinda ûtu na hadhi yake na yako lakini ikashindikana. Vivyohivyo kwa Mwanamke.

Ni yule Mtibeli kutoka nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama, Shinyanga.
Umepotoka
 
Nakushauri jaribu kaandika mada unazozielewa vizuri Kama zamani
Zina ambazo huna uelewa nazo achana
Leo umepuyanga
INGAwa ni mawazo yako

Umejaribu kumtetea huyo mwimbaji Kana kwamba ilikuwa ni ndoa za utotoni
Kisheria na kimaumbile mtoto wa kike akishafikiasha miaka 18 ni MTU mzima anayejielewa kufanya maamuzi
Ya kuolewa au kutokuolewq Tena aolewe na nani
Pili huyo ni mkristo Tena mlokole ambaye mara nyingi lazima sala na ibada zihusike Sana kabla ya ndoa

Kwa hiyo Kama aliamua kuishi na mume wake kinafiki alifanya akiwa na akili timamu
Kwa historia Ibahimu alimpita mke wake miaka 10
Na biblia inasema alimwita bwana maana yake alitambua nafasi yake na majukumu yake
Siku zote mwanaume ni kichwa Cha familia haijalishi mwanmke ana cheo au HUDUMA kubwa kiasi gani
Lazima awe mtii na mnyekevu kwa bwana wake

Kwa Sasa umeacha fact naona unatafuta ushabiki wa Mfumo mpya wa kutaka kumuondoa mwanaume nafasi yake
 
Me walioridhika.

1. Yusufu.

2. Enock.

3. Ayubu.

4. Mimi.

Ke wasioridhika.

1. Ever.

2. Delilah.

3. Mary.

4. Yezebeli.

5..................

Ke zilizoridhika

1. Mariam Mama wa Yesu
2. Sara MKE wa Ibrahim
3. Rebeka Mke wa Yakobo
4. malkia Esther mke wa Ahusuero
5. Abigail MKE wa Daudi

Me ambazo hazikuridhika
1. Amnoni Mtoto wa Daudi
2. Yuda Msaliti
3. Samson mwenye miguvu
4. Nduguze Yusufu
5. Yakobo Kumtapeli Esau
6. Kaini nduguye Haviko(Abel)

Au unataka tuwataje ambao tunawajua kwa nyakati hizi?
 
Mbona kuna wanawake wengi tu wananiomba niwaoe ina maana wanakubali kuwa watumwa wangu ni kweli kwamba wanawake walioolewa ni watumwa
 
Namna bora ya kuondoa haya ni kuwapa Watu elimu ya kweli. Ili kila mtu awe huru.

Huoni humu wanaume hawataki na wanaogopa wanawake waliosoma na wenye kazi? Sababu kubwa ni kuwa wanataka Wanawake Watumwa na sio Wake.

Mwanaume hataki kubishiwa jambo ilhali ukiangalia kakosea huoni hapo kuna tatizo.
Hili unalionaje Mtibeli? Hata wanawake wanaojitambua, wasomi na wako financially stable bado wanataka walipiwe mahari tena kubwa kwa sababu, kwa namna moja au nyingine, mahari kubwa eti inaakisi thamani yao kwenye familia na jamii inayowazunguka. Kwamba ukimuoa bila kumtolea mahari au kwa kutoa mahari kiduchu basi ndoa yenu itaonekana haina thamani kwa wanajamii na ni kama utani tu kwa wazazi. Jambo hili kidogo huwa linanishangaza!

Wanawake pia njooni hapa mtoe maoni yenu. Kwa nini bado mnapigania mahari tena ya mamilioni wakati huo huo mnapigania usawa dhidi ya mikatale ya mfumo dume? 😳 😳 😳 😳
 
Back
Top Bottom