Anayofanya Christina Shusho ni matokeo ya Wanaume wengi kuoa Wanawake Watumwa wasio huru. Siku wakipata Uhuru wao hayo ndio hutokeaga

Upo sahihi kwa misingi ya kisiasa na dunia ya sasa inavyotaka binadamu tuishi.
Women deserve freedom.

Maswali yangu kwako mkuu?

1.Do women really need freedom?
Is freedom what women really want?
Uhuru ni haki ya mtu bila kujali anataka au hatakî. Haki ni lazima sio hiyari.

2.freedom is earned not given, can you talk about it.

Jaribu kupambana na Nature

Hata hivyo wanawake sio kama wanapewa Uhuru ila uhuru wao wanaupigania wenyewe kwa namna mbalimbali.
According to nature Freedom is one of the important Masculine core values.

I dont find freedom in any of the feminine core values.

Tukijikita kwenye fraudulent politics that spread nothing but chaos ni jambo la busara kuwapa women freedom kama hutaki matatizo .

Binafsi sina shida na wakina miss independent i do respect em like other brothers.

Mkuu mimi sio mfuasi wa Watu wanaopenda kupendelewa. Nataka Watu wapewe haki zao. Hilo tuu.

Hicho mnachokipinga ndio hichohicho CCM na vyama vya upinzani vinavyofanya
 
Samahani Mtoa Mada , Naomba uniambie Mfumo Dume wa KiMungu upoje ?
 
Mkuu wazungu ni Watu kama sisi tuu.
Elewa kuwa kuja wazungu wengi tuu wanapenda mfumo dume kama ilivyo waafrika au jamii zote.

Pia Wazungu wana movements nyingi mno kuachana na hiyo moja ya Gender.
Mfano ishu ya Kupingana na ubaguzi wa rangi. Hivi unajua bila ya wazungu mpaka hivi leo bado tungekuwa Makoloni?
Neno ukoloni mambo leo halijapatikana kibahati mbaya mkuu.

Sisi bado tunatawaliwa.
Kama unataka ukweli fuatilia hotuba zote za juliasi utagundua hilo.

Tujikite kwenye mada naona leo umeamua kuplay as a Devil's advocate kwenye hii thread yako.

The fact sijamzungumzia c shusho na situation yake nimeamua kutonasa kweny huu mtego.
 
Mtoa Mada , Naomba uniambie Mwanamke ameelezewaje ( awe vipi ) kwenye Familia ? Tumia Biblia

Na Mwanaume Ameelezewaje ( Awe Vipi ) kwenye Familia ? Tumia Biblia

Kwanini nimekuambia Biblia , Ndio Neno la Mungu Muumbaji ....
 
Kwani kipi kwenye mada ambacho hakipo sàhihi ili nione msingi wa hoja yako?
 
ANAYOFANYA CHRISTINA SHUSHO NI MATOKEO YA WANAUME WENGI KUOA WANAWAKE WATUMWA "WASIOHURU. SIKU WAKIPATA UHURU WAO HAYO NDIO HUTOKEAGA.

Anaandika Robert Heriel
Mtibeli

Huwezi mfanya Mwanamke mtumwa alafu ukamuita Mkeo.
Unajua Watu wengi wamechukua wanawake na kuwageuza watumwa wa kingono na vijakazi wao alafu hujinasibu kuwa Wameoa. Hakuna ndoa ya hivyo. Sema umemnunua Mwanamke na kumgeuza mtumwa wa ngôno na kijakazi wako hapo sisi Watibeli tutakuelewa.

Mfano, kwenye ndoa hakunaga ndoa ya Wake wengi. Ila kwenye utumwa wanaume huruhusiwa kuchukua wanawake watumwa wengi na kuwaita Wake zao ilhali sio kweli na sio Haki.

Kama ilivyo kwa sisi wanaume tusivyoweza kukubali kuwa na Mwanamke mwenye mahusiano na wanaume wawili. Ndivyo hivyohivyo kwa wanawake.

Wanaume wengi hupenda kuishi na Wanawake watumwa kuliko kuoa Mke. Sio ajabu wanaume wengi hujiamini na kutaka Mwanamke mwenye kipato duni au asiyefanya kazi, na wengi huenda mbali kwa kuchukua vibinti vidogo ili wavitumikishe kitumwa.

Kimantiki huwezi pata kitu kinachoitwa heshima kwa mtumwa. Mtumwa hawezi kukupa heshima. Heshima hutolewa na Watu Huru.
Kupewa heshima na mtu asiyehuru au mtumwa huitwa nidhamu ya woga, unafiki na ulaghai.

Kuoa Mwanamke mdogo kiumri ambaye hana maamuzi sio tuu ukatili bali pia ni dhulma ambayo baadaye lazima iligharimu.

Mimi kama Mtibeli halisi nasema, hasa kwa vijana. Ikiwa unahitaji kuishi na mwanaume ambaye utamuita mke basi yakupasa ûtafute mwanamke aliyehuru.
Namaanisha huru kiakili, kihisia, kimwili na kiroho.

Christina Shusho NI kielelezo cha wanawake wengi walioolewa pasipo uhuru wao kuheshimiwa na kuthaminiwa.

Nilieleza pia, Mke hatolewi Mahari. Ila watumwa hutolewa mahari.
Mwanamke aliyehuru hawezi kukubali kutolewa mahari kwa sababu mahari msingi wake mkuu ni kumdunisha Mwanamke na kumdhalilisha ingawaje kwa umbo la nje waliolianzisha walilifanya kama kumheshimisha.

Mwanaume ni bora ikiwa atajua kusimamia Haki. Na Mwanamke atakuwa bora kama mwanaume ikiwa atajua haki zake na nani wa kuzisimamia.

Usioe Mwanamke asiyehuru(tegemezi) na kama utamuoa basi hakikisha unampatia uhuru wake. Ajitegemee.

Usimuozeshe binti yako kama bado hayupo huru. Huko ni kumkosea binti yako.

Usioe Mwanamke asiyefanyakazi, na kama umemuoa akiwa hana kazi basi hakikisha unampa kazi au anasimamia kazi na miradi ya familia. Nazungumzia kazi za kuzalisha kipato sio kazi za nyumbani. Kazi za nyumbani zitafanywa na mtu yeyote au machine. Baba au mume uwe kiongozi alafu mke au mama awe msaidizi. Hiyo ndio tafsiri ya ndoa kama hamtaki iwe ndoani.

Usioe Mwanamke ambaye hakupendi(moyo wake haupo huru na wewe). Atakusumbua na wewe utamsumbua.

Usimlazimishe Mwanamke kuwa na wewe hata kama mmeishi miaka mingi.
Usiingilie uhuru wa mtu mwingine wa kuchagua na kuutendea mwili wake. Kama ameku-cheat na anataka mwanaume mwingine muache aende.

Elewa, Mwanamke aliyehuru hadanganywi ila anafanya kwa Makusudi.
Ila watumwa hudanganywa kwa sababu wapo kwenye harakati za kutafuta uhuru wao.

Usioe mwanamke asiyeweza kujitunza mwenyewe, wala kujitafutia kipato. Huyo sio mke, huyo ni mtumwa.

Mke mchapakazi haimaanishi kazi za nyumbani pekee bali kazi za uzalishaji mali. Hata siku usipokuwepo unajua kabisa ile ndoto ya familia uitakayo itatimizwa na mkeo. Na sio ukifa basi watoto wako ndio habari imeisha.

Oa Mwanamke anayejua Haki zake kwani mtu kujua haki zake ni tafsiri ya kujua haki zako pia.
Mtu asiyejua haki zake hawezi kujua haki zako.

Elewa, mwanamke anayekubali kuonewa jua naye kuna sehemu ànakuonea au upo wakati unaokuja atakuonea tuu. Kwa sababu hiyo ni HAKI.

Ukijiona wewe ni mwanaume na unathamani kwenye ndoa kuliko Mwanamke elewa hata mwanamke atajiona anathamani kuliko wewe. Haitakuwa ndoa bali ndoano full kuumizana.
Lakini ukijitoa kwa mwenzako naye atajitoa. Ukimtañguliza mwenzako naye atakutanguliza.

Heshima yako kama mwanaume haipo kwa kumfanya Mwanamke mtumwa wako. Ila ipo kwa kumfanya Mwanamke kuwa Mtu na kulinda utu wake.
Yale yote unayotaka kufanyiwa basi mfanyie mwenzako. Na yale yote isiyotaka kufanyiwa basi usimfanyie mwenzako.

Kuwa mwanaume sio tafsiri ya tiketi ya kufanya dhulma na uhalifu wa kijinsia kwa Mwanamke.
Kama nilivyoandikaga, kuwa mzazi sio kigezo cha kufanya dhulma kwa watoto wako kisa uliwazaa.

Ni ruhusa na Haki yako kumuacha(kutoa talaka) Mwanamke ambaye ulimpenda, na ukafanya kila jitihada na kuheshimu na kulinda ûtu na hadhi yake na yako lakini ikashindikana. Vivyohivyo kwa Mwanamke.

Ni yule Mtibeli kutoka nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama, Shinyanga.
Hoja Ulizoandika kwa sehemu kubwa ni sahihi lakini sidhani kama unauthibitisho wa kutosha kuhusisha ndoa ya Christina Shusho katika mazingira uliyoandika.
 
Uhuru ni haki ya mtu bila kujali anataka au hatakî. Haki ni lazima sio hiyari.

Hata hivyo wanawake sio kama wanapewa Uhuru ila uhuru wao wanaupigania wenyewe kwa namna mbalimbali.

Mkuu mimi sio mfuasi wa Watu wanaopenda kupendelewa. Nataka Watu wapewe haki zao. Hilo tuu.

Hicho mnachokipinga ndio hichohicho CCM na vyama vya upinzani vinavyofanya
Kama ni mahakamani hii kesi utashinda 100%

Nilitegemea utatumia falsafa za kitibeli katika hili.
 
Mtoa Mada , Naomba uniambie Mwanamke ameelezewaje ( awe vipi ) kwenye Familia ? Tumia Biblia

Na Mwanaume Ameelezewaje ( Awe Vipi ) kwenye Familia ? Tumia Biblia

Kwanini nimekuambia Biblia , Ndio Neno la Mungu Muumbaji ....

Mithali 31 inamuelezea Mwanamke anatakiwa kuwaje. Kisha amtii mumewe.

Mume anatakiwa ampende Mkewe.

Neno mke na mume linakuja baada ya wawili hao kupendana(kukubaliana).
Lakini kama kuna mmoja Kalazimishwa automatically protokali haiwezi kufuatwa kwa sababu msingi mkuu umevunjwa
 
Hoja Ulizoandika kwa sehemu kubwa ni sahihi lakini sidhani kama unauthibitisho wa kutosha kuhusisha ndoa ya Christina Shusho katika mazingira uliyoandika.

Nimeandika kutokana na kile alichoeleza Christina Shusho mwenyewe.
Alafu Christina Shusho hapa ni Case study tuu ila mada inahusu Watu wote
 
Kama ni mahakamani hii kesi utashinda 100%

Nilitegemea utatumia falsafa za kitibeli katika hili.

Hata kitibeli nitashinda Mkuu.
Kwa sababu Utibeli ni Haki, upendo, maarifa na ukweli. Ambapo kwa mahakama kinachohitajika ni kimoja tuu ukweli(ushahidi)
 
Mbona hilo lipo wazi! Binafsi nafurahi kuona baadhi ya watu wanaona ukweli wa mambo nje ya mihemko. Ukweli ambao hauhitaji democracy kuthibitika kuwa ni ukweli. Hii inaonesha kuwa there's hope in our society.

Badala ya kumlaumu Tina, ingependeza kuchukua key take-aways kwenye hili saga, especially from mzee shusho na wazazi wa Tina.

Mwanamke anapaswa kuolewa akiwa anajitambua na ameridhia. Kinyume na hapo ni biashara ya utumwa.
Kuna nini kwani
 
Uhuru
Uhuru ni zaidi ya vile ambavyo umajaribu kusema kuwa wanawake wanatakiwa kupewa uhuru.

Kumtetea mwanamke asifanye majukumu yake muhimu kwenye familia hiyo siyo kumpa uhuru .

Hakuna sehemu nimesema Mwanamke asifanye majukumu yake katika familia. Ila ñilichoandika ni kuwa majukumu ya Mwanamke ndani ya familia ni makubwa na yanakaribiana na ya mwanaume ndio maàna ya mke ni msaidizi wa mume hata siku mume asipokuwepo mke ndio anabeba familia na anakuwa kichwa cha nyumba
 
ANAYOFANYA CHRISTINA SHUSHO NI MATOKEO YA WANAUME WENGI KUOA WANAWAKE WATUMWA "WASIOHURU. SIKU WAKIPATA UHURU WAO HAYO NDIO HUTOKEAGA.

Anaandika Robert Heriel
Mtibeli

Huwezi mfanya Mwanamke mtumwa alafu ukamuita Mkeo.
Unajua Watu wengi wamechukua wanawake na kuwageuza watumwa wa kingono na vijakazi wao alafu hujinasibu kuwa Wameoa. Hakuna ndoa ya hivyo. Sema umemnunua Mwanamke na kumgeuza mtumwa wa ngôno na kijakazi wako hapo sisi Watibeli tutakuelewa.

Mfano, kwenye ndoa hakunaga ndoa ya Wake wengi. Ila kwenye utumwa wanaume huruhusiwa kuchukua wanawake watumwa wengi na kuwaita Wake zao ilhali sio kweli na sio Haki.

Kama ilivyo kwa sisi wanaume tusivyoweza kukubali kuwa na Mwanamke mwenye mahusiano na wanaume wawili. Ndivyo hivyohivyo kwa wanawake.

Wanaume wengi hupenda kuishi na Wanawake watumwa kuliko kuoa Mke. Sio ajabu wanaume wengi hujiamini na kutaka Mwanamke mwenye kipato duni au asiyefanya kazi, na wengi huenda mbali kwa kuchukua vibinti vidogo ili wavitumikishe kitumwa.

Kimantiki huwezi pata kitu kinachoitwa heshima kwa mtumwa. Mtumwa hawezi kukupa heshima. Heshima hutolewa na Watu Huru.
Kupewa heshima na mtu asiyehuru au mtumwa huitwa nidhamu ya woga, unafiki na ulaghai.

Kuoa Mwanamke mdogo kiumri ambaye hana maamuzi sio tuu ukatili bali pia ni dhulma ambayo baadaye lazima iligharimu.

Mimi kama Mtibeli halisi nasema, hasa kwa vijana. Ikiwa unahitaji kuishi na mwanaume ambaye utamuita mke basi yakupasa ûtafute mwanamke aliyehuru.
Namaanisha huru kiakili, kihisia, kimwili na kiroho.

Christina Shusho NI kielelezo cha wanawake wengi walioolewa pasipo uhuru wao kuheshimiwa na kuthaminiwa.

Nilieleza pia, Mke hatolewi Mahari. Ila watumwa hutolewa mahari.
Mwanamke aliyehuru hawezi kukubali kutolewa mahari kwa sababu mahari msingi wake mkuu ni kumdunisha Mwanamke na kumdhalilisha ingawaje kwa umbo la nje waliolianzisha walilifanya kama kumheshimisha.

Mwanaume ni bora ikiwa atajua kusimamia Haki. Na Mwanamke atakuwa bora kama mwanaume ikiwa atajua haki zake na nani wa kuzisimamia.

Usioe Mwanamke asiyehuru(tegemezi) na kama utamuoa basi hakikisha unampatia uhuru wake. Ajitegemee.

Usimuozeshe binti yako kama bado hayupo huru. Huko ni kumkosea binti yako.

Usioe Mwanamke asiyefanyakazi, na kama umemuoa akiwa hana kazi basi hakikisha unampa kazi au anasimamia kazi na miradi ya familia. Nazungumzia kazi za kuzalisha kipato sio kazi za nyumbani. Kazi za nyumbani zitafanywa na mtu yeyote au machine. Baba au mume uwe kiongozi alafu mke au mama awe msaidizi. Hiyo ndio tafsiri ya ndoa kama hamtaki iwe ndoani.

Usioe Mwanamke ambaye hakupendi(moyo wake haupo huru na wewe). Atakusumbua na wewe utamsumbua.

Usimlazimishe Mwanamke kuwa na wewe hata kama mmeishi miaka mingi.
Usiingilie uhuru wa mtu mwingine wa kuchagua na kuutendea mwili wake. Kama ameku-cheat na anataka mwanaume mwingine muache aende.

Elewa, Mwanamke aliyehuru hadanganywi ila anafanya kwa Makusudi.
Ila watumwa hudanganywa kwa sababu wapo kwenye harakati za kutafuta uhuru wao.

Usioe mwanamke asiyeweza kujitunza mwenyewe, wala kujitafutia kipato. Huyo sio mke, huyo ni mtumwa.

Mke mchapakazi haimaanishi kazi za nyumbani pekee bali kazi za uzalishaji mali. Hata siku usipokuwepo unajua kabisa ile ndoto ya familia uitakayo itatimizwa na mkeo. Na sio ukifa basi watoto wako ndio habari imeisha.

Oa Mwanamke anayejua Haki zake kwani mtu kujua haki zake ni tafsiri ya kujua haki zako pia.
Mtu asiyejua haki zake hawezi kujua haki zako.

Elewa, mwanamke anayekubali kuonewa jua naye kuna sehemu ànakuonea au upo wakati unaokuja atakuonea tuu. Kwa sababu hiyo ni HAKI.

Ukijiona wewe ni mwanaume na unathamani kwenye ndoa kuliko Mwanamke elewa hata mwanamke atajiona anathamani kuliko wewe. Haitakuwa ndoa bali ndoano full kuumizana.
Lakini ukijitoa kwa mwenzako naye atajitoa. Ukimtañguliza mwenzako naye atakutanguliza.

Heshima yako kama mwanaume haipo kwa kumfanya Mwanamke mtumwa wako. Ila ipo kwa kumfanya Mwanamke kuwa Mtu na kulinda utu wake.
Yale yote unayotaka kufanyiwa basi mfanyie mwenzako. Na yale yote isiyotaka kufanyiwa basi usimfanyie mwenzako.

Kuwa mwanaume sio tafsiri ya tiketi ya kufanya dhulma na uhalifu wa kijinsia kwa Mwanamke.
Kama nilivyoandikaga, kuwa mzazi sio kigezo cha kufanya dhulma kwa watoto wako kisa uliwazaa.

Ni ruhusa na Haki yako kumuacha(kutoa talaka) Mwanamke ambaye ulimpenda, na ukafanya kila jitihada na kuheshimu na kulinda ûtu na hadhi yake na yako lakini ikashindikana. Vivyohivyo kwa Mwanamke.

Ni yule Mtibeli kutoka nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama, Shinyanga.
Hii 50/50 ndio imeiangamiza dunia
 
Mtu akitaka kutenda dhambi huja na sababu lukuki kuhalalisha dhambi zake.Hata Adamu alipomkosea Mungu alikuja na sababu kibao. Pia mtoto wake, Kaini wakati ana muua nduguye Abeli pia alikuwa ana sababu zake alipoulizwa na Mungu. Kiufupi, Hakuna kinachoJustify yeye kuvunja ndoa. Anakwenda kinyume na Biblia anayoiimba 🤔
 
Kavunja sheria ipi Mkuu ya biblia?
Na wazazi walitumia kifungu gani cha sheria kumlazimisha ndoa?
Maana yeye Utetezi wake ni kuwa aliolewa kwa amri ya wazazi na sio hiyari yake.
 
Hakuna sehemu nimesema Mwanamke asifanye majukumu yake katika familia. Ila ñilichoandika ni kuwa majukumu ya Mwanamke ndani ya familia ni makubwa na yanakaribiana na ya mwanaume ndio maàna ya mke ni msaidizi wa mume hata siku mume asipokuwepo mke ndio anabeba familia na anakuwa kichwa cha nyumba

Mkuu hii ngoma ni nzito
Mwisho wa siku hatuwezi kushindana na mfumo .
 
Kavunja sheria ipi Mkuu ya biblia?
Na wazazi walitumia kifungu gani cha sheria kumlazimisha ndoa?
Maana yeye Utetezi wake ni kuwa aliolewa kwa amri ya wazazi na sio hiyari yake.
Miaka 19 ni mtu mzima. Kabla ya kufunga ndoa huwa unaulizwa pale mbele ya watu wote kama amekubali. Kwanini asikatae? Narudia tena mtu akiamua kutenda dhambi, visingizio havikosekani. Ndoa za kikristo huwa hazivunjiki, labda mmoja wapo, Kati ya wana ndoa, azini🤔
 
Back
Top Bottom