Anayofanya Christina Shusho ni matokeo ya Wanaume wengi kuoa Wanawake Watumwa wasio huru. Siku wakipata Uhuru wao hayo ndio hutokeaga

Ke yupi aliwahi kuridhika tangu kuumbwa kwa ulimwengu? Unadhani una akili sana kuliko aliyeumba Ke na kuagiza Me waishi nao kwa akili?

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Ke yupi aliwahi kuridhika tangu kuumbwa kwa ulimwengu? Unadhani una akili sana kuliko aliyemuumba Ke na kuagiza Me waishi nao kwa akili?

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.

Kwani ni mwanaume gani kwenye hii dunia aliwahi kuridhika?
Nikupe takwimu ya matukio tuliyoyafanya wanaume kwa kutokuridhika?

Elewa Mwanamke na mwanaume wote ni binadamu.
 
Ukweli mtupu japo huu ni mkuki moyoni kwa wanaume, ndoa nyingi ni za mme na mtumwa tu.....
Utumwa unaofichwa kwa mwamvuli wa upendo na utii na bla bla nyingi.

Namna bora ya kuondoa haya ni kuwapa Watu elimu ya kweli. Ili kila mtu awe huru.

Huoni humu wanaume hawataki na wanaogopa wanawake waliosoma na wenye kazi? Sababu kubwa ni kuwa wanataka Wanawake Watumwa na sio Wake.

Mwanaume hataki kubishiwa jambo ilhali ukiangalia kakosea huoni hapo kuna tatizo.
 
Leo unakataa wanaume kuwa na wake wengi wakati huko nyuma umewahi kuandika kuwa wanaume kuwa na wake wengi ni jambo sahihi. Siyo contradiction hiyo?.
Jambo kuwa kiasili haimaanishi ni HAKI.
Niliwahi andika hivyo lakini haimaanishi nililiunga mkono.

Unapozungumza Umri una maana kuwa mabinti wenye miaka 18 wasiolewe au?.

Mwanamke aolewe katika umri ambao kwa hiyari yake anataka kuolewa.
 
Kwani ni mwanaume gani kwenye hii dunia aliwahi kuridhika?
Nikupe takwimu ya matukio tuliyoyafanya wanaume kwa kutokuridhika?

Elewa Mwanamke na mwanaume wote ni binadamu.
Me walioridhika.

1. Yusufu.

2. Enock.

3. Ayubu.

4. Mimi.

Ke wasioridhika.

1. Ever.

2. Delilah.

3. Mary.

4. Yezebeli.

5. Mke wa Mfalme Potifa aliyetaka kumbaka Yusufu.

6........
 
NDOA Si uwanja wa vita.

Ikiwa mume na mke ni mwili mmoja,

Hizo harakati za kudai Uhuru wa mke zinatoka wapi kama Si Kwa shetani?
 
Umepotoka
 
Nakushauri jaribu kaandika mada unazozielewa vizuri Kama zamani
Zina ambazo huna uelewa nazo achana
Leo umepuyanga
INGAwa ni mawazo yako

Umejaribu kumtetea huyo mwimbaji Kana kwamba ilikuwa ni ndoa za utotoni
Kisheria na kimaumbile mtoto wa kike akishafikiasha miaka 18 ni MTU mzima anayejielewa kufanya maamuzi
Ya kuolewa au kutokuolewq Tena aolewe na nani
Pili huyo ni mkristo Tena mlokole ambaye mara nyingi lazima sala na ibada zihusike Sana kabla ya ndoa

Kwa hiyo Kama aliamua kuishi na mume wake kinafiki alifanya akiwa na akili timamu
Kwa historia Ibahimu alimpita mke wake miaka 10
Na biblia inasema alimwita bwana maana yake alitambua nafasi yake na majukumu yake
Siku zote mwanaume ni kichwa Cha familia haijalishi mwanmke ana cheo au HUDUMA kubwa kiasi gani
Lazima awe mtii na mnyekevu kwa bwana wake

Kwa Sasa umeacha fact naona unatafuta ushabiki wa Mfumo mpya wa kutaka kumuondoa mwanaume nafasi yake
 
Me walioridhika.

1. Yusufu.

2. Enock.

3. Ayubu.

4. Mimi.

Ke wasioridhika.

1. Ever.

2. Delilah.

3. Mary.

4. Yezebeli.

5..................

Ke zilizoridhika

1. Mariam Mama wa Yesu
2. Sara MKE wa Ibrahim
3. Rebeka Mke wa Yakobo
4. malkia Esther mke wa Ahusuero
5. Abigail MKE wa Daudi

Me ambazo hazikuridhika
1. Amnoni Mtoto wa Daudi
2. Yuda Msaliti
3. Samson mwenye miguvu
4. Nduguze Yusufu
5. Yakobo Kumtapeli Esau
6. Kaini nduguye Haviko(Abel)

Au unataka tuwataje ambao tunawajua kwa nyakati hizi?
 
Mbona kuna wanawake wengi tu wananiomba niwaoe ina maana wanakubali kuwa watumwa wangu ni kweli kwamba wanawake walioolewa ni watumwa
 
Hili unalionaje Mtibeli? Hata wanawake wanaojitambua, wasomi na wako financially stable bado wanataka walipiwe mahari tena kubwa kwa sababu, kwa namna moja au nyingine, mahari kubwa eti inaakisi thamani yao kwenye familia na jamii inayowazunguka. Kwamba ukimuoa bila kumtolea mahari au kwa kutoa mahari kiduchu basi ndoa yenu itaonekana haina thamani kwa wanajamii na ni kama utani tu kwa wazazi. Jambo hili kidogo huwa linanishangaza!

Wanawake pia njooni hapa mtoe maoni yenu. Kwa nini bado mnapigania mahari tena ya mamilioni wakati huo huo mnapigania usawa dhidi ya mikatale ya mfumo dume? 😳 😳 😳 😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…