Anayofanya Christina Shusho ni matokeo ya Wanaume wengi kuoa Wanawake Watumwa wasio huru. Siku wakipata Uhuru wao hayo ndio hutokeaga

Mkuu?
Concept ya uhuru nadhan kuna mengi nahitaji kujifunza.

Ngoja niweke kambi hapa nione wengine wanasemaje?

Uhuru bila kufanya uhalifu wala dhambi ndio huitwa Uhuru.

Sasa mwanamke kuwa huru kwa nini baadhi ya Watu huona shida? Nîni wanafaidika wanawake wanapoteseka kihisia, kiakili, kiroho na kimwili?

Najua wapo wanaume pia wanateseka kwa kasumba na dhana potofu kwa kisingizio cha uanaume.

Mfano, umenyeke na kuteseka kutafuta pesa ili umhudumie Mwanamke ambaye sio mkeo na huishi naye. Huo ni unyanyasaji
 
Kwa nyuzi zake na reply inaonyesha bado ni mtoto anayeongozwa na fantasy
 
Jalali akuongoze.
Watu tuwaze tunavyowaza, tuhubiri tunayoyaamini ila kwenye hii dunia UHALISIA NDIO CHUJIO na muda unatosha kabisa kuthibitisha hilo.
Ni wachache sana wameweza kutenganisha hisia zao kwenye kufanya maamuzi,na hao ndio wanaofuzu.
Maadamu andiko lako linaishi,na Christina tunamtumia kama sampuli....tuache uhalisia uamue.
ULIMWENGU NDIO MAMA
 
Inaonyesha alikuwa na tamaa zake binafsi kwa huyo mume wake akamua kuishi naye kinafiki kwa miaka yote ambao baada ya kuzipata anaona Hana maana Tena kwake
Neno “inaonyesha” ni tafsiri yako wewe binafsi ili ku-justify point yako.

Yeye amesema alilazimishwa Halafu wewe umetafuta neno la kusadikika kwa upeo wa akili yako ili upate hoja

Kama alilazimishwa na wazazi sisi hatujui, mapito aliyokuwa akipitia ndani ya ndoa yake vilevile hatuyajui.
 
Mpinga kristo ni wale wasiotaka ukweli na wanaopinga Haki.
Huyo Christina keshakuambia Ndoa alilazimishwa sasa wewe unataka kusemaje?

(Mimi nachoelewa ni Shusho amepata shambulio la kiroho akashindwa kujinasua)

Hapa naunga mkono kiuhalisi wakristo ambao wako karibu sana na MUNGU ndio wanapigwa vita kubwa sana coz wengi huwa wanajikuta wamedondoka kwa kusema wamesikia sauti ya roho ya mtakatifu ikiwaambia this and this kumbe ni Bwana DEVIL huwa wanashindwa kutofautisha Is this the Voice of GOD/SATAN? na kama hulijui neno vizuri UNAENDA NA MAJI.
 
NAkubaliana na ww kwa asilimia 100% juu uhuru huo uloeleza kwan mm pia naheshimu haki na utu wa mwanamke duniani.
Lakini tatizo lako haliapply kwa shusho hata kidogo.
Mkuu shusho aliolewa akiwa na miaka 19 ambayo kwa mtu ambae hakwenda shule ni mmama .mm by 19 mama yangu alikuwa na 2 kids.
Pili ndoa ni mkataba wenye maadili yake.kinachotokea ni ulimbukeni wa exposure baada ya mafanikio.ntatoa mfano wa wakinga kariakoo.
Wanawake wakinga huwa sio wazuri ni wafupi na shapeless na wanasura za babu.
Sasa wakinga wakiwa kwao huwa hawana exposure wanajikuta wanachagua mke out of love na limited expoure .wanaoa kikristo na wanaanza saka mali na mkewe .
Sababu ni wapiganaji na wabahili wanajikuta wanapata mtaji mkubwa ndani ya 2 to 5yrs .ndo kwa konekshen ya ndugu zao wanaingia kariakoo.
Hapo wanajuana waaminifu sana kuna mkinga nlimlipa milion nkatega kwa kuongeza elfu kumi asee alipiga na simu kabisa .
Sasa wanakopeshana mzigo zana unakuta ndani ya miaka miaka 10 anakuwa bilionaire ashanunua mahotel na migorofa kama yote.
Tatizo sasa anguko la wakinga limepatikana vyema .ni walaini kwa pisi kali unakuta wanaacha wake zao ili waoe mislay qeen.yaan wakinga ndo madanga wa makahaba dar.
Hapo wamejikuta wanajiingiza kwenye starehe na wengi nawajua wameachana na ndoa na wamefilisika.
Nini point yangu? Ndoa ukiifunga hususan ya kikristo ni mkataba na Mungu .biblia haiatoa takwa la mwanamke kumpenda mume limeagiza kumuheshimu.kupenda ni jambo la wanaume .mara ngapi mwanamke asie kupenda ukilala nae tu anabadilika ? Mwanaume kwa manamke asiempenda hata atoe tigo haisaidii.
Ukiingia na mtu ndoa ya kikristo kama ulikosea au uliingia kwa dhiki kaa na ndoa yako kuheshimu mungu sio mume.
Shusho aliolewa akiwa na umri wa kufanya maaamuzi 19 akamuapia mume kwa mungu .leo ametenda dhambi isiyo na msamaha inaitwa KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU.Yaan kusema mungu alimuonesha avunje ndoa akamtumikie .dhambi ya kumsingizia mungu uongo
 

Nimesoma post yako kama nusu tu nikaona huna uelewa wa mambo ya Ndoa hivyo huna sifa ya kuandika mambo yanayo husiana na ushauri wa ndoa; unge endelea na yale mengine ya kisiasa
1. Kudhibitisha kuwa huna sifa ya kuongelea mambo ya Ndoa, umeweza kumsikiliza Christina Shusho na kuamini kila anachosema na kutoa hukumu wakati hujasikiliza upande wa pili wa mUme wake
2. Kwa maelezo yako ni kuwa, mwanamke asiolewe kama hana kazi au niseme wanaume wasije kuoa wanawake wasio na kazi au Kipato; sijui unajua ni asilimia ngapi ya wanawake au niseme vijana wenye kazi?
3. Kama unafikiri mtu akioa mke kwa sababu anataka asifanye dhambi ya kuzini mtaani ananyanyasa mke wake kwani anataka kufanya tendo la ndoa; inabidi ujitafakari upya...
4. Hiyo ya kusema mke asilipiwe mahari sijui umetoa wapi????
5. Kwa wenye maarifa wanajua kuwa, masuala ya ndoa sio mepesi kama kuongelea Siasa au pengine kuongelea mpira wa Yanga & Simba
 
Tafuta Hela Wewe mke wa Bure Bila mahari hayupo

Mahari unapangiwa kupima uwezo wako moja je una kipato Cha kutunza familia? Ukisema huna Hela ya mahari tu huyo mkeo atakula Mawe akija kwako?

Ndio.maana Hadi wachungaji wafungisha ndoa huuliza kama huyo mwanaume mahari alilipa au la kuwa hawamdai chochote Kabla kufungisha ndoa

Mahari tu inakushinda hiyo familia utatunzaje unataka mke akajiuze au?

Mahari ni interview kupima kama una kipato Cha kutunza familia huna wazazi wanaojielewa watagoma kuwa hatutaki aoe mtoto wetu sababu waweza kuwa mzigo Kwa wakwe wanunue Hadi chakula wakuletee Wewe lofa mkubwa ule na mkeo

Huna Hela ya mahari lofa Wewe nenda kawe padri wa kanisa katoliki ambao Hawaoi achana na ndoto za kuoa bure
 
Mkuu kabla sijadandia naomba unijuze unaposema kuolewa kama mtumwa unamaanisha nini?
Ina maana tina ameolewa kabla ya kutimiza miaka 18?
Namkumbuka alikuwa maarufu kwa wimbo wake wa UNIKUMBUKE
Je wakati anaibuka kuwa maarufu alikuwa ameolewa au alikuwa kwa wazazi wake?
 

Mkuu, mada imetolewa kulingana na maelezo ya shusho mwenyewe. Kuhusu uhakika hilo sio juu yetu. Tunajadili kile ambacho amekifanya na kile ambacho ndani ya jamii tunakuomba.

Shusho ametoa hoja zake. Hoja kuu ni hizi za kuachana na mumewe;
1. Alilazimishwa kuolewa na wazazi
2. Kutimiza ndoto yake ya kumtumikia Mungu.

Mada yangu imejikita katika hoja yake ya kwanza kuwa uhuru wake wa kuchagua mwenza uliingiliwa.
Na hiki anachokifanya ni matokeo tuu ya kile alichotaka ni siku nyingi ajikomboe apate uhuru wake.

Kuhusu Mungu wake hilo silijui. Sijui anamtumikia mungu yupi na kama amebadili Mungu pia huyo mungu wake mpya simjui. Hapa ninajadili vitu vilivyowazi na dhahiri.

Hoja ya uhakika wa kupendwa au kutokupendwa hilo wala sio jambo gumu. Kujua mtu anayekupenda ni rahisi mno.

Kuhusu kuchapiwa hiyo haipo ndani ya uhuru wangu. Kila mtu anahaki ya kutumia mwili wake atakavyo. Hiyo ni Haki. Lakini kama nikijua mke wangu anachapwa yaani ametumia uhuru wake kutumia mwili wake kula na mtu mwingine mimi nami nitafanya maamuzi yangu ambayo hayataingilia uhuru wa mtu mwingine na wala kuvunja sheria za nchi na Mungu ninayemuamini.
 
Huwezi panga kumpenda mtu inakuja automatic
Tunaongelea upendo wa kwenye mahusiano na sio wa baba kwa mtoto
Unatakiwa ujue kuna aina nyingi za upendo
Watoto ndiyo wanadhani upendo wa mwanamke na mwanaume huja automatically. Ukiwa mtu mzima utajua watu wanapendeana, pesa, sura, matako, elimu, tabia, macho, swaga, umaarufu, nk nk. Na anayempendea mtu pesa na anayempendea mwingine matako hawana tofauti. Hakuna mwenye upendo wa kweli zaidi ya mwingine.
 
Mwanamke kuna mda inabidi akubali kuolewa na mwanaume flani sababu ndo aliyekuja na yuko tayari kumuoa sasa unavyosema mwanamke awe na uhuru ni kichekesho kwakweli
Kama alikubali bila kulazimishwa hilo halina Tatizo, ikiwa ni kinyume na hapo huo ni utumwa.

Umeelewa mada lakini mkuu?
 
Ndoa inatakiwa ije na version mpya jamani hii ya zamani ipo outdated sana....haikidhi wala kuendana na nyakati za sasa.
 

Kulazimishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…