Andika hapa ndoto zako za usiku ili kukicha uweze kutafsiriwa

Andika hapa ndoto zako za usiku ili kukicha uweze kutafsiriwa

Kuota ngombe wanachinjwa nyumban kwako wameizunguka nyumba
Ilikuwa inakuonyesha kwamba watu wema humalizwa na watu wachache wabaya na pia sio kila anayeadhibiwa ni mkosefu wengine wanaonewa tu na watu wenye uwezo wa kufanya ivo kwaiyo inakupa onyo kwepa sana mazingira ya ivo
 
fafanua hii umenieleza kwa kifupi sana
Kwa mfano umegombana na mke/mme wako unaanza kusema kwa rafiki yako, umegombana na familia yako unaanza kutangaza kwa watu, umepigwa kibuti unalalama kwa watu, maisha yamekugomea unamwambia kila mtu hata kama hana msaada ndoto imekuonya vitu vya aina hii na vinginevyo
 
Vitoto vingi humu ni vishirikina,
Kuna ID humu naoteshwa inaroga mpaka mapaka halafu ni katoto tuu.
 
Kumuota mpenzi wako wa zamani Kila Mara zaidi ya Mara kumi Nini tafsiri yake.
 
Mkuu Folk Part II

Sijui kama ndoto hii imeshaulizwa humu maana naamini ni ndoto ya kawaida kwa watu wengi japo ina version mbalimbali.

Unaota upo shule ya primary/o'level/A'level/chuoni. Vividly kabisa na washikaji. Mara ni siku ya mtihani wenzako wanafanya mtihani wewe mara huna kalamu, mara darasa hulioni au mwalimu anakukatalia kuingia kwenye chumba cha mtihani ali mradi vurugu tupu.

Au ukiingia kwenye chumba cha mtihani unakuta mtihani ni mgumu hatari huwezi hata swali moja wakati wenzio wameanza kumaliza na kukusanya kazi zao wewe bado unahangaika tu.

Na mara nyingi katika ndoto hizi za shule unakuwa unamwota mtu au watu wale wale. Yaani kila ukiota wahusika ni wale wale!

Na hii. Unajaribu kuwahi airport lakini kunakuwa na ishu. Mara passport huioni. Mara mizigo yako ina matatizo au ndege mbovu...ali mradi tu mpaka wengine watasafiri we bado unahangaika.

Asante sana
 
Ndoto namba 1 kuhusu raisi kikwete

hii ilikuwa ina kuonyesha na kukumbusha kwamba ubinadamu ndo kitu cha msingi zaidi. Hata siku ukiwa na mali nyingi, vyeo vikubwa, ukiwa boss kazini usiwadharau waliochini yako waheshimu tu

Ndoto namba 2 kuhusu binti na sufuria

Kiroho ilikuwa inakuonyesha kwamba upendo au faraja ni kitu cha muhimu sana kwa watu wengine kwa kuwazawadia au kuwapa msaada na unapowasaidia kuwapa msaada uonyeshe furaha sio kuanza kuwasema vibaya au unakunja sura
Chondechonde isikupeleke kwamba ni siku ya harusi unavikwa pete hii itakuwa tafsiri ya kimazingira na sio kiroho

ndoto namba 3 kuhusu jamaa yako aliefariki

kiroho ilikuwa imekuonyesha vitu vi3 1. Nguvu ya kufanya maamuzi 2.haki 3.kila penye kizuri au kibaya pana chuki

1. Nguvu
ili ufanye vitu vyako na viende unahitaji pawa ya hicho kitu husika pawa zenyewe zaweza kua pesa, cheo, elimu n.k ndo maana kwenye ndoto boss wako alifanya maamuzi bila kupingwa

2.haki
umeonyweshwa kwenye ndoto kuwa kwa sasa mambo mengi hayaendi kwa haki kama inavyotakiwa. Ndoto inakufungua ni jinsi gani inabidi upate kitu hata kama si haki yako. Labda kwa kutumia undugu, kujenga urafiki na mwenye sekta husika. Kutumia pesa ila cha msingi upate unachokitaka

3. Chuki

umeonyeshwa kwamba unavopiga hatua moja kwenda nyingine maadui wengi ni watu wako wa karibu hapo unakumbushwa kuwa makini nao na kuishi nao kwa akili


ndoto namba 4 kumhusu mama yake binti

ulikuwa unakumbushwa kwamba sio kwamba rafiki zako ambao unastarehe nao na kura raha nao watakuwa msaada kwenye shida wengi wao huteleza ila wale uliopita nao kwenye magumu na kuwasaidia huwa ni faraja wakati wa shida na kwenye ndoto umeonyeshwa kujali mtu mwenye shida ni jambo jema hata kwa mtu mwingine tofauti na huyo mama yake binti
Asante Mkuu umefafanua vyema sana Allah (SAW) akubariki sana. Sasa hapo kwenye hio ishu ya Boss hapo kuna siku niliota tena Barua ya Kuitwa Kazini ikiwa na jina na shahihi ya Waziri wa Wizara husika pamoja na Sahihi ya huyo Boss na hii ilikuwa na maaana gani ? Japo hata huko kazini mpaka leo sijaitwa. Na hata hivyo siwaziii sana kuhusu hili
 
Back
Top Bottom