Andiko hili katika Biblia ndio kifungu katili zaidi kuwepo Duniani. Je, ni kweli Mungu aliamrisha ukatili wa namna hii?

Andiko hili katika Biblia ndio kifungu katili zaidi kuwepo Duniani. Je, ni kweli Mungu aliamrisha ukatili wa namna hii?

Status
Not open for further replies.
Mungu haonei.

Biblia Iko wazi.

Kwa vipindi tofauti Waamaleki waliwavamia Wana Israel na kuwapiga na kuwapora mali zao kipindi hiko waisrael wamemwasi Mungu.

Waliipoanza kumlilia Mungu na kumwomba Awasamehe dhambi zao.

Ndio Mungu anawaamuri wawachakaze Waamaleki.

Kwa msiiosoma maandiko, Waamaleki walikua eneo la NEGEV NA SINAI YA SASA..

Waamuzi 6:3---7 ....
Basi ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepanda mashamba, Wamidiani wakakwea, na Waamaleki, na hao wana wa mashariki; wakakwea juu yao;

wakapanga marago juu yao, na kuyaharibu hayo maongeo ya nchi, hata ufikapo Gaza,( Gaza hii ndio hii hii ya Leo ambayo Wapalestina wanasema ni yao, hakika Israel aendeleze kichapo tu na aichukie Gaza) wala hawakuacha katika Israeli riziki ziwazo zote; kondoo, wala ng'ombe, wala punda.

Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.

Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia Bwana.


Baada ya hapo Kichapo kikawashukia Waamalaki na Mungu akakifita kizazi chote Cha Amaleki, uzao wa ESAU.🤣🤣🤣

Hili Taifa ni la Mungu
 
Wanadai Yesu ni Mungu anaupendo na huruma , sasa huruma Iko wapi mpaka kwa vitoto vimekosa Nini ?
Hizo ni hadithi sawa tu na Alfu lela ulela.

Hizo habari hazipo, hazijawahi kuwepo na hazitakuja kuwepo, Ni kazi za ubuni [Fasihi Andishi].

Work of Fictions.

Nuhu alitengeneza jahazi vipimo vyake hivi hapa .
 
Wanao tenda dhambi na maovu ni maadui wa Mungu.

Ndiyo maana ata ukisoma biblia unaona kwamba Mungu alitafuta kisa kati ya Samson na wafilisiti Ili Samson apate kuwa uwa

Daudi naye pia hivyo hivyo shughuli yake ilikuwa kuwa angamiza maadui wa Mungu.
Acheni upuuzi, huyo Mungu ni katili namna gani?, haya hao watu waliofanya makosa je watoto wadogo,wanyama na mali zisizohusika na hao watenda dhambi haki Yao ikoje?, Hamuoni kuwa Mungu wenu anajipinga mwenyewe ktk maandiko aliposena Uovu wa mtu hautorithiwa kwa mwana? Hapo hapo Kuna mistari inayosema uovu wa mtu utaadhibiwa mpka vizazi vi4, je lipi ni sahihi?.

Ni muda Sasa wa waafrika kuamka na kuzikataa hizi TAKATAKA tulizokalilishwa na wazungu wakituaminisha ndio utakatifu, kumbe Ushenzi mtupu.

Ukristo+uislam ndio chanzo cha maovu hapa duniani, maajabu hutoona wale wanaoitwa wapagani wakifanya unyama kwa viumbe wengine, Bali ni hao wafia dini wanaojiita watu wema na watenda mema na Mungu wao mwenye huruma, lkn matendo Yao ni zaidi ya ushetani.

Hata maandiko yenu yanaprove kuwa huyo Mungu wenu wa ukristo+uislam ndiye aliyeangamiza maisha ya watu+wanyama wengi wasio na hatia kuliko hata huyo shetan anaeitwa mbaya na muovu, Sasa sijui Kati ya Mungu na shetan ni yupi muovu.

Maajabu pia Kuna maelfu ya dini na Imani, lkn hutoona zikifanya wala kufundisha maovu na chuki kama hizi dini zenu za kishetani za Abraham(uyahudi, ukristo, uislam), hizi dini ni hovyo kabisa.

Huu ni muda wa watu kuamka na kuujua ukweli
 
Mungu wa Wayahudi na Waarabu ni katili sana, ila Mungu wa Wayahudi yeye hacheki na wowote
 
Jamaa walipokuwa wakitoka misri Kuna mahala Mungu alikasirika mno akapata kuwa hakuna mwanaume aliye juu sijui ya 18yrs atakayeioma Ile nchi ya ahadi so wote watafia njiani.
Mungu wa majeshi so majeshi yote ni ya Mungu na sio wahasibu,walimuona,wahandisi,mahakimu wala.wafanyabiashara Bali ni Mungu ama baba yetu wa majeshi. Kuna mdau mmoja akasema kuwa ukimchunguza sana Mungu utashindwa kumuabudu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom