Anna Elisha Mghwira anarudi ACT? CCM atakaa kama mwanachama wa kawaida? Vitawezekana kweli?

ACT na CCM hakuna Tofauti tofauti yao ni Rangi za bendera tu vyote sio Vyama vya Upinzani
 
Uko sahihi lakini kwenye kule wajukuu UACHE keki ya uRC kweli? Mbona keki tamu ile?
 
Unajua kuna mentality mbaya sana kwamba mwanasiasa kustaafu kwake mpaka afariki.

Sasa ikitokea kama hivi, ndio drama zinaanza mara kafukuzwa, kakataliwa au katemwa.
 
Huenda waliwahi kunyang'anyana.....
 
Hivi ni vyeo vya furaha ya Rais. At the president pleasure. Haviulizwi ni kwa furaha yake tu ameamua kumzawadia mmoja wa wastaafu cheo wakati wengine wakiendelea na ustaafu wao.

Ni kama wewe umewakuta omba omba wawili barabarani mmoja ukampa msaada mmoja na mwingine ukamwacha hakuna atakayekughasi. Hiyo ni kwa furaha yako.

Na sisi tusiighasi furaha ya raisi.
 
Ukweapo wasalimie vizuri unaowapita njiani ili wakati wa anguko wakupokee. Sijui mama aliwasalimia au la. Ninahisi atapata kimwanya kengine humohumo CCM.
 

Daaaah Kuliacha hilo Puto ni shegeda.

 
Unajua kuna mentality mbaya sana kwamba mwanasiasa kustaafu kwake mpaka afariki.

Sasa ikitokea kama hivi, ndio drama zinaanza mara kafukuzwa, kakataliwa au katemwa.
Ndugu Mkaruka any permanent withdrawal from a particular work-force is considered a retirement.
Sasa naona ndugu yangu Erythrocyte amekomaa sana na umri tu wakati kuna mengine mengi.

Mwanasiasa kwenye ngazi za uteuzi Tenure yake hutegemea Pleasure of the President,
Tofauti na teuzi nyingine ambazo ziko kisheria na hutoa muda maalum wa Tenure.

Kama ulivyosema, kuna tatizo kubwa sana kimtazamo hapa Tanzania.........
 
Sisi shida yetu ni kufahamishwa tu , lakini hizi lugha zenu za vijana kustaafu huku wazee wakiajiriwa kwenye nafasi zile zile tunashindwa kuelewa , wala hatuna ugomvi wowote na maamuzi yenu
 
Sisi shida yetu ni kufahamishwa tu , lakini hizi lugha zenu za vijana kustaafu huku wazee wakiajiriwa kwenye nafasi zile zile tunashindwa kuelewa , wala hatuna ugomvi wowote na maamuzi yenu
Mkuu mimi sikulaumu, wala sikuhumu......

Ila nachosema, you should have known better ndugu Erythrocyte, kwa nafasi ya ushawishi uliyonayo mbele ya jamii ya kitanzania tunategemea uwe unafanya tafiti za kutosha kabla ya kuandika kitu ambacho kinaweza taharuki au kuchanganya (Negative Connotation) watanzania wenye uelewa mdogo.

Lakini ukiendelea kukishupalia huku na kule, sisi wengine tunaweza kutafasiri kwamba una ajenda yako binafsi. Nafahamu wewe ni msomi mzuri tu, and I hope hili utalizingatia na kuweka weledi mbele..........

Huu ni ushauri tu.......
 
Mimi kwenye andiko lile ( ambalo hata hivyo wakubwa wameli merge ) niliuliza katika hali ya kushangaa tu na wala sikuwa na ajenda nyuma ya pazia , nadhani unanifahamu vizuri , nikiwa na ajenda yangu huwa simung'unyi maneno na wala siji na mafumbo yoyote yale , natoboa hadharani bila kuficha .

Sasa labda ili nisionekane mbaya basi labda nisiwe nahoji haya masuala yenu yanayohusu teuzi za viongozi japo wanateuliwa kwenye nafasi za umma .
 
Mnyatutu huyu anaenda cheza na wajukuu zake, si lazma siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…