Anna Tibaijuka: Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential, tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga!

Anna Tibaijuka: Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential, tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga!

Itabdi uwape somo sana watanzania hawajui chochote kwa kweli.
Kwa kweli kwenye hili, nimejitahidi sana,
Karibu sana pande hizi
Kwanza nilianzia hapa, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

ikaja kuwaomba waheshimiwa wabunge wetu, kwenye kuridhia IGA ya DPW, watangulize mbele maslahi ya taifa Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!.

Na baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia mkataba huo bila kufanya due diligence yoyote kumhusu Mwarabu wa Dubai na hadhi ya mkataba wenyewe, kwanza nikasisitiza kuunga mkono hoja, Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?.

Kisha nikahoji uwezo wa Bunge letu na uwezo wa wabunge wetu kujadili jambo kubwa kama hili Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? .

Pia nikatoa angalizo la maeneo yenye ukakasi ili HGA iwe imenyooka Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! na kesho Jumapili, nitaandika makala kwenye gazeti la Nipashe kuhusu huu mkataba
P
 
Nisubiri kitu gani wakati mkataba umeshakuwa unatekelezwa tangu October 2022?
Ndio maana nimewashauri Watanzania wanahitaji elimu ya mikataba, ile IGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkataba ni HGA, bado!.
Hiyo miaka yako 30 unaiweka kwa mapenzi yako tu, niambie umeiona wapi kwenye yale makubaliano yaliyowafanya DP World waanze utekelezaji wao tangu mwaka jana?
Kuna vitu ukiwa hujui ndio utashangaa miaka 30 na kuiona mingi!. Unaujua mkataba wa bomba la gesi ni wa miaka mingapi? Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ya Mkopo wa Exim Bank-China ni "Changa la Macho?!".
Kwenye yale makubaliano ya mwaka jana, Article 23 inazungumzia duration and termination, ambapo hapo hawajaweka muda maalum wa kwisha mkataba, kama ni miaka miwili, tatu, tano, kumi au 100..
Duration haiwekwi kwenye IGA, duration inawekwa kwenye HGA
Wao wamezungumzia tu kwamba, mkataba unaweza kwisha pakiwepo na permanent cessation of all project activities, sasa hebu niambie, hizo project activities zinaweza seize vipi? au mpaka pale maji ya bahari na maziwa yatapokauka?!
No sio hivyo, HGA itaweka projects na duration, project zote zikikamilika ndipo mkataba unakwisha.
Ok, bado kipengele kidogo cha kwanza kwenye hiyo article 23 niliyokupa kinasema, mwarabu anaweza kuamua kuendelea kuwepo akiona bado anacho cha kuvuna, hata kama maji ya bahari na maziwa yatakauka!.
Yes kwasababu anaweza kutengeneza bahati!, Bandari ya Dubai ni artificial port, imetengenezwa, ndio the biggest artificial port in the world!.
P
 
Prof Anna Tibaijuka anasema Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential so tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga

Tibaijuka anasema kupitia Ukurasa wake wa twitter kwamba bado ana Imani Mkataba Huo wa DP World utarekebishwa kwa kutumia Wataalamu Wetu wa Uchumi

Mlale unono!
Anna Tibaijuka !! Nakumbuka statement zake mbili tofauti alizozitoa ndani ya masaa yasiyozidi 24 kwenye Radio moja hapa Nchini !

Kwanza alisema huko Umoja wa mataifa kipo kitengo chenye kutoa msaada wa kurekebisha mikataba inayoonekana ni ya kinyonyaji ambayo Nchi husika iliingia kichwa kichwa !

Next day nikamsikia akisema tofauti kabisa na alichokisema jana yake kuhusu hiyo mikataba ya madini iliyokuwa ikilalamikiwa sana na wananchi !
Ilikuwa ni katika awamu ya nne !!!
WanasiHasa ni shida kuwaelewa !!
 
Kwa kweli kwenye hili, nimejitahidi sana,
Karibu sana pande hizi
Kwanza nilianzia hapa, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

ikaja kuwaomba waheshimiwa wabunge wetu, kwenye kuridhia IGA ya DPW, watangulize mbele maslahi ya taifa Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!.

Na baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia mkataba huo bila kufanya due diligence yoyote kumhusu Mwarabu wa Dubai na hadhi ya mkataba wenyewe, kwanza nikasisitiza kuunga mkono hoja, Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?.

Kisha nikahoji uwezo wa Bunge letu na uwezo wa wabunge wetu kujadili jambo kubwa kama hili Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? .

Pia nikatoa angalizo la maeneo yenye ukakasi ili HGA iwe imenyooka Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! na kesho Jumapili, nitaandika makala kwenye gazeti la Nipashe kuhusu huu mkataba
P
Japo unajitaidi sana kuielimisha jamii kuhusu mikataba lakini watanzania walio wengi pamoja na wewe unazungumzia tu upande mmoja wa uhalali wa mikataba kutokana na nature ya mikataba ya kibiashara ilivyo kokote duniani hata hapa kwetu kwenye mabank na mikopo ya taasisi ndogondogo.

Kiualisia mkopo wa kibiashara lazima uwe na masharti, hakuna anayepinga hilo, Ila Shida kubwa inakuja kwenye ambavyo makampuni au taasisi tunazoingia nazo hiyo mikataba kutuzidi ujanja wa vipengele vya mkataba,uongo kwenye utekelezaji,uongo kwenye ukadiliaji,uongo wa kitaalamu.

Unakuta kampuni fulani inakuja Kwa staili ya utafiti inaleta wataalamu na wakishafanikisha ugunduzi wao wanaleta taarifa serikalini yenye chumvi au limao na ukishawapa Mladi hauleti matokeo yaliyotarajiwa au unatoa matarajio ya ziada lakini kwenye mikataba unakuta Hakuna hivyo vipengele.
 
Sio Dubai Tu hata Zanzibar Ports Authority ni Mshindani Mkubwa na wa karibu kabisa Wa Tanzania Ports Authority kwa bandari za Tanganyika
Ndio maana kuna watu wengi lengo mzigo ni kuleta Tanganyika lakini wanashushia makontena Zanzibar kisha wanaleta kama Loose cargo huku Tanganyika kutumia majahazi kwa kutumia Smuggling practices kwenye bandari bubu

Pia Zanzibar wana lengo la kujenga bandari kubwa zaidi
Hivyo ni hatari sana kwa Wazanzibar kuamua hatima ya bandari shindani kwao Watanganyika
Ndio maana wanataka kuzitoa sadaka kwa wajomba zao waarabu wakati huo huo za Zanzibar zipo salama chini ya SMZ kwa maslahi mapana ya Wazanzibar peke yao daima dumu

NB
Tanganyika = Zanzibar
Tanzania Bara = Tanzania Visiwani

Kama kuna jina la Zanzibar mwenzie Tanganyika.
 
Unapotosha.

Kwenye ule mkataba,
Mkuu denooJ , mjinga ni mtu asiyejua, mtu kuwa mjinga sio kosa!, mjinga akiisha elimishwa, ujinga unamtoka anakuwa mweruvu, mjinga anayeelimishwa ujinga isipomtoka, huyo sasa sio mjinga!. Naomba nikuelimishe kwa mara ya mwisho, IGA sio mkataba ni MoU ya makubaliano ya kuingia mkataba wa HGA, mkataba ndio kila kitu, naomba tusiendelee kuijadili IGA, subirieni HGA!. Naomba niwaibie tuu kuwa HGA, DPW anapewa tuu kitengo cha ma container terminal only!.
Part 2 General Obligations, na Article 2 ya ule mkataba, pale kwenye Objectives of the Agreement, panatamka wazi kabisa, Waarabu wamekabidhiwa ports zote za maziwa na bahari waziendeshe Tanzania Bara yote, tangu October 2022.
Lengo la agreement ni kuonyeshea nia lakini HGA ndio itasema anagaiwa nini. Wakati unapanga kuoa pia mnapanga mpate watoto wangapi, sisi tulipanga watoto wawili, tulipopata tuhahamia UK, then US, wakaendelea kuongezeka sasa wako 9!.

IGA inaweza kuweka nia yoyote lakini HGA ndio mkataba, tusubirie mkataba!.
Wanaziendesha kwenye maeneo yafuatayo kulingana na makubaliano;

Development, improvement, management, and operation of lake ports, special economic zones, logistic parks, trade corridors...
Hii ni nia tuu, mkataba utaeleza.
Inshort, Samia msaliti amewakabidhi wajomba zake kila kitu kwenye bandari zetu zote Tanzania bara.
Tuache upotoshaji jameni, Samia hajakabidhi chochote kwa yeyote!.
P
 
Prof Anna Tibaijuka anasema Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential so tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga

Tibaijuka anasema kupitia Ukurasa wake wa twitter kwamba bado ana Imani Mkataba Huo wa DP World utarekebishwa kwa kutumia Wataalamu Wetu wa Uchumi

Mlale unono!
Bora DP World ajitoe tuu manaa Wajamaa wamefura ,tubakie vile vile na kujikongoja .
 
Huyu Profesa...Milioni 10 pesa ya mboga.

Prof. Tibaijuka
alipokuwa madarakani alitaka kuuza sehemu ya Kigamboni kwa mwekezaji,kwa ajili ya Mradi wa Kigamboni New City project.

Magufuli aliufuta.Mradi.
Mzushi sana huyu mama

Ova
 
Back
Top Bottom