Hapo sijamuwekea hata gia ya
Kiduku Lilo kashaanza kulalamika.
Huyu guluguja lazima fimbo zinamuuma, nikieleza maisha yangu kikawaida tu bila kujua kwamba najisifia, kashaona najisifia.
Kuna watu wako hivyo.
Nakumbuka kuna siku shule Tambaza, nilikuwa naagana na masela.
Nikamwambia mchizi mmoja tulikuwa tunakaa wote Oysterbay "Nitakupigia simu baadaye tuongee". Tulikuwa tunaongea sana,enzi za land line, just for the hell of it.
Yule mchizi ali mind.Naye alikuwa anakaa Oysterbay.
Akasema "Wewe mbona unaleta mambo ya kupigiana simu pale kuna watoto wa Temeke kwao hamna simu?".
Nikawa nashangaa sana.
Sasa kama kwao hakuna simu hilo linakuwaje kosa langu?
Mimi ndiye nilisababisha wakose simu?
Pengine mimi natakiwa niwaamshe wenzangu ambao wanaona simu ni anasa wajue kwamba tunatakiwa kuwasiliana kirahisi kwa simu, na kwamba simu si anasa!
Sasa huyu mshamba anaweza kuniona najigamba hapa, kumbe mimi ni tabia yangu kuongea kwa uhuru kinyamwezi tu bila kujali mshamba yupi atafikiria vipi kuhusu maisha yangu.
Yani mimi nianze kujali mshamba fulani atanifikiria vipi kwa sababu gani?
Namuogopa au vipi?
Tell him to get the fvck outta here!