Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hongereni sana The Gunners, kumfunga Mama Cita goli 5 sio mchezo, sidhani ndani ya hii misimu minne kuna timu nyingine yoyote iliyoweza kumgonga City goli 5.
Mngefanikiwa kumgonga goli 6 ingependeza zaidi tukawapachika rasmi jina la Man6 kama tulivyo wagongaga nyie goli 8 na kuwapachika jina la Arse8.
All in all leo jiji na Manchester limefedheheshwa vibaya mno sio kwa Nyumbu wala hawa dada zake Nyumbu.
 
Nipo safarini, sicheki game.

Hao wanaomtukana kai wamechelewa kumjua, sisi tulisema kai ni kiazi, wao wakabaki na takwimu zao sijui ariel duels, sijui kimeenda kimerudi..
Mie nilishagongelea msumari kai ni kiazi na hafai kuchezea arsenal.

Ni kama vile nilivyopokea matusi wakati nasimama na partey, watu walipiga kelele wee, kiko wapi.

Kai ni kiazi.
Ikiwezekana miaka ya kai ipunguzwe apewe partey
Kiongozi wao ni hamis matakwimu😂, nakumbuka bro uli sema hapa.
 
Hii ndio tofauti yetu sisi na Liverpool. Na ndio maana Liverpool hayupo pale juu kimakosa.. Liverpool kwenye pressing wapo vizuri sana hawajawahi kuridhika.. Ukiingalia hii mechi ni kama vile Arsenal wameridhika na hawataki kuwapress Man city ambayo inaonekana wapo Vulnerable sana. Kuna muda wanacheza back pass ambazo hazina maana wakisubiri man city wafanye makosa ndio watumie nafasi.
we mpira unaangiliaje, kwamba Liverpool ni wazuri kwenye press? huyo sio klopp ni slot
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hongereni sana The Gunners, kumfunga Mama Cita goli 5 sio mchezo, sidhani ndani ya hii misimu minne kuna timu nyingine yoyote iliyoweza kumgonga City goli 5.
Mngefanikiwa kumgonga goli 6 ingependeza zaidi tukawapachika rasmi jina la Man6 kama tulivyo wagongaga nyie goli 8 na kuwapachika jina la Arse8.
All in all leo jiji na Manchester limefedheheshwa vibaya mno sio kwa Nyumbu wala hawa dada zake Nyumbu.
Naona umetukubali kiaina, lakini bado umetusagia kunguni!
 
Wachache wataona hii kwakua tumeshinda
Kweli. Hata Odegaard alikula njano kwa kumkasirikia refa kwa kupuliza filimbi kwa foul baada ya Odegaard kumnyang'anya mpira Silva nje ya 18 yao na kuanzisha shambulizi ambalo huenda lingeisha na goli. Ode aliona kama amepata mpira kihalali kabisa...ila hasira zake zikampa kadi. Nadhani mchezaji wa City asingepewa kadi kwa hali kama ile.
 
Back
Top Bottom