Nadhani hakuna yeyote katika wapenzi wa soka hapa au duniani kote ambaye angekubali utabiri wa kwamba L'pool wangewachapa MANU 4-1, wengi tungesema wanaweza kushinda lakini siyo kwa mabao mengi kiasi hicho. L'pool ni wazuri sana maana kuweza kuzifunga timu mbili bora za Ulaya MANU na RM mabao 8-1 katika muda wa siku chache ni achievement ya hali ya juu. Kama wasingekuwa na vigugumizi vya miguu wanapocheza na vitimu vidogovidogo kama Middlesborough basi wangekuwa wameshika usukani wa EPL.
Liverpool hawaaminiki, yaani hawana consistance. ni vigumu sana kuwatabiria japokuwa ni wazuri sana