Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

GOAL FOR ARSENAL! Fabregas makes it four! He steals in at the near post to meet Bendtner's low cross. Terrible defending, and it's now 4-0!
 
Wakuu,

Leo Arsenal wamecheza mpira mzuri na wa kuamrisha mchezo. Vermaelen ni mchezaji muhimu kwa Arsenal hasa kwenye defence.

Ni faraja kubwa kumuona Eduardo amerudi na ushirikiano wake na Robin Van Persie unaonekana.

Alexandre Song ambae amepewa jukumu la kulinda walinzi wa nyuma au "backfour" ndie bado mpaka sasa anaimarika.

Tatizo la Wigan lilikuwa ni kujihami halafu kushambulia kwa kushtukiza lakini kwa Arsenal siku zote ni kushambulia na kufunga.
 
Teh teh teh Kipofu akiona mwezi inakuwa balaaa kubwa....Hongera kufunga wachovu!
 
...nilijua tu! ndio maana sijatia neno hapa!

Jamani nimetoa pongezi na hata ile mechi na Man Citeh nilitoa pole...sasa leo imekuwa nongwa oooh defense yetu bomba....mumeshau timu hiyo hiyo ilicheza na Man Utd na Man Citeh.....!
 
Thomas-Vermaelen-Arsenal-Wigan-Premier-League_2362488.jpg



Thomas-Vermaelen-Arsenal-Wigan-Premier-League_2362481.jpg



Thomas-Vermaelen-Arsenal-Wigan-Premier-League_2362564.jpg



Eduardo-Arsenal-Wigan-Premier-League_2362554.jpg

 
hawa wigan watashuka daraja wakifanya mchezo manake jamaa wametuachia kabisa kucheza mpira tunavyotaka.mechi ilikuwa rahisi mno siwezi kusema tuna tisha kwani kulikuwa na weakness kwenye finishing sana (van persie).
 
Akikaa vizuri anaweza kumtoa Fabiansk namba 2
fabianski mkali sana mie nilikuwa naona kama anakuwa threat kwa almunia soon,manone mzuri sema hile mechi ni ndogo sana kumpima.arsenal hatuna kipa yule anaweza kufanya match winning type of saves kama wakina van der sar na cech.almunia nadhani hule moto ulikuwa wakumnyang'anya namba leahman tu sikuizi jamaa hajitumii na akifanya mchezo nadhani wenger ataleta namba one mwingine.
 
Teh teh teh Kipofu akiona mwezi inakuwa balaaa kubwa....Hongera kufunga wachovu!

Watu bana!....Arsenal ikifunga...imewafunga wachovu.....Chelsea, ikiwafunga hao hao....mnaita mpambano ulikuwa mkali na vijana wanaonyesha ushindani........!

Masa..mpira haufuti ile kwenye hesabu inaitwa commutative or associative property..i.e. if A=B and B=C, then A=C......mpira ni tofauti kaka!
 
Watu bana!....Arsenal ikifunga...imewafunga wachovu.....Chelsea, ikiwafunga hao hao....mnaita mpambano ulikuwa mkali na vijana wanaonyesha ushindani........!Masa..mpira haufuti ile kwenye hesabu inaitwa commutative or associative property..i.e. if A=B and B=C, then A=C......mpira ni tofauti kaka!

Mzee usifanye sherehe kumfunga Wigan.....subiri ukutane na Tottenham, Liverpool, Chelsea, AV etc (Kumbuka vichapo vya Man City na Utd)
 
Mzee usifanye sherehe kumfunga Wigan.....subiri ukutane na Tottenham, Liverpool, Chelsea, AV etc (Kumbuka vichapo vya Man City na Utd)

Mkuu unapotakiwa kufurahi unatakiwa ufanye hivyo.....ukiwa na msiba unahuzunika accordingly.....vinginevyo maisha hayaendi au?
 
Mkuu unapotakiwa kufurahi unatakiwa ufanye hivyo.....ukiwa na msiba unahuzunika accordingly.....vinginevyo maisha hayaendi au?

...hao ndio wanaotaka mfiwa aendelee kuvaa maguo meusi tuuu maisha yake yote... msiba ushakwisha, uchuro wa nini?...🙂
 
Back
Top Bottom