Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

Hivi huwa hawakazii sana kuwa ukiuwa ni dhambi kubwa sana?
Huko huwa kwenye kuabudu huwa mnaenda kujifunza nini?

Mbona mauwaji yametamalaki hivyo?

Mjitafakari sana huu sio mda wa kuulizana kwanini yanatokea haya bali mumrudie Mungu sana na muogope sana dhambi period
 
Jamii sahv zimeporonyoka sahivi

Ova
 
Kapoteza watoto wawili aliyowalea kwa uchungu jamani 🤕🤕🤕mmoja kafa

Mwingine anaenda vaa overall
Acha uongo!
Amepotea mmoja tu, aliyekufa.

Huyo mwingine atafungwa kifungo kifupi anatoka maana bado infant.
 
Hizi taarifa za kuuana ni kama imekuwa janga la kitaifa
Ilikuwepo tangu zamani, sema taarifa zilikuwa hazisambai kama sasa. Teknolojia imeongeza upatikanaji wa habari
 
Hii Hatar sana,huu mwaka una nini kila siku habar hizi
 
Kijana James mwenye umri wa miaka 16 anatuhumiwa kumuua kaka yake anaitwa Zakayo huku baba mzazi akikiri kushindwa kuwaamua ndugu hao wawili waliokuwa wakigombana kisa mifugo.

Mimi naitwa Paulo Sindio, ni baba mzazi wa watoto hao, walianza kugombana mbele yangu kisa kikiwa ni uswagaji wa mifugo kurudi polini, wote ni Watoto wang una wa mama mmoja.

Akielezea tukio hilo, Paulo amesema: “Walikorofishana baada ya mkubwa kumwambia mdogo kuwa anatakiwa kwenda kuswaga mifugo kauli ambayo ilipingwa na James na baada ya muda wakaanza kupigana.

“Walipigana, mimi nikanyanyuka kwa ajili ya kwenda kuwaamua, kumbe mwenzake tayari alikuwa ameshamchoma kisu kwenye moyo, tulivyompeleka hospitali ikakutwa ameshafariki.

“Sina la kusema, wazee wa ukoo wapo wataamua wenyewe, sina la kufanya, na sijui alipo, kama ameenda kujiua au la sijui alipo. Polisi tayari wana taarifa na wanalifuatilia.”


Source: Globaltv
Ni shida sana
 
Back
Top Bottom