Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

Arusha, amuua kaka yake kwa kisu baba yake akishuhudia

Unapoambiwa zama za mwisho dont think of 10 - 20 years to come. Kwa sasa unaona jambo la uzinzi na wanawake kutembea uchi lilivyo? Bas jua ni bado sana itafika wakati uzinzi utakua unafanyika barabarani na wanawake watatembea uchi kabisa na hapo ndo hasira ya mungu itashuka
Hayo mbona yapo sema hujatembea ukaona. Kuna sehemu ukienda ni exclusive utakayoyakuta huko tena hapa hapa dsm utashangaa. Haya mambo yapo sana hivi una kipindi cha roman empire kulikuwa na sarafu zimewekwa picha ya style mbalimbali ya kufanya ngono, mteja anachofanya ni kumpa malaya sarafu ya style anayotaka.
Zilikuwa zimetengenezwa na serikali. Dunia duara ya kale yanarudi
 
hizi laana kuna watu wametutafutia.

mnamuuaje mtu mzalendo mtegemee mambo kwenda vyema tu!!!!
leo hii polisi 7 wanaua mtu mmoja kisa pesa zake alizotafuta kwa jasho lake.
idadi ya watu wanaokutwa wamekufa bila taarifa inashtusha.

yaani kuna laana hili taifa.
 
Duuh!! Ipo haja ya kujikita kwenye imani zetu kisawa sawa huenda tukawa na maamuzi yasiyo na madhara makubwa namna hii.
 
Acha uongo!
Amepotea mmoja tu, aliyekufa.

Huyo mwingine atafungwa kifungo kifupi anatoka maana bado infant.
Infant??? Infant ni mtoto wa miaka mingapi??
Kijana alikuwa ana miaka 16 ni under age sio infant hivyo atakaa jela ikithibitika mahakamani kwamba ndiye aliyeua.Bado hajakamatwa.Alikimbia baada ya tukio.
 
Sasa mikasa,mauaji kama haya utasingizia utawala

Ilaumu jamii

Ova
Hapana, kuna abnormal different things are happening. Mdau hapo juu amesema kila tawala huja na roho zake.
Naweza kuamini
 
Right from the start kwa wenye kuamini dini .Watoto wa Adam mmoja alimuua mwenzake.
Vita vya kwanza vya dunia inakadiriwa walikufa watu milioni 7.
Vita vya pili vya dunia inakadiriwa walikufa watu milioni 50.
Idadi ya watu inavyozidi kuongezeka,mmomonyoko wa maadili,hali ngumu ya maisha na uhuru wa vyombo vya habari kwenye kuripoti matukio umefanya tuone matukio ni mengi lakini ni matokeo ya dunia ilivyo sasa hivi.
Zamani jamii zilikuwa zinasaidiana kulea watoto.Wazee wa kijiji na mijini walikuwa na sauti kwenye kulea kwa kutoa ushauri na hata ikibidi kuingilia kati wakiona mambo yanakwenda mrama.
Siku hizi thubutu huwezi kusema lolote kuhusu watoto wasiokuwa chini ya himaya yako.
 
Infant??? Infant ni mtoto wa miaka mingapi??
Kijana alikuwa ana miaka 16 ni under age sio infant hivyo atakaa jela ikithibitika mahakamani kwamba ndiye aliyeua.Bado hajakamatwa.Alikimbia baada ya tukio.
Atakaa mwaka mmoja au miwili anaachiwa maana bado anahesabika under 18.
 
Kijana James mwenye umri wa miaka 16 anatuhumiwa kumuua kaka yake anaitwa Zakayo huku baba mzazi akikiri kushindwa kuwaamua ndugu hao wawili waliokuwa wakigombana kisa mifugo.

Mimi naitwa Paulo Sindio, ni baba mzazi wa watoto hao, walianza kugombana mbele yangu kisa kikiwa ni uswagaji wa mifugo kurudi porini, wote ni Watoto wangu wa mama mmoja.

Akielezea tukio hilo, Paulo amesema: “Walikorofishana baada ya mkubwa kumwambia mdogo kuwa anatakiwa kwenda kuswaga mifugo kauli ambayo ilipingwa na James na baada ya muda wakaanza kupigana.

“Walipigana, mimi nikanyanyuka kwa ajili ya kwenda kuwaamua, kumbe mwenzake tayari alikuwa ameshamchoma kisu kwenye moyo, tulivyompeleka hospitali ikakutwa ameshafariki.

“Sina la kusema, wazee wa ukoo wapo wataamua wenyewe, sina la kufanya, na sijui alipo, kama ameenda kujiua au la sijui alipo. Polisi tayari wana taarifa na wanalifuatilia.”


Source: Globaltv
Mara ya mwisho Mungu kutajwa na serikali ilikua wiki mbili kambla ya Mzee kuugua,.
Taifa lililokua likimtegemea Mungu limempa kidogo, tunahitaji toba,
 
Kisha wale malaika wakamwambia Loti: " Je, una mtu mwingine yeyote hapa? Wakwe zako, wanao, mabinti wako, na watu wengine wowote wa ukoo jijini, waondoe mahali hapa! Kwa maana tutaliangamiza jiji hili, kwa sababu kilio dhidi ya wakaaji wake kwa kweli kimekuwa kikubwa sana mbele za Mungu, hivi kwamba Mungu ametutuma tuliangamize jiji hili"
Kwa hiyo Loti akatoka nje na kuanza kuzungumza na wakwe zake ambao wangewaoa mabinti zake, akawaambia tena na tena: "Ondokeni! Ondokeni mahali hapa, kwa sababu Mungu ataliangamiza jiji hili!" Lakini machoni pa wakwe zake alionekana kama mtu anayefanya mzaha.
 
Back
Top Bottom