ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Uliisha wahi kutoa rushwa? Ujue kabisa wale watu walimnyanganya simu, alafu wanakulinda muda wote wa kukupeleka benk.
 
mzee laki 7 kwa mwezi ndogo?
 
Jambo la msingi watanzania tujifunze kuwa wazalendo na kuachana na mambo ya kialifu vinginevyo watu wakiwa wanatimiza majukumu yao mtawaona wabaya mnawashawishi wenyewe kuwapa pesa ili wawaache na kwanini utoe hongo acha uhalifu au kubali kupelekwa mahakamani ukapate haki yako..
 
Rushwa na uporaji ndio maisha halisi ya askari polisi karibia 90%

Hiki kilichomtokea profesa ndio maisha waliyozea wananchi wa kawaida.

Humo kwenye vituo vya polisi kuna mambo ya kusikitisha sana.

Polisi wana njaa sana
Nakubali, mara nyingi nimepita na gari kwakweli pembeni mwa barabara mabadiliko ni makubwa sana, hata sipaelewi tena wakati kipindi hicho hayo maeneo ilikuwa mbuga tu
 
Daah ndiyo maana yule afande (dada flani nilimuona kwenye clip) alikuwa anawapa za uso kwamba kama ni njaa badala ya kufungua akaunti kwenye mifuko ya watu waende bank.. [emoji23] [emoji23] Anasema hizi njaa njaaa zenuu hizi...
 
Huyu mzee atarudishiwa tu
Ana watu wazito watamsaidia
Inasemekana kuna askari mmoja
Naye alichukua gawio katoka nduki
Ila tu ukifatilia na kumsikia huyu mzee
Kuna mtu wa karibu anayemjua alimtengenezea huu mchongo

Ova
Tatizo kwa njaa za hao polisi, je hiyo pesa bado itakuwepo? Hawajapiga mgao kweli na wakubwa zao? Halafu issue iluvyofumuka si watakuwa wametumia hizi hizo pesa kujaribu kuizima??
 
Polisi wa Arusha majambazi wengi sana mbaya zaidi mchongo unaanzia bank wanakuja huku wakijua una shilingi ngapi huo mchezo hata yule Mkuu wa wilaya hai kaucheza sana kujifanya kufatilia risit za tra watu wamelia mno...
Dawa yake inachemka huyo mmasai ataenda kuchunga ng'ombe muda sio mrefu.
 
Madhara ya kuwapeleka Depo watu wasio na maadili ndiyo haya sasa.
Yaani jeshi la polisi linahitaji reform ya hali ya juu, haiwezekani misingi ya ajira ya tangu zamani bado iendelee kuwepo hadi leo, (Eti mtu anaomba kazi kwa barua na kupata mdhamini ambae ni mtendaji wa polisi humo humo) kabla ya kuwaandikisha askari wanatakiwa wawafanyie vetting ya hali ya juu. Bila ya hivyo haya mambo ya rushwa ndani ya vituo vya polisi hayatokwisha hata siku moja.
 
...Nimvekwazika kidogo hapo Mkuu. Kama huyu Profesa naye alikuwa ni Msafi na hana Mazonge zonge yoyote, kwa nini alitaka kuwapa hao makalamba hela yote hiyo wakati moyomi ansjua yupo safi na hana kosa lolote?
Inafikirisha. [emoji848][emoji848]
We ndezi kweli kwahiyo ulitaka mzee akanyee ndoo kwa upuuzi wa hao wajinga, alichofanya mzee ni ku keep low profile then baadae akaibuka kishujaa ndezi wenzako hawana kazi sasa hivi.

Hilo ni fundisho kwa ndezi wengine wenye tabia kama hizo
 
Nakumbuka siku Polisi walinikuta niko maeneo ya viwanja vyangu usiku mmoja, walikuwa askari wasiopungua nane wakiwa na gari lao la doria usiku wa kwenye saa sita saba hivi, mmoja wao alishuka kwenye gari na kuja hadi nilipo, kwavile naonekana kama kachalii na rangi yangu kama msomali flani hivi, aliponifikia akaanza kunikaripia kwa ukali, unafanya nini hapo! Bila kuogopa wala kubabaika nami nikamjibu kwani umeniona nafanya nini, nilikuwa nimevaa jeans flani hivi blue , juu nimevaa pullover hoodie pia la blue lenye kijani mikononi nikiwa natafuna bazooka. Sijakaa vizuri jamaa akaniambia tema unachokitafuna. Nami nikamjibu Niteme kwa minajili gani? Na nikamwambia samahani constable naomba tuheshimiane kwasababu hunifahamu na wala nisingependa unifahamu, ila ukitaka tufahamiane basi sio mbaya unaweza kujitambulisha. Basi hakuongeza neno zaidi ya kuniambia samahani nilidhani ni hawa vijana wa kisomali wanatafuna gomba. Ndani ya muda huo huo akaondoka zake. Nilichojifunza ni kwamba hata ikitokea umekutana nao na hakuna kosa lolote ulilofanya, kwanza kabisa usibabaike wala usiogope. Mara nyingi huwa wanajaribu kukuyumbisha ili waone kama utayumba (Psychological), kwani kawaida ya mhalifu hata kama hakuna kosa alilofanya kwa muda huo lakini lazima atajishtukia.
 
Your browser is not able to display this video.


Kati ya watu 9 walioshiriki uharamia huu, watatu ni mabaunsa wa Sabaya na wengine ni askari polisi wa kituo cha USA River. Huyu ni Profesa Justine Maeda, amekua Mhadhiri wa chuo kikuu cha UDSM kwa miaka mingi, baadae akateuliwa kuwa mshauri wa Rais Nyerere, na baadae akawa Mkurugenzi wa UNICEF nchini Zimbabwe hadi alipostaafu.

Sabaya akishirikiana na askari polisi wa kituo cha USA River, walichukua vipande viwili vya mhogo wakavikausha vizuri, wakavipiga msasa na kuving'arisha kwa polish. Kisha wakaingia shambani Profesa huyu na kuviweka kwenye mzinga wa nyuki bila yeye kujua.

Baada ya siku chache wakamfuata na kumtuhumu kwamba anamiliki nyara za serikali ambazo ni pembe za ndovu. Profesa akasema hajawahi hata kuona hizo pembe zinafananaje. Akawaruhusu wapekue nyumba, lakini hawakua na interest ya nyumba, wakaenda moja kwa moja shambani kwenye mizinga ya nyuki na kutoa vipande viwili walivyodai ni pembe za ndovu (kumbe ni mihogo wamepaka polish).

Wakamwambia mzee hii ni kesi ya uhujumu uchumi kwa hiyo ili asipelekwe mahakamani awape TZS 200M. Akasema hana kiasi hicho cha fedha, baada ya kujadiliana wakataka 100M. Mzee wa watu kwa kuogopa kufia jela akaenda bank na kukomba akiba yake yote na kuwapa.

Hivi ndivyo "jambazi" Sabaya alivyotumia mamlala yake vibaya kwa kulindwa na nguvu kutoka juu. Mtu anatoka Hai anaenda kufanya uhalifu mkoa mwingine lakini hachukuliwi hatua yoyote. Juzi nilipoweka orodha ya hoteli alizolala Arusha bila kulipa, nikaambiwa Mwanza, Dodoma, Moshi, Dar, Tanga kote huko amewahi kulala na kugoma kulipa bill ya mamilioni ya shilingi.

Ni aibu sana kwamba kati ya watanzania milioni 60, huyu "jambazi" alionekana anafaa

Credi Malisa GJ

My Take
Mnaomtetea Sabaya fikirieni kipimwa akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…