Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,021
- 79,710
Kweli mkuu ila kuna kipindi nimezinguana nao nilikuwa na jamaa yangu yupo na manzi wake sasa jamaa huwa mzee wake ana store ya mazao maeneo ya Mbauda Arusha.huu ndio uanaume.
usilete ujuaji sana mbele ya askari na usitie unyonge,bali kuwa mtulivu wakati wote.
Siku hiyo jamaa kamwita manzi akaja mtaa na mimi huwa nampa company msela mda mwingi tupo wote mpaka leo hii. Basi siku hiyo akapigiwa simu ilikuwa usiku saa mbili kuwa kuna gari ina gunia kama kumi na mbili za maharage ila ji gari ya majani ya chai hivyo itafika si muda akagungue store mzigo ushushwe.
Tukatoka pale tulipokuwa na jamaa na manzi wake (sio mbali na store) kufika mara gari kweli ikaja mzigo ukashushwa chap na makuli wawili. Ile tumefunga tunataka kuondoka mara ikaja defender huku Arusha naonaga wanatumiaga za Sunny Safari sijui wanakodi au wanahongwa sijui.
Jamaa wakakomaa fungueni kuna mzigo wa magendo umeingizwa ndani. Hapo nilikuwa nishatupia kinywaji moja inatwa zanzi ipo kama amarula siku hizi hakipo vilikuwa vinawekwa kwenye kiroba.
Nikamwambia jamaa yangu usifungue. Halafu hao polisi nikawachana kuwa hatufungui mpaka mtupe search warrant. Jamaa wakakomaa pale nikawaambia tupelekeni mnapotaka hatufungi hapa bila search warrant.
Yule manzi akaanza kulia anaomba watusamehe akakatwa kofi akatulia 😂. Wale askari wakaanza kusema "unajifanya unajua sasa twende pandeni kwenye gari" nikawaambia poa twendeni ila nikawaambia kabla ya hapo ngoja tutoe taarifa home kuwa tumekamatwa.
Jamaa akampigia mshua wake simu akamweleza mshua akasema poa anakuja central. Basi tukapanda kwenye pira manzi alikuwa wa kwanza kupanda akakalia seat zile kama bench nikamwambia akae chini maana jamaa wangemzingua (kama hujawahi pakiwa kwenye pira siku ukikamatwa ukipakiwa usikalie seat utapigwa kama mbwa koko, kaa kwenye floor ya body ya gari).
Basi jamaa wakatekenya ndinga wakaanza kuondoka tumetoka hata sio mbali kabla ya kuingia lami mijamaa ikaona hatulainiki ikatuachia tukasepa zetu.
Sometimes ukiwa na ujasiri na kujua sheria inasaidia. Ila angalia na watu wenyewe kuna askari wengine yupo radhi akuchape shaba ukimbishia.