ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

huu ndio uanaume.

usilete ujuaji sana mbele ya askari na usitie unyonge,bali kuwa mtulivu wakati wote.
Kweli mkuu ila kuna kipindi nimezinguana nao nilikuwa na jamaa yangu yupo na manzi wake sasa jamaa huwa mzee wake ana store ya mazao maeneo ya Mbauda Arusha.

Siku hiyo jamaa kamwita manzi akaja mtaa na mimi huwa nampa company msela mda mwingi tupo wote mpaka leo hii. Basi siku hiyo akapigiwa simu ilikuwa usiku saa mbili kuwa kuna gari ina gunia kama kumi na mbili za maharage ila ji gari ya majani ya chai hivyo itafika si muda akagungue store mzigo ushushwe.

Tukatoka pale tulipokuwa na jamaa na manzi wake (sio mbali na store) kufika mara gari kweli ikaja mzigo ukashushwa chap na makuli wawili. Ile tumefunga tunataka kuondoka mara ikaja defender huku Arusha naonaga wanatumiaga za Sunny Safari sijui wanakodi au wanahongwa sijui.

Jamaa wakakomaa fungueni kuna mzigo wa magendo umeingizwa ndani. Hapo nilikuwa nishatupia kinywaji moja inatwa zanzi ipo kama amarula siku hizi hakipo vilikuwa vinawekwa kwenye kiroba.

Nikamwambia jamaa yangu usifungue. Halafu hao polisi nikawachana kuwa hatufungui mpaka mtupe search warrant. Jamaa wakakomaa pale nikawaambia tupelekeni mnapotaka hatufungi hapa bila search warrant.

Yule manzi akaanza kulia anaomba watusamehe akakatwa kofi akatulia 😂. Wale askari wakaanza kusema "unajifanya unajua sasa twende pandeni kwenye gari" nikawaambia poa twendeni ila nikawaambia kabla ya hapo ngoja tutoe taarifa home kuwa tumekamatwa.

Jamaa akampigia mshua wake simu akamweleza mshua akasema poa anakuja central. Basi tukapanda kwenye pira manzi alikuwa wa kwanza kupanda akakalia seat zile kama bench nikamwambia akae chini maana jamaa wangemzingua (kama hujawahi pakiwa kwenye pira siku ukikamatwa ukipakiwa usikalie seat utapigwa kama mbwa koko, kaa kwenye floor ya body ya gari).

Basi jamaa wakatekenya ndinga wakaanza kuondoka tumetoka hata sio mbali kabla ya kuingia lami mijamaa ikaona hatulainiki ikatuachia tukasepa zetu.

Sometimes ukiwa na ujasiri na kujua sheria inasaidia. Ila angalia na watu wenyewe kuna askari wengine yupo radhi akuchape shaba ukimbishia.
 
Hivi pale maeneo ya NAIC/DANISH kuna shamba linajulikana "Kwa Maeda", ndo nyumbani kwa huyu Mzee? Na Miss Tanzania mmoja miaka ya 93/94 aliitwa Aina Maeda ni binti yake? Long time sana miaka hiyo nilikuwa nikitumwa hapo kuchukua maranda kwa ajili ya banda la kuku... 🤣 🤣

Dah, nimepamisi sana Usa River mitaa ya Danish, Naic, Ngusero, Leganga, ile njia ya kupandishia DikDik kuna shemeji yangu alikuwa na shamba la Mpunga huko nilikuwa nikifunga shule naenda kumpiga tafu kazi za shamba. RAHA SANA ARUSHA man!
Mkuu ni Ngarasero Ngusero ipo mjini. Dik Dik juu huko ukirudi utapasahau pamejengeka sana. Ndio shamba la maeda njia ya kwenda Dik Dik.

Sasa hivi kahamishia warehouse yake na shughuli zake kutoka usa kwenda maji ya chai. Mjanja sana kwasababu sasa hivi maji ya ujenzi ni mwingi.
 
Hao police kwanza inatakiwa watema pesa yote,rpc kajibu kirahisi sana hajaongelea kuhusu pesa kurudishwa sembuse nae kala mgao....police wote tabia zao ni moja
Polisi hapo Usa waonevu sana. Kuna yula alikulaga chuma anaitwa mapunda jamaa muonevu sana walikujaga homu wakambambikizia kesi kaka yangu yani jamaa sitamsahau
 
Kwa kweli bora kuweka hela nje maana Bank zetu hazina siri kabisa
Police wanajuaje kama kuna hela za mteja Bank na wanapitia kirahisi?

Yaani ni kama ile kesi ya Yule Mama alieibiwa hela zake kwenye Simu banking
Ifike mahali watuhumiwa hata kama ni Bank wanatoa Siri za mteja wafunguliwe mashtaka
 
Serikali ya awamu ya 5 imekomesha rushwaaaa.

Kuna mbugila itakuja kusema hii ni awamu ya 6.
Hilo la serkali ya awamu ya tano linakujaje. Rushwa, wizi, na uvunjivu wa sheria hauwezi kusema umeumaliza. Uarabuni wanakata mikono, wanatoa macho, na kukata ndimi, lakini haya yote hayajzuia kuvunja sheria. Uwezekano mkubwa na kupuguza saana haya makosa. lakini kusema yaishe, no way. Hata nchi zilizoendelea bado corruption ipo.
 
Hilo la serkali ya awamu ya tano linakujaje. Rushwa, wizi, na uvunjivu wa sheria hauwezi kusema umeumaliza. Uarabuni wanakata mikono, wanatoa macho, na kukata ndimi, lakini haya yote hayajzuia kuvunja sheria. Uwezekano mkubwa na kupuguza saana haya makosa. lakini kusema yaishe, no way. Hata nchi zilizoendelea bado corruption ipo.
Kuna mbugila itakuja kusema hii ni awamu ya 6.
 
Mkuu ni Ngarasero Ngusero ipo mjini. Dik Dik juu huko ukirudi utapasahau pamejengeka sana. Ndio shamba la maeda njia ya kwenda Dik Dik.

Sasa hivi kahamishia warehouse yake na shughuli zake kutoka usa kwenda maji ya chai. Mjanja sana kwasababu sasa hivi maji ya ujenzi ni mwingi.
Kumbe Mgerasi unapajua chuga vizuri. Hayo maeneo nimetamba sana enzi nasoma sekondari maana tulikuwa tunatoroka kwenda club moja ilikuwa inaitwa nadhani lefaa kama sijakosea ilikuwa Leganga.
 
Katika wizara zote wizara ya mambo ya ndani na genge lake la polisi wanahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa aisee
Polisi wengi ni mijizi mikubwa,walafi,njaa njaa,na wapenda rushwa wakubwa Nina ushahidi juu ya Hilo kabisaaaa hii mijitu inawalinda wahalifu na kuwapa case innocent people!
 
Kwa wasiomjua huyu prof. Lile ghorofa pale Leganga ambako TRA wamepanga,NSSF etc ndio la huyo dingi.

Na lile jengo ambako Meru Community bank walikua wamepanga ni la mdogo wake huyo Prof.(ambako ndipo alipoenda kuomba hio mil 30 iliyopelea kwny ile rushwa ya mil 100).
...Nimvekwazika kidogo hapo Mkuu. Kama huyu Profesa naye alikuwa ni Msafi na hana Mazonge zonge yoyote, kwa nini alitaka kuwapa hao makalamba hela yote hiyo wakati moyomi ansjua yupo safi na hana kosa lolote?
Inafikirisha. [emoji848][emoji848]
 
...Nimvekwazika kidogo hapo Mkuu. Kama huyu Profesa naye alikuwa ni Msafi na hana Mazonge zonge yoyote, kwa nini alitaka kuwapa hao makalamba hela yote hiyo wakati moyomi ansjua yupo safi na hana kosa lolote?
Inafikirisha. [emoji848][emoji848]
nchi hii ni zaidi ya uijuavyo mkuu.

hapa tuko na polisi kwa ujinga wao,ila mzee tumemsahau kabisa.
 
Nimefuatilia kwa karibu sana tukio la unyanyasaji na ujambazi aliofanyiwa na polis wa kituo cha polis Usa River kule Arusha, Prof Maeda la million 100, nikagundua, kuwa pamoja na polisi 7 kufukuzwa kazi hado hadi leo OCD na OC CID,na mkuu wa kituo cha polisi Usa River, wapi kazini na wanaendelea kuchapa kazi kama kawaida na IGP amepiga kimya kama kawaida yake. Ninashauri nilio wataja waunganishwe na hao askari 7 na kufikishwa mahakamani haraka na mapema iwezekanavyo.
 
Back
Top Bottom