Arusha: Atobolewa Jicho na kung'olewa meno mawili kisa wivu wa mapenzi

Matukio ya kushamiri kwa wivu wa mapenzi mkoani Arusha yaanza kutikisa tena mara baada ya Mwanamke Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Jackline Mnkonyi{38} mkazi wa Sombetini Jijini Arusha mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku alipata kipigo kikali kutoka kwa mume wake ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno mawili na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

IMG-20230526-WA0016.jpg

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema kuwa baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambuwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini bila ya kujitambua.View attachment 2635779

Alisema Mume wake mara baada ya kufika eneo la nyumbani aliwapigia simu wazazi wake na wazazi wake walipofungua geti walimkuta katika hali mbaya na baadae waliamua kumchukua na asubuhiu alipelekwa hospital ya kaloleni kwa matibabu zaidi.

Akizungumza Mkasa huo alisema kuwa,mchana wa mei 23 mwaka huu alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Simiyu aliyetambuliwa kwa jina la Vicent Matai .

IMG-20230526-WA0017-768x1024.jpg

Jackline alisema na kumtaja mume wake kwa jina la ,Isaack Mnyagi Mwalimu na mkazi wa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro huja baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na zaidi kuona watoto wawili aliozaa nao na siku hiyo alikuja usiku ghafla.
Alisema alipofika nyumbani Sombetini maajira ya saa 4.45 usiku aligonga mlango na kufunguliwa na watoto lakini hakutaka salamu na kuingia chumbani na alipomfuata alitoka chumbani.

Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na alimjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana na kusema kuwa ni mtu wake na huwa wanafanya umalaya hatua ambayo alipinga lakini alijikutaja akipigwa na ‘’mjeledi’’ mgongoni.

FB_IMG_1685098776337.jpg

Picha ya Mume wa Jacline aliye mshambulia Mke wake kwa silaa za jadi .

Alisema alijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana na Mume wake Mnyagi alichukua Plaizi kifaa cha gereji na kumwamuru afungue mdomo na kung’olewa jino moja baada ya lingine huku akipata kipigo kikali na kujikuta na maumivu makali hadi jana.

Jackline alisema hatua hiyo aliona kama haitoshi aliamua kuchukua kitu chenye Icha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona na kumwambia maneno mazito na mtusi huku akiendelea kupigwa hali iliyomfanya kupoteza fahamu.

Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kutupwa getini kwani nilishtuka nikiwa hospital .

‘’Nimetobolewa jicho na nimeng’olewa meno mawili kwa chombo kinachoitwa Plaiz nina maamuvi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wake kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu’’alisema Jackline

Naye Mzazi wa Jackline,Mzee Elimilis John Mkonyi alisema kuwa baada ya kumpeleka katika hospital ya Rufaa ya Mount Meru na kupata matibabu alikwenda kituo kikuu cha polisi Arusha na kufungua jalada shambuli la kuzulu mwili kesi namba ARS/RB/5416/2023.

IMG-20230526-WA0002.jpg

Muonekano wa Jackline akiwa mzima kabla ya kupata kipigo kutoka kwa mume wake
Aisee huyu jamaa namfahamu, tena ni member humu jf
 
Itoshe kusema siwezi toa maoni kwa njia unayoitaka na wala muda wa kushindana nawe sina.. Kikubwa tujikite kwenye mada itapendeza zaidi.
Usingeni quote from the beginning,
Ukiwa na huzuni sana kaiombe mahakama msaidiane kifungo na huyo ticha mshenzi,

Kwanza nimewaza wanafunzi walikua wanaishi nae vipi sio alikua anawapiga sana huyu [emoji848]
 
Nawaza tuu kwa sauti....
Kwani hii ni mara yake ya kwanza kupigwa kiasi hiko??? Maana kwa kupigwa huku huyu mwanaume lazima ni mpigaji tuuu...mmh Mungu ampoje huyu bidada lakini ndo tayari ashapata ulemavu ....
Huyo hajampiga, kambomoa
 
Sijapendezwa na reaction ya mwanamme juu ya mke wake,njia nzuri ni kuachna ili watoto waendelee kuwa na baba na mama wenye siha njema.Niko katika ndoa kwa zaidi ya miaka kumi,sijawahi waza kumpiga mke wangu,naomba sana mungu azidi kunisimamia nisijefanya upuuzi kama wa huyu jamaa.

Nadhani njia nzuri kwa wanandoa ukiona mkeo anachepuka kama huwezi vumilia peaneni taraka ili watoto waendelee kupata malezi ya baba na mama,huyu jamaa aliyepiga mke anaenda kupoteza muda wake jera kwa upuuzi kabisa.

Mimi huwachukulia hawa watu wanaowajeruji hadi kuwaachia ulemavu wenza wao na hata wale wanaowauwa wenza wao kwa sababu za wivu wakimapenzi ni watu wabinafsi , wasiojari masrahi ya watu wengine,hebu chukulia una watoto,ndugu zako pia wanakutegemea sasa unakuja haribu future ya watoto wako kwa sababu ya mtu mlo kutana mkiwa watu wazima,unaleta huzuni kwa ndugu zako kwa jambo la kipuuzi kabisa, mwanamke mzinzi ni wakuachana naye nasio kumjeruhi au kumuua.ticha kila mwaka anamwaga wanawake wengi uraiani,si angefukuza Huyo mke akaoa mtoto mbichi tu

Waaume wenzangu tujifunze kuhandle hasra na busara zitawale sana
 
Matukio ya kushamiri kwa wivu wa mapenzi mkoani Arusha yaanza kutikisa tena mara baada ya Mwanamke Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Jackline Mnkonyi{38} mkazi wa Sombetini Jijini Arusha mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku alipata kipigo kikali kutoka kwa mume wake ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno mawili na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

IMG-20230526-WA0016.jpg

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema kuwa baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambuwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini bila ya kujitambua.View attachment 2635779

Alisema Mume wake mara baada ya kufika eneo la nyumbani aliwapigia simu wazazi wake na wazazi wake walipofungua geti walimkuta katika hali mbaya na baadae waliamua kumchukua na asubuhiu alipelekwa hospital ya kaloleni kwa matibabu zaidi.

Akizungumza Mkasa huo alisema kuwa,mchana wa mei 23 mwaka huu alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Simiyu aliyetambuliwa kwa jina la Vicent Matai .

IMG-20230526-WA0017-768x1024.jpg

Jackline alisema na kumtaja mume wake kwa jina la ,Isaack Mnyagi Mwalimu na mkazi wa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro huja baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na zaidi kuona watoto wawili aliozaa nao na siku hiyo alikuja usiku ghafla.
Alisema alipofika nyumbani Sombetini maajira ya saa 4.45 usiku aligonga mlango na kufunguliwa na watoto lakini hakutaka salamu na kuingia chumbani na alipomfuata alitoka chumbani.

Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na alimjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana na kusema kuwa ni mtu wake na huwa wanafanya umalaya hatua ambayo alipinga lakini alijikutaja akipigwa na ‘’mjeledi’’ mgongoni.

FB_IMG_1685098776337.jpg

Picha ya Mume wa Jacline aliye mshambulia Mke wake kwa silaa za jadi .

Alisema alijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana na Mume wake Mnyagi alichukua Plaizi kifaa cha gereji na kumwamuru afungue mdomo na kung’olewa jino moja baada ya lingine huku akipata kipigo kikali na kujikuta na maumivu makali hadi jana.

Jackline alisema hatua hiyo aliona kama haitoshi aliamua kuchukua kitu chenye Icha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona na kumwambia maneno mazito na mtusi huku akiendelea kupigwa hali iliyomfanya kupoteza fahamu.

Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kutupwa getini kwani nilishtuka nikiwa hospital .

‘’Nimetobolewa jicho na nimeng’olewa meno mawili kwa chombo kinachoitwa Plaiz nina maamuvi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wake kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu’’alisema Jackline

Naye Mzazi wa Jackline,Mzee Elimilis John Mkonyi alisema kuwa baada ya kumpeleka katika hospital ya Rufaa ya Mount Meru na kupata matibabu alikwenda kituo kikuu cha polisi Arusha na kufungua jalada shambuli la kuzulu mwili kesi namba ARS/RB/5416/2023.

IMG-20230526-WA0002.jpg

Muonekano wa Jackline akiwa mzima kabla ya kupata kipigo kutoka kwa mume wake
Mjomba konyo
 
Usingeni quote from the beginning,
Ukiwa na huzuni sana kaiombe mahakama msaidiane kifungo na huyo ticha mshenzi,

Kwanza nimewaza wanafunzi walikua wanaishi nae vipi sio alikua anawapiga sana huyu [emoji848]
weka ushahididi.
 
Back
Top Bottom