Mmmmmmhmn watu tunakuwaga na mikwara hapa ila kuna wanaume wenzetu wapo kivitendo zaidi. Mmmmmm hadi nimeogopa aisee.
Huyu mwamba ni katili balaa. Halafu hii inaonekana si mara ya kwanza kwa huyu dada kupewa kipigo. Maana wana watoto wawili hao so it means wameshakuwa pamoja muda mrefu.
Halafu nihoji, mwanaume anaishi vipi Rombo mkewe akabakia Arusha?! Hapa si ni kumpa majaribu huyo dada wa watu?!
Anyways, turudi kwenye mada, hiki sio kipigo cha kumpa mwanamke wako especially mama watoto. Najua hawa viumbe muda mwingine huwa wanatia hasira kupita kiwango hadi unaishiwa maneno unatamani hata ulie ili akuelewe.
But ni vema kuwa na subira na kuwaepuka zile nyakati wanapokengeuka na kutufanya tujiskie kupata kichaa. Dawa ya mwanamke. Mkorofi ni kumtafutia mwanamke mwenzake ambaye atafanya kile unachotaka yeye akufanyie halafu akakataa kwa jeuri tu za kike mradi kisiwe Haram.
Jamaa amepitiliza sana kwenye hili, dada yake au mdogo wake wa kike angepigwa hivi yeye angejisikia namna ipi?
Tuheshimu Ndoa zetu, tuepuke sababu za kijinga zinazoweza wafanya wenza wetu kurukwa akili na kufanya matukio ya kikatili.
Sent from my JKM-LX1 using
JamiiForums mobile app