Arusha hivi "vifodi" ni kuchafua jiji achaneni navyo

Geneva of Africa mnatumia vifodi??
Mnalidhalilisha taifa nyie.
 
Acheni ushamba, toeni hivyo vipanya barabarani muweke magari.
 
Coaster zikiwepo ndio usafiri utakuwa bora zaidi sasa kwa sababu magari yatakuwa machache yanayopakia watu wengi. Ruti zinaweza kurefushwa. Ondoeni hivyo vipanya barabarani.
 
Sehemu ambazo barabara ni nzuri vipanya viondolewe coaster ziweke.
Halafu kwa nini jiji linakuwa na barabara mbovu kiasi hicho cha kuchagua magari??
Si ni bora irudushwe kuwa manispaa.
Hali ya barabara kwa baadhi ya maeneo sio nzuri. Let's be honest. Let's say route ya stendi kuu to ilboru via mianzini like juu ni kubovu Hadi ilkiding'a ulisema unapeleka gari laini ujue imekula kwako
 
Serikali pia inweza kuongeza ushuru mkubwa kwa hiace na kuweka ushuru mdogo kwa coaster kuvitumua hivyo vipanya.
 
Bora lishushwe tu iwe manispaa
Mimi wakati naishi huko nilikuwa naonaga ni poa tu ila nilivyotoka nakenda Mbeya na Mwanza nikagundua Arusha ni jiji ambalo linatabia za kimanispaa ni kama hawakuwa tayari kuwa jiji. Kwa kweli Mwanza ni jiji bora sana.
 
Coaster zitakuwa chache na kupunguza magari barabarani pia jambo ambalo litaboresha usafiri pia. Ruti zinawezwa kurefushwa kwa kuunganishwa.
 
Yani dar pekee yake ndio wanatumia coaster
 
Pigeni Coster Mayai zisanye abiria. Arusha hamstahili vigari vya Malawi, Malawi ndo muwaachie hivyo vigari vya watoto wa vidudu...Malawi wanatumia vi-Nissan Vanette na ninyi chuga mnawaiga hawa.
Haha mkuu inaonekana ubwezini Malawi unakujua vizuri
 
Kila mmoja aweke kosta moja moja vifodi vyenyewe vitapungua
 
Route ndefu coaster itoke ngaramton,sakina,mianzin,mount meru,sanawari,mnazareti, tengeru mpka kikatiti....
Monduli-njiro
ile barabara ya East Africa nayo sijui Isha Anza kutumika..
Watu wa Arusha Ni wavivu wanataka slop na wanaridhika kwa kitu kdgo wakishapata hela ya Konyagi ndo Basi tena .
Ikifika saa tatu na unakaa USA river aisee hesabu maumivu ...route zote zinaishia kwa mrefu na tengeru tu.
 
Wapigadebe stand ya mabasi Arusha kipindi hiki Cha baridi Kali, jeshi la polisi wasipochukua hatua Kali, kuwalazimisha wapigadebe waoge kuna dalili ya kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza. Trust me.
 
Unafananishaje Dar na Arusha? Dar kwa hili joto hata kituo kwa kituo unapanda basi sio Arusha aisee. Pia Arusha basi zinaisha saa tatu Ila Dar usiku mzima Kuna mishe. Dar haifanani kabisa na chuga hata population yake ni kubwa.

Angalia basi za kimara au mbagala zinavyogombaniwa Ila Arusha hauwezi kuona watu wanapandia madirishani Tena unakuta ni eicher au Dyana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…