Arusha: Mzee Iddi Maganga abomoa nyumba zake mbili(200M) baada ya wanawe kuacha kufanya kazi na kusubiri urithi

Arusha: Mzee Iddi Maganga abomoa nyumba zake mbili(200M) baada ya wanawe kuacha kufanya kazi na kusubiri urithi

Tena huyo kijana ashukuru sana mwingine angemshitaki kwa kosa la attempt to killing intentionally!
 
Mnasemaga story ina pande mbili mbona haraka mnakuwa majaji ilihali hamna uelewa na story ya upande wa pili?
 
Unamfungia Baba yako ndani kwenye chumba cha giza wiki nzima bila chakula ili afe urithi Nyumba!

Watu wanatafuta ili walee wazazi wao, wengine wanataka kuua wazazi wao ili warithi Nyumba ya mzazi wao!

Mzee Idd ametumia maamuzi ya haraka sana, kwanza angefungua kesi ya watoto wake kujaribu kumuua kwa kumfungia ndani wiki nzima bila chakula, halafu angeweka sawa mambo yake ya mirathi, watoto kuanza kugombea mali za mzazi huku akiwa hai ni dalili ya kujikatia tamaa mapema kutafuta vyao.
Dawa ni kuwapiga chini hata urithi wa kandambili wasipate
 
Mzee wangu wa karibu sana. Huo ushauri nlimpa mimi. Ili watoto wake wawe na akili. Na ilitokea sababu mtoto wake mmoja alianza kumtongoza demu wangu akimwahidi kuwa atampa pesa akipata urithi wake. Nikamwambia mzee hawa watoto wako watakuja kukuua sababu ya nyumba ,zichome moto. Akafikiria akasema nmeshauri vizuri akaenda choma moto
 
Kaskazini hakunaga ujinga wa kusubiri urithi
Thubutu. Mbona migogoro ya mirathi huko Kaskazini ndio inaongoza ? Watoto wa Mrema, Wa Mengi na Erato Msuya ? Usijitekenye. Huko ndio vinara wa kumendea urithi. Kawadanganye wanywa mbege wenzio
 
Kuna mjinga mwingine aliwahi kuja hapa Jamii forums naye anadai ana miaka sijui 37 anaomba ushauri kumshitaki babake eti ameuza nyumba na amekataa kugawia fungu lake. Ndo kama huyo mjinga wa Arusha kisa kuna vijifremu anapokea kodi kwa kushirikiana na mdogo wake wa kike kaona njia rahisi nikumfungia mzee ndani bila chakula ili afe warithi mali. Hii laana haitomwacha unamfungia babako ndani mpaka anakula mavi yake, majirani wameona huruma na kumpigia simu binti wa mzee mganga ambaye ni dada wa huyu mpumbavu, binti akaja na mme wake wamevunja mlango na kukuta mzee tayari amepoteza fahamu.

Ndo kumuahisha hosp ambako ameenda kuzinduka akiwa hajui nani kampeleka pale. Japo mzee amechukuwa uamuzi wa hasira lakini hatupaswi kumlaumu kwa sababu hatujui amepitia mangapi, alafu hizi jamii hawa wazee ********** sijui kwa nini zinaamini sana kwenye urithi badala ya kufanya kazi na kujiandalia maisha.
Ukikuta sana watu wanagombania nyumba za urithi mara nyingi utakuta wanyamwezi, wazaramo,wakwere na wale wa ujiji kigoma huko wale walioishi Kariokoo karioakoo miaka mingi.
Ni mara chache sana kukuta sisi wakurya tukigombania urithi wa nyumba.
Hao watoto wa Mrema na wa Mengi wanaogombania mirathi in Wanyamwezi ?
 
Daah haya maisha ya wahuni kusubiri urithi imekomaa sana hata majibu ya vijana humu pakiwa na fursa yeyote unaona kabisa hawa wanasubiri mali ya kugawiwa...
 
Mzee chai sana, nmemskiliza vizuri mwanae, mdogo wake na majirani nmegundua Mzee ni hamnazo.
 
Back
Top Bottom