Arusha: Mzee Iddi Maganga abomoa nyumba zake mbili(200M) baada ya wanawe kuacha kufanya kazi na kusubiri urithi

Arusha: Mzee Iddi Maganga abomoa nyumba zake mbili(200M) baada ya wanawe kuacha kufanya kazi na kusubiri urithi

Hizi habari sio kweli acheni mambo ya vjiweni mtoto wakike ndio amemuokoa baba yake
Aliyemfungia ni wakiume na ugomvi ni wa muda mrefu sana
Diwani anakiri hilo
Huwezi kuuza nyumba kiholela
Lazima kata na mtaa wako wajue
Sasa Inamaana Diwani hajui na mashahidi hawajui?
Watoto walitaka kumuua Mzee wao

Diwani anakiri hata usafi wa chumba chake Mzee kina kaa Mwezi hakijafanyiwa usafi. Mzee amekula mavi yake unajua hilo?
Uliyoandika ni kabla ya binti yake kuja kumchukua baada ya kufungiwa ndani.
Sheria gani inayosema unapotaka kuuza nyumba yako ni lazima diwani ajue?
Wenzio tupo next na eneo la tukio wewe unasubiria watu wa media warushe clip.
 
Mitoto ya late 80s, 90s na early 2000!
Bure kabisa. Hawana tofauti na watoto wa Kino Migo Mwananyamala na Mbezi beach. Yenyewe ni kula kulala. Pombe siku nzima. Kuibia wazazi. Kuzaa hovyo hovyo na madawa ya kulevya.
Hovyo kabisa kabisa [emoji35][emoji3062][emoji2959]
Watake radhi watoto wa kinondoni original siyo wote wanasubiria urithi
Wengine wazee wetu hawakuwa hata na urithi wa kutuachia

Ova
 
Mkazi wa Ngarenaro, Mzee Iddi Maganga amebomoa nyumba zake mbili zenye thamani ya milioni 200 akiwatuhumu watoto wake kumfanyia ndivyo sivyo.

Akiongea kwa uchungu, Mzee Maganga amesema mmoja wa watoto wake anayeitwa Abdallah alimfungia kwenye chumba chenye giza wiki nzima bila chakula mpaka kufikia kula kinyesi chake. Mzee Maganga amesema aliokolewa na mtoto wake wa kike baada ya kutomuona muda mrefu.

Mzee Maganga amebomoa nyumba zake na kuwataka watoto wake wakafanye kazi badala ya kukaa wakimendea urithi.

Hasira...Hasara!
 
Ukitazama umri wa huyo mzee na hayo maamuzi aliyoyachukua haiwezi kuwa ajabu, ajabu ni wewe kushangaa umri huo huwa wanakuwa na akili za namna gani ama labda haujawai kukaa na watu wenye umri huo.
Kama ni kawaida kwa wazee unaowafahamu kuchoma nyumba zao ni sawa tu.
 
Hili ni tatizo kubwa sana kwa Jamii zetu za kitanzania, hivi karibuni nilikutana na mzee mmoja wa MIAKA 54 ananiambia amepambana kwa miaka minne iliyopita akaihamisha familia yake kwenye nyumba yake baada ya kukaa kwao muda mrefu, Sasa hivi amemwacha kaka yake wa MIAKA 60 Bado anakaa kwao na familia yake hiyo yote ni kwa SABABU wananyumba MAKUMBUSHO hivyo wote wanaoa na kuzaliana hapo.

All in all huyo mzee kafanya la maana maana watoto wamegeuka Israel.
 
Sidhani kam .zinafika 200m..maana.mabati yamechoka mno mno...au alimaanisha 20m
Mkuu kaa ukijua thamani hapo sio ya nyumba bali ni ya kiwanja. Na ndio maana baada ya kununua mnunuzi amebomoa hizo nyumba.

So kiuhalisia mnunuzi hakununua hizo nyumba bali amenunua kiwanja. Ngarenaro kama hujui ipo Arusha mjini kati.
 
Hii mitoto ya Manzese na Buguruni yote mijizi tu inaota mchana kuwa itakuwa mitajiri
 
Mzee kachemsha, angeuza akahamia mjini kula bata na Ashura.
Kwa jinsi anavyoelezea huyo mzee inaonesha huenda hata hati za nyumba hiyo walishampokonya. Sasa atauzaje bila hati? kaone isiwe tabu bora liwalo na liwe. Pia kwenye hiyo clip nimemsikia akisema atauza, probably atauza kiwanja baada ya kuzisambaratisha kabisa nyumba zake.
 
Back
Top Bottom