Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo maana askari alienda na mwenzake. Kwanini yeye apige mke hadi mke aombe msaada wa polisi? Tena ameshika na panga, si angeuwa mke na watoto?Askari angefuata ethics za kazi yake. Tukio hilo lilikuwa linamhusu personally kwa kupigiwa simu ya mkononi na marehemu,angetuma askari wengine kukwepa kuwa emotional involved.Inawezekana emotions ziliathiri maamuzi yake.
Na ndo nishasema huo ujinga wa uchepukaji hauna nafasi kwanguMkuu na hali halisi ni kuwa hata kama polisi alikuwa anachepuka na huyo mke wa mtu ataanza kumkwepa sasa baada ya kuwa mjane. Sijui hili jambo huwa lina siri gani lakini mara nyingi mwanamke ''anapendeka'' anapokuwa kwenye ndoa lakini mara akiachika wanaume wanaanza kumpiga chenga.
Ukishakufa hakuna wa kukutetea tena, badala yake kesi itapindishwa na mwisho wa siku marehemu ndie anakuwa mwenye makosa.Polisi wa kituo cha Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wanadaiwa kumpiga risasi raia aliyetambuliwa kwa jina la Yohana Nasieli kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi kati ya mke wa marehemu na askari polisi.
Habari kutoka kwa ndugu na majirani wa marehemu zilisema kuwa tukio hilo limetokea aprill 12 mwaka huu majira ya saa 1.35 usiku katika mtaa wa sabasaba kata ya Monduli Tarafa ya Kisongo wilayani humo.
Vyanzo vilisema kuwa siku ya tukio ya marehemu alikuwana ugomvi na mke wake, Paulina Kiliani{37} na kumlalamikia mke wake kuwa sio mwaminifu katika ndoa akimtuhumu kuwa na mahusiano na askari polisi aliyefanya mauaji {jina linahifadhiwa} kuwa ndio mvunja ndoa yake.
Vyanzo vya habari viliendelea kusema kuwa siku ya mauaji marehemu na mke wake walikuwa na ugomvi mkubwa na kufikia hatua ya kupigana na mke alimpigia simu ya kiganjani askari polisi huyo na kumwelezea kupigwa kwake na mume wake na askari huyo akiwa na mwenza wakiwa na silaha walikwenda eneo la tukio.
Habari zilisema kuwa baada ya marehemu kumwona askari yule yule anayemtuhumu kufanya mapenzi na mke wake akiwa wa kwanza kufika eneo la tukio,marehemu kwa hasira huku akiongea kwa jazba kuwa wewe ndio niliyekuwa nakutafuta ghafla aliingia ndani ya nyumba yake na kuchukua panga kwa nia ya kumtishia askari huyo akiwa na mwenzake ili aondoke eneo la tukio.
Vyanzo vilisema kuwa kabla ya marehemu kufanya tukio la kutaka kumkata Askari huyo,ghafla askari huyo alifyatua risasi na kumpiga marehemu kifuani kushoto na mguuni na kufariki dunia papo hapo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alithibitisha tukio hilo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo imesema kuwa NASIELI alijeruhiwa kwa risasi upande wa kushoto wa mguu na kwenye bega la mkono wa kushoto baada ya kukaidi amri halali ya askari Polisi ya kukamatwa na kutaka kumkata askari panga alilokuwa nalo mkononi mwake.
Kamanda aliendelea kueleza katika taarifa yake kuwa marehemu alikuwa amewafungia watoto wake na mtoto wa jirani yake ndani ya nyumba kwania ya kuwadhuru na baada ya kutoa taarifa askari waliamua kwenda eneo la tukio kwa nia ya kuwaokoa watoto lakini pia kumkamata mtuhumiwa.
Taarifa ilisema baada ya kufika eneo la tukio walianza kugonga mlango uliokuwa umefungwa ili kuokoa watoto waliokuwa hatarini wakati wanaokoa watoto hao nje ya nyumba hiyo walimwona mtuhumiwa huyo akiwa amejificha akiwa ameshika panga Mkononi huku akiwa fuata askari hao kwa lengo la kuwadhuru.
Alisema baada ya hali hiyo ndipo alipoamua kumpiga risasi kwenye bega lake la kushoto hali iliyosababisha kuvuja damu nyingi na kisha kupelekwa katika hospital ya wilaya ya Monduli na mtuhumiwa huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.
Ends...
Huyo polisi alijua ana maslahi na hiyo kesi asingejihusisha nayo.Hapo ukisoma kwa makini. Hiyo kesi wote watatu wana makosa pauline ana makosa, polisi ana makosa na marehemu pia ana makosa. Hata kama ni nyie mngekua ndo huyo polisi ni lazima mngejihami tu. Sasa kama marehemu angemkata kweri hilo panga? Ilikua ni lazima ajihami. Mim ndo maana sitokuja kuoa. Tena habari kama hizi ndo zinanikata moto kabisa.
Kibaya zaidi majirani wataishi na ushahidi milele sasa siku watoto wakikua na kujua ndio kakosa kotee..watoto watamchukia hadi ajute mara kumi! Raha za muda mfupi zinagharimisha maisha yake...jamani dunia hiiLipi ni lipi? Tuamini majirani au kamanda wa mkoa?
Kama shida ni wivu kama walivyosema majirani, mke tayari amekosa mme, amebaki mjane, na huyo askari hatomuoa. Yani amekosa bara na Pwani na hii dhambi itamtafuna maisha yake yote.
[emoji3]KwambaJamani mbona mi nimeachwa na kale kamchepuko kangu nimetulia nashangaa juzi natumiwa sms mambo kucheki namba yake nikamjibu mambolo,
Cha ajabu shapata mchepuko mwingine mkali zaidi yake ila vitoto vya chuo ni kucheza navyo kulingana na mdundo
Kama wana mtoto wa kiume aanze kudili na alomuua baba yake,huwa ni rahisi tu mtu akiamua coz huyo askari anakunywa maji tunayo kunywa,ata chakula pumzi na aridhi ni hii hii chapu tu.Askari yupo sahihi hata kama alikuwa anatembea na huyo Paulina.
Ni bora mwanamke akianza kwenda polis hafai tenaBora kuachana tu ikiwa hamuelewani.
Hapo hawawezi kuendelea ni karma mbelekwambeleHaya sasa amekufa na kuwaacha waendelee na mapenzi