ARUSHA: Polisi hawara aua mume wa ndoa kwa risasi

Askari angefuata ethics za kazi yake. Tukio hilo lilikuwa linamhusu personally kwa kupigiwa simu ya mkononi na marehemu,angetuma askari wengine kukwepa kuwa emotional involved.Inawezekana emotions ziliathiri maamuzi yake.
Ndiyo maana askari alienda na mwenzake. Kwanini yeye apige mke hadi mke aombe msaada wa polisi? Tena ameshika na panga, si angeuwa mke na watoto?
 
Na ndo nishasema huo ujinga wa uchepukaji hauna nafasi kwangu
 
Ukishakufa hakuna wa kukutetea tena, badala yake kesi itapindishwa na mwisho wa siku marehemu ndie anakuwa mwenye makosa.

Its sad
 
POLISI wa Kituo Kikuu cha Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumpiga risasi raia aliyetambuliwa kwa jina la Yohana Nasieli katika mazingira yanayohusishwa na mapenzi. Majirani na ndugu wa marehemu wanadai kuwa, tukio hilo lilitokea Aprili 12 mwaka huu saa 1.35 usiku katika Mtaa wa Sabasaba, Kata ya Monduli Tarafa ya Kisongo wilayani humo.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio, Nasieli alikuwa na ugomvi na mkewe, Paulina Kiliani (37), akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na polisi aliyedaiwa kuua (jina linahifadhiwa).

Kwa mujibu wa vyanzo, siku ya tukio Nasieli aligombana na mkewe hadi wakapigana na ndipo Paulina akampigia simu ya kiganjani polisi huyo kumpa taarifa kuwa amepigwa na mumewe.

Alielezwa kuwa, baada ya kupata taarifa hizo, askari huyo na mwenzake wakiwa na silaha walikwenda eneo la tukio. Inadaiwa kuwa baada ya Nasieli kumwona polisi anayemtuhumu kuwa na uhusiano na mkewe, alizidi kukasirika na kuongea kwa jazba kisha akaingia ndani kuchukua panga kwa lengo la kumdhuru askari polisi huyo.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa kabla ya Nasieli kutimiza lengo lake, askari polisi huyo alimpiga risasi kifuani upande wa kushoto na mguuni na Nasieli akafa papo hapo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema Nasieli alijeruhiwa kwa risasi mguu wa kushoto na kwenye bega la mkono wa kushoto.
Taarifa ya Kamanda Masejo ilieleza kuwa, raia huyo alikaidi amri ya polisi ya kutaka kumkamata na alitaka kumkata askari kwa panga alilokuwa nalo mkononi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Paulina ni mfanyabiashara na anaishi eneo la Sabasaba. Kamanda Masejo alieleza kuwa, awali mama huyo alifika Kituo cha Polisi akamtambulisha Nasieli kuwa ni mpenzi wake na kufungua kesi dhidi ya Nasieli ya kutolewa lugha ya matusi.

Alieleza kuwa, mchana wa siku ya tukio, mlalamikaji alirudi tena katika kituo cha Polisi akidai kuwa mpenzi wake alimpiga na kumsababishia majeraha kwenye kidole na sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Masejo alieleza kuwa, Nasieli pia aliwafungia wanawe na mtoto wa jirani ndani ya nyumba kwa nia ya na kuwadhuru na baada ya Polisi kupata taarifa walikwenda eneo la tukio kwa nia ya kuwaokoa watoto na kumkamata mtuhumiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kufika eneo la tukio waligonga mlango uliokuwa umefungwa na wakati wanaokoa watoto, walimuona Nasieli akiwa amejificha akiwa na panga mkononi na akafuata askari kwa lengo la kuwadhuru.

Alieleza askari hao walimuamuru Nasieli asimame, lakini hakutii na aliendelea kuwafuata akiwa amenyanyua panga. Kwa mujibu wa kamanda huyo, askari hao walirudi nyuma mitaa kadhaa, lakini Nasieli aliendelea kuwafuata na askari walianza kukimbia, wakapotezana na mtuhumiwa akawa anamfukuza askari polisi mmoja.

Alisema askari polisi aliyekuwa akikimbizwa alipiga risasi mbili juu ili mtuhumiwa asimame, lakini alizidi kumfuata hivyo akampiga risasi mguu wa kushoto, lakini Nasieli alizidi kumsogelea askari ambaye kwa wakati huo alikuwa ameanguka.

Kiongozi huyo wa polisi alisema Nasieli alimfikia askari polisi na alitaka kumnyang’anya silaha aina ya SMG. Kamanda Masejo alieleza kuwa katika purukushani hiyo, polisi alimpiga risasi Nasieli kwenye bega la kushoto akavuja damu nyingi.

Kwa mujibu wa Polisi, Nasieli aliaga dunia wakati akipata tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.

Chanzo: HabariLeo
 
Huyo polisi alijua ana maslahi na hiyo kesi asingejihusisha nayo.
 
Hii habari ngoja nitulie nisome taratibu. Na huku naombea aende jela uyu akaozee huko.
 
Askari ashatolewa kwenye msala hapo, dah!
 
Lipi ni lipi? Tuamini majirani au kamanda wa mkoa?
Kama shida ni wivu kama walivyosema majirani, mke tayari amekosa mme, amebaki mjane, na huyo askari hatomuoa. Yani amekosa bara na Pwani na hii dhambi itamtafuna maisha yake yote.
Kibaya zaidi majirani wataishi na ushahidi milele sasa siku watoto wakikua na kujua ndio kakosa kotee..watoto watamchukia hadi ajute mara kumi! Raha za muda mfupi zinagharimisha maisha yake...jamani dunia hii
 
Kwa kawaida RPCs huwa wanasoma taarifa wanazopelekewa na hao askari wa chini kuanzia OCDs OC CIDs na wanaokuwa doria na operations mbalimbali za kipolisi, hili ni tatizo kubwa sana kwa sababu eneo la polisi wahalifu ni hili la ngazi ya chini na ambalo lina ufundi wa kusema uongo wa kiwango cha juu sana.

Kama mfumo wa utoaji taarifa hautabadilishwa na kutegemea huu uliopo uhalifu ndani ya polisi fosi hauwezi kuisha kamwe.
 
Askari kwenye matukio ya kihalifu mara nyingi huchelewa kufika,huo ugomvi wa ndoa amefika haraka.
Kulikoni!!!
 
Jamani mbona mi nimeachwa na kale kamchepuko kangu nimetulia nashangaa juzi natumiwa sms mambo kucheki namba yake nikamjibu mambolo,

Cha ajabu shapata mchepuko mwingine mkali zaidi yake ila vitoto vya chuo ni kucheza navyo kulingana na mdundo
[emoji3]Kwamba

Yeye:Mambo
Wewe:Mambolo
 
Huyo mwanamke amethamini ukahaba kuliko utu. Aendelee na ukahaba
 
Askari yupo sahihi hata kama alikuwa anatembea na huyo Paulina.
Kama wana mtoto wa kiume aanze kudili na alomuua baba yake,huwa ni rahisi tu mtu akiamua coz huyo askari anakunywa maji tunayo kunywa,ata chakula pumzi na aridhi ni hii hii chapu tu.
 
Haya sasa amekufa na kuwaacha waendelee na mapenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…