Arusha: Wanne wadaiwa kufariki dunia baada ya Noah kusombwa na maji ikijaribu kuvuka barabara iliyofunikwa na maji

Arusha: Wanne wadaiwa kufariki dunia baada ya Noah kusombwa na maji ikijaribu kuvuka barabara iliyofunikwa na maji

Wanasema ni watatu mpk sasa mtoto mmoja bado anatafutwa
 
Kuna watu akili zao sijui vipi?
We una familia nzima ndani ya gari unalidumbukiza kwenye maji kasi unaiona,
Si hata angewashusha au kusubiri mkondo wa maji upungue?
Sasa familia nzima ishakufa watu sita.
ndugu km kawaida wataanza kugombea Mali tu.
Mlikua mnawai wapi?
Si mngesubiri, au nenda wewe jemedari na gari yako
Utumbukie humo,
unabwaga familia nzima ndani ya maji.
Inasikitisha sana
Habari iko TBC Jioni hii
Wanakuaga na ujuaji na ubishi wa kijinga wa kulazimisha mambo
 
Dereva kapona
ukiangalia vizuri kilichotokea unaweza usimlaumu yule jamaa aka marehemu.

Ile gari Noah ilikuwa kwenye foleni ya magari mengine na yote yaliyokuwa mbele madogo tu kama lake yaliweza kupita ikiwepo RAV4, nafikiri hili lilimpa ujasiri wa cross kwa kupima na macho na kuona anaweza kupita.

Mamlaka kuanzia RTO, Tanroads, RPC nk wanahusika na hivi vifo kwa kutokuwa na road patrol hasa kwenye highways wakati tu inapoanza mvua kubwa, lengo ni kuchunguza hali ya barabara kitalaam na haraka kuweka vizuizi kuzuia matumizi ya barabara na hata kutoa tahadhari wakati wote.

Mwenyezi Mungu wamesamehe dhambi zao marehemu na kuwaondolea adhabu kabri ndugu zetu wale.
 
Tuliwai kukutwa na same scenario kipindi cha el- ninyo.
Safarini Shinyanga.
Dom bahi daraja limevunjika mto maji km yale tukaona huko hatutoboi,ikabidi kukunja kwamtoro,
Dereva mbishi anawai kupeleka zawadi za sikukuu kwa wanae.
Tukakunja huko
Ilikua 110 londo, tumesota sana njiani mpk tukafika hapo kati kwa wasandawe.
Hapo tukakuta daraja nalo limesombwa ikabidi tutafanyaje.
Jamaa kadai tukae ndani gari iwe nzito tutapita.
Nikamwambia tujaze mawe iwe nzito upite nayo mi sikai humo ndani wala ndugu yangu.
Akagima.
Bahati nzuri wakatokea wanajeshi toka Singida na roli lao.
Walivyokuta pale hapapitiki.
Wakaingia shamba jaza miti pale mtoni mpk pakajaa wakasema nyie piteni kwanza si tutapita tu baada yenu.
Sijui ilikua mtego😁,
Tukapita fresh na wao wakavuka wakapunga mkono haoo.
Tumefika mbele kidogo gari ikateleza ndani ya maji tena.
Hapo katikati ya pori ni milio ya simba na chui tu.
Ikabidi kujifungia tulale humo ndani.
Kesho kukakucha wakaja hao wasandawi(hadzabe)
Sukuma gari wapi wanadai hela tunawapa sukuma tena wapi wanadai hela iongezwa tunawapa.
Mpk usiku hola.
Hapo njaa balaa.
Katokea mwl mmoja ndio kasema twende home nikatengeneze ugali japo mle.
Tukaongozana toka pale porini mpk kwake.
Buku 5 kachinja jogoo na dona la kutosha.
Tulikua tumeenda na muhaya mmoja bonge kufika kule kashiba kagoma kurudi pale tumekwama🤣🤣🤣🤣.
Ikabidi nigeuze mwenyewe maana nikifkiria wenzangu hawajala siku 2 na hasa bwa mdogo.
Aisee ningeliwa na wanyama siku hiyo.
Nilikutana nao wawili wakaniangalia tu.
Nikapita mwenyewe nikafika salama na ugali kuku.
Wale wengine wakafurahi sana kupata chochote.
Tulikua sita pia.
Kesho wasandawi wakaja rundo tukakomaa gari ikatoka.
Tukampitia yule mpuuzi pale kwa mwalimu amelala, tukaendelea na safari.
Tulifika salama.
 
Kilichompa Ujasiri dereva wa Noah ni kuona magari mengine madogo ya Aina yake yakipita bila shida,na yeye akaunga trela.ila kifo bana kinakuja kwa kushangaza sana
Magari yenye 4wheel Yana uhafadhali kwenye Mazingira kama Yale, uzito WA engine unasaidia kuvuta Gari
 
Nimeona clip ya tukio aisee yalikuwa yanapita magari mengi ila NOA ikazidiwa nguvu ikabebwa. Ila ni hatari kuendesha gari kwenye maji yanayotembea
Noah ni nyepesi
 
Kilichompa Ujasiri dereva wa Noah ni kuona magari mengine madogo ya Aina yake yakipita bila shida,na yeye akaunga trela.ila kifo bana kinakuja kwa kushangaza sana
Kwa gari zenye 4WD zinakuwa na nguvu zaidi kuvuka kwenye mazingira kama hayo......ndo maana inawezekana Noah imefeli kwa kutokuwa na 4WD, anyway lesson learnt......R.I.P kwa waliofikwa na umauti.
 
Kuna watu akili zao sijui vipi?
We una familia nzima ndani ya gari unalidumbukiza kwenye maji kasi unaiona,
Si hata angewashusha au kusubiri mkondo wa maji upungue?
Sasa familia nzima ishakufa watu sita.
ndugu km kawaida wataanza kugombea Mali tu.
Mlikua mnawai wapi?
Si mngesubiri, au nenda wewe jemedari na gari yako
Utumbukie humo,
unabwaga familia nzima ndani ya maji.
Inasikitisha sana
Habari iko TBC Jioni hii
Na si kesi ya mwanzo...mara kadhaa ishatokea ila watu hawajifunzi

R. I. P, ndio khatma, kila nafsi inayoishi itakufa pia
 
Sasa huyu nae ki gari cha kilo 1500 ana kupitisha kwenye maji yanayo enda kwa speed ..afu kwenye iyo video ina onesha Ali enda kwenye kingo kabsa
 
Nimeona niingilie kutoa mawazo yangu.
Tusiwalaumu hawa waliokumbwa na mkasa huu kuwa ni wazembe kwa sababu zifuatazo
1.Noa ni gari ambalo uzito wake sio mkubwa
2.Noa sehemu kubwa ni uwazi kama vile boti lilivo au tuseme ngalawa
3.Huenda upepo kwenye matairi ulikuwa umejaa ipasavyo
4.Kama matairi aliweka hewa ya Nitrogen
5.Yeye alikuwa anaangalia magari yaliyokuwa yamemtangulia yamepita kwanini yeye asipite?
UDADAVUZI
1.Uzito wa gari ukiwa mdogo halina uwezo wa kujikita chini vizuri
2.Kitu chochote kikiwa na uwazi ni rahisi kuelea na ndio maana shillingi inazama meli haizami hii ni fizikia sasa
3.Upepo unavyokuwa mwingi ndio uwezo wa ku elea unaongezeka kumbukeni hata meli inapotengenezwa nchi kavu wanapotaka kuungiza majini wanajaza upepo matube makubwa kama ya gari kuifanya ielee
4.Specific gravity ya Nitrogen ni ndogo kuliko ya air
5.Kila gari lina uzito wake mfano magari ya 4Wheel yana himili hii hali na pia malori hasa yenye mizigo au mabasi sasa yenye alikuwa anashindanisha kipanya chake na wenzake.

Watu wanalaumu ajali ya Handeni hawa walipita daraja likakatika

By the way rest in peace
Usilaumu kuwa ni wazembe sio kila mtu anajua fizikia
 
Back
Top Bottom