Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Uko vizuri katika kufuatilia news kuhusu TZ. Bila shaka unaielewa nchi hiyo kwa undani wake. Itabidi RAO akutafutie walau nafasi ya ajira katika ubalozi wa Kenya nchini TZ hapo atakapoapishwa kuwa rais.

Shukrani, ila mimi ni kawaida yangu kufuatilia haya mataifa ya Afrika, njoo kule Nairaland.com uone ninavyofuatilia Nigeria.
Sema kwa Tanzania huwa nafuatilia zaidi kidogo maana nilipaishi kwa miaka kadhaa.
 
Mkuu field marshall1 , naunga mkono hoja, Rais Samia ni muwazi na baraka sana kwa taifa Letu.

Kiukweli amejitahidi sana kuwa muwazi kwenye mengi lakini ili uwazi ulete manufaa, uwazi huo ni lazima uwe the truth na ufuatiwe na uwajibikaji, yaani truthfulness and transparency must be followed by accountability. Truthfulness ni ukweli kamili yaani full truth.

Mfano kwenye utengenezaji wa filamu ya Royal Tour, kuna transparency ya kiasi cha pesa kilichotumika. Tumeambiwa kimechangwa na matajiri fulani!. Michango yoyote ya kumchangia Mkuu wa nchi must be see through transparency. Sikumbuki kuwahi kuona fund raising letter or event ya kumchangia rais wetu kutengeneza filamu, this means two things,
1. Barua za kuomba michango zilifanywa siri, zikapelekwa kwenye funding institutions kimya kimya, fedha zinatolewa. Kwa vile huyu ni Rais wetu, sisi Watanzania we have the right to information ni kina nani wamemchangia rais wetu, kila aliyechanga ni nani na amechangia kiasi gani?.
2. Inawezekana hakukutwa na fundraising ya aina yoyote, bali Rais wetu ndio amekuwa sponsored kugharimiwa, we as Tanzanian public, we have the right to disclosure ni matajiri gani wamem sponsor Rais wetu na kwa kiasi gani, ili tuondoe mashaka ya uwepo wa any conflict of interest kati ya ma sponsor na biashara zao. Ikitokea ni wafanyabiashara, then lazima kuwepo maximum transparency ni kina nani, wametumia kiasi gani ili tujiridhishe ni Charity money na sio enticed donations itakayo kuja kuwa paid back Kwa kickbacks kwenye tenders kubwa kubwa, this being the case, inamaanisha kuna uwezekano wa rais wetu amehongwa sponsorship ya kutengenezewa movie?.

Na baada ya full disclosure ya sources of the monies, then accountability ya matumizi ya kila senti, ikiwemo artists fee za starring wa hiyo movie.

Tuhuma kama hii ya rais wetu kuhongwa iliwahi kutolewa kule nyuma, na ubalozi wa Marekani kumtuhumu rais wetu fulani kuhongwa suti!. Ni sisi sisi JF tulisimama na rais wetu tukawataka Marekani watuombe radhi Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi! hivyo kwenye Royal Tour, baada ya shamra shamra za uzinduzi huku na kule, tukitulia, tuta demand full disclosure na sio hizi half truths kwasababu Ikulu yetu ni mahala patakatifu, hakuna biashara ya aina yoyote mahala pale patakatifu petu!. Hata rais wetu fulani alipofanya biashara akiwa Ikulu yetu, sisi wa kupinga biashara Ikulu, tulipinga Je, wajua kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa? Kinga ya kutoshitakiwa haihusu Rais kufanya biashara Ikulu hili Mwalimu aliliongea vizuri kabisa na mimi nilikuwepo hapo siku hiyo.
P
 
Wewe ushazeeka teuzi zinataka vijana mzee jiandae mwezi ujao sabasaba we kila kiongozi unamlamba miguu [emoji16]
 
Toka amwache huru muhalifu no1 tanzania ...yule singasinga basi wote mnaompongeza huyo mama ni WAHUNI TU ...NA WAHUNI NDIYO WOTE WASIOKUWA WAZALENDO AU WENYEKUCHUKIA UZALENDO
 
Mimi Mkenya hapa, napenda sana kusoma makala yako, huwa very deep, insightful and thought provoking, sema ndugu zako wazembe wa kusoma, comments zao zinaonyesha hawasomi kitu na kuelewa, wanajibu tu moja kwa moja.
Wala haujakosea jirani.
 
Toka amwache huru muhalifu no1 tanzania ...yule singasinga basi wote mnaompongeza huyo mama ni WAHUNI TU ...NA WAHUNI NDIYO WOTE WASIOKUWA WAZALENDO AU WENYEKUCHUKIA UZALENDO
Mkuu Lwiva , Tanzania tunafuata mfumo wa haki wa Jumuiya ya Madola, laws of commons, kila mtuhumiwa anahesabika innocent until proven guilty by the court of competent jurisdiction. Hivyo huyo unayemuita mhalifu number 1, sio mhalifu kabisa maana hakuhukumiwa na mahakama yoyote.

Mimi ni miongoni mwa waandishi waliojitokeza kuwatetea hawa kupitia makala hizi Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

na hii Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...
P
 
Mayalla wakati wa kichaa yule uliufyata na kugeuka msifiaji wa ujinga. Ogopa kitu njaa
 
Pascal Mayalla
Wakati wa Mwendazake ulimsifu kwa makala lukuki
Sasa umehamia kumsifu rais Samia kwa style yake nzuri ya utawala, tatizo ni kwamba hawa wawili huwezi kusema wanna mfumo uliofanana wa utawala
Unabadilika badilika.
 
Labda tujue kwanza, ubatili uliingizwa na "mfumo" au "mwenyekiti". Kama ni wa mfumo, hapo hata mwenyekiti hakuna anachoweza kufanya. Mwenyekiti anaweza kuwa na nia njema kabisa, lakini kama mfumo hautaki; hakuna mabadiliko. Bado naamini Kikwete alikuwa na nia ya kuleta katiba mpya, lakini kilichomwangusha ni mfumo "kumgomea". Maana Mkapa siamini kama alikuwa mjinga na mbinafsi kiasi cha kukubali yale mabadiliko; nini kilichomsukuma? Na sasa hivi hakipo?
 
Mkuu MtamaMchungu ,ubatili wenyewe imechomekewa systematic and not individually
Ubatili wenyewe ni huu
KATIBA YETU INA UBATILI, SHERIA YA UCHAGUZI INA UBATILI!. na SHURTI HILI KWENYE KATIBA YETU NI BATILI!

Mama ni mpenda haki mtenda haki, akiujua ubatili huu jinsi ulivyo chomekewa, tunakwenda kuumuonyesha

P
 
Mayalla wakati wa yule uliufyata na kugeuka msifiaji wa ujinga. Ogopa kitu njaa
Mkuu Gulwa , kwanza ni mimi ile 2014, ndiye niliye eleza humu kuwa 2015 ni JPM na kuzieleza sababu zikiwemo strengths na weakness zake Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Pia nilishauri yule mgombea wangu Elections 2015 - Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!

Na baada ya uchaguzi, mbona nilisema kila kitu Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Wewe ulikuwa unakutana na mabandiko ya kumsifu tuu, yale ya critics ulikuwa hoyaoni?
P
 
Pascal Mayalla
Wakati wa Mwendazake ulimsifu kwa makala lukuki
Mkuu Babu Ochu, kwanza ni kweli nilisifu kwa makala lukuki, jee zilikuwa ni sifa za uongo?. Magufuli alikuwa jembe au sii jembe?. Makala zote za kusifu, alistahili, jee makala zangu lukuki za criticism of JPM ulikuwa unaiona?.
Sasa umehamia kumsifu rais Samia kwa style yake nzuri ya utawala
Kama ulivyo eleza kuhusu style nzuri ya utawala wa Samia, jee anastahili kusifiwa?. Na kwa Samia, jee umeona makala za sifa tuu?, za criticism jee hujaziona?.
tatizo ni kwamba hawa wawili huwezi kusema wanna mfumo uliofanana wa utawala
Unabadilika badilika.
Kuna mtu yoyote amewahi kusema Sa💯 na JPM wanafanana mifumo?.
JPM utawala wake ulikuwa Top-buttom style huku akijenga watu, powerful people. Sa💯 yeye ni Bottom-Up, style huku akijenga mifumo, systems Pascal Mayalla: Tanzania sasa inajenga Mifumo na sio kujenga watu kama enzi za Hayati Magufuli
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…