Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa

Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa

Sijawahi kuyumba popote!, besides being a journalist, I was mjeda, hivyo huko nnavyo dhani nimeyumba ni just survivor mechanism
P
Hapa ndiyo watu wanakugeuzia kibao mkuu na kukuita Paschal Njaa, angalia mtu kama Aloyce Nyanda anapata misukosuko sn na kipindi chake cha The Big Agenda lakini jamaa kasimama imara bila uoga
 
Hapana mkuu ukifanya vizuri tutakusifia na ukiharibu tutakupa ukweli
Asante ila sifanyi kitu ili kusifiwa wala sina tatizo na critics ila tunapaswa kuheshimiana, mtu akisema halipendi jina fulani alililopachikwa basi msilitumie
P
 
Hapa ndiyo watu wanakugeuzia kibao mkuu na kukuita Paschal Njaa, angalia mtu kama Aloyce Nyanda anapata misukosuko sn na kipindi chake cha The Big Agenda lakini jamaa kasimama imara bila uoga
There are so many ways of survival mechanisms, the bottom line is survival and I'm a survivor.
P
 
Asante ya nini wakati KATIBA yako inaruhusu mikusanyiko ya kisiasa na maandamano. Yaani mtu anakupora haki yako afu anakurudishia baada ya muda then unampigia magoti kumwanbia asante? 🙄😳
 
Wanasisiem ni waoga sana hawana ujasiri wa kutetea rasilimali za nchi hii ndio maana wanatumia nguvu nyingi kuwa dhibiti CDM
 
Wanabodi,
.
Kwenye hili la kuzuiwa mikutano ya hadhara, kwa vyàma vya siasa kwa vile mikutano hiyo ya vyama vya siasa ni jambo ambalo limeruhusiwa na katiba, hivyo vyama vya siasa kufanya mikutano ni miongoni mwa haki za vyama vya siasa zilizoainishwa na katiba, hata lile swali langu la Ikulu, kumuuliza rais wa JMT, ametumia mamlaka gani kwenye kifungu kipi cha sheria, kuzuia jàmbo lililoruhusiwa na katiba?, japo sikumbuki siku ile pale ikulu nilijibiwa nini, lakini sasa ndio Rais Samia, amemjibia.

Waswahili wana msemo, "anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga!", jambo linalozuiliwa kwa utashi tuu, bila kifungu chochote, cha katiba au sheria, sasa limeruhusiwa kwa utashi tena, bila kutumia kifungu chochote cha katiba na sheria. Jambo lolote lililozuiliwa, linaporuhusiwa, hatua ya kwanza ni kushukuru kwa jambo hilo kurusiwa, hivyo Watanzania wote tujiunge pamoja na kusema kwa kauli moja, "Asante Sana Mama".

Tena afadhali ya hili la haki ya mikutano ya siasa, limefanywa kwa utashi tuu kwa kutumia kauli tuu, yaani mikutano ilizuiliwa kwa kauli, na sasa imeruhusiwa kwa kauli, lakini kuna na haki nyingine mbili ambazo ndizo haki kuu za kiraia zilizotolewa na katiba yetu, haki za kuchagua na kuchaguliwa, haki moja kati ya haki mbili hizo, imegeuzwa hisani!. Haki ya kuchagua yenyewe bado ipo, ila haki ya kuchaguliwa imegeuzwa hisani!.
Hakuna mwana CCM hata mmoja anayethubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi.
Wewe Paskali huwezi kuthubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi, hususan kwenye 'forum' za CCM.
Duh...!, Mkuu fundimchundo , karibu bandiko hili, jee hapa ninadai nini?.
P
 
.
Kwa vile Rais wetu Mama Samia, keshaonyesha utashi, kwa kauli na matendo, tuzidi kumuombea ili Mungu amuwezeshe ayaweze yote haya kabla hajamaliza awamu yake hii ya kwanza, ili hata ikitokea akaendelea kwa awamu ya pili, hiyo itakuwa ni awamu ya shukrani na kumpa asante kwa aliyotatenda, na sio awamu ya kukamilisha ambayo hayakumamilika.

Mungu Mbariki Rais Samia

Mungu Ibariki Tanzania

Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Back
Top Bottom