Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Hakika yake,
For wonderers and adventurers!
Vitabu vinakusafirisha kiakili utajikuta places na nyakati zisizofikika kabisa.

tuwahimize watoto wetu kusoma ni utamaduni mzuri sana, kuna majibu mengi ya changamoto zetu kwa namna ya tofauti ya kipekee sana, mimi nasoma naye page kwa page, tunaulizana tumejifunza nini? author kafail wapi, kafaulu kufikisha ujumbe gani nk
It sharpens his mind zaidi na zaidi, siyo rahisi kwa sababu ya hizi games na animated series ila tunapambana hivyo hivyo kuna kukasirikiana kabisa lakini tunasonga.
Safi sana mkuu! Keep it up.

Naamini, kama alau nusu ya the so called Wasomi nchini mwetu wangevidhamini Vitabu zaidi ya wanavyodhamini vyeti vyao, kungeweza kuleta utofauti mkubwa sana. Usomi wao ungethihirika kwa vitendo!!!

Kwa mara nyingine tena, hongera! Unamwonesha mwanao njia sahihi! Keep it up.
 
Sio vitabu tu, hata picha,movie,miziki,maongezi,simulizi, na vitu vyote vinavyoingia kupitia macho na masikio ni chakula cha ubongo.

Hivyo basi, imekupasa mwanadamu kuwa makini na kile unacholisha ubongo wako.
Kwakuwa You are what you eat.

Huwezi kupanda mahindi ukategemea kuvuna mpunga.
Asante.Mfano JF unaizungumzaje,ni nzuri kwa ubongo au? Please be honest kwenye jibu
 
Sio vitabu tu, hata picha,movie,miziki,maongezi,simulizi, na vitu vyote vinavyoingia kupitia macho na masikio ni chakula cha ubongo.

Hivyo basi, imekupasa mwanadamu kuwa makini na kile unacholisha ubongo wako.
Kwakuwa You are what you eat.

Huwezi kupanda mahindi ukategemea kuvuna mpunga.
Naam! Kwa kadiri ya ufahamu wangu, ni sahihi kwa asilimia mia moja. Kiingiacho ndicho kitokacho!

Ukitaka kufahamu movie zinazotazamwa kwa wingi na watoto wa eneo fulani, ni rahisi sana. Fuatilia michezo yao. Sikiliza na maongezi yao.

Ukimsikia akiigiza kama Shehe, ujue amekuwa akimsikia Shehe mara nyingi zaidi kuliko wengine. Ukimwona anaigiliza kuomba kichungaji, ni matokeo ya kilichomo akilini mwake.

Je ukimsikia alisema, "IYAA!! ISH! ISH! ISH!", huku akifanya ishara kama wacheza kung fu, utashindwa kuelewa Movie za kung fu ndizo zimekuwa Mwalimu wake?

Kila kitu kiingiacho akilini, iwe kwa bahati au kwa kukusudia, vitatafuta kujidhihirisha kwa nje

Ndiyo maana mkubwa mmoja kule Marekani aliwakataza wasaidizi wake kumpelekea gazeti lo lote litakalokuwa limemwandika vibaya. Alijua kuwa linaweza likamtoa kwenye reli.

Ni muhimu sana kulinda fikra zetu na za watu wetu.
 
Mungu akubariki!

Umetoa msaada mkubwa sana kwa watu watakaokuelewa ulichoshauri!

Vitabu vina maarifa mengi sana!

Vina majibu yote muhimu ktk MAISHA!

Hongera sana!
🙏🙏🙏
 
Hadithi za alfu ulela tu.

Baada ya kusoma hivyo vitabu, hali ya kiuchumi imeongezeka? Kama ni hapana, hapo tunachoshana bure tu.
 
Naam! Kwa kadiri ya ufahamu wangu, ni sahihi kwa asilimia mia moja. Kiingiacho ndicho kitokacho!

Ukitaka kufahamu movie zinazotazamwa kwa wingi na watoto wa eneo fulani, ni rahisi sana. Fuatilia michezo yao. Sikiliza na maongezi yao.

Ukimsikia akiigiza kama Shehe, ujue amekuwa akimsikia Shehe mara nyingi zaidi kuliko wengine. Ukimwona anaigiliza kuomba kichungaji, ni matokeo ya kilichomo akilini mwake.

Je ukimsikia alisema, "IYAA!! ISH! ISH! ISH!", huku akifanya ishara kama wacheza kung fu, utashindwa kuelewa Movie za kung fu ndizo zimekuwa Mwalimu wake.

Kila kitu kiingiacho akilini, iwe kwa bahati kwa kusudiwa, vitatafuta kujidhihirisha kwa nje

Ndiyo maana mkubwa mmoja kule Marekani aliwakataza wasaidizi wake kumpelekea gazeti lo lote litakalokuwa limemwandika vibaya. Alijua kuwa linaweza likamtoa kwenye reli.

Ni muhimu sana kulinda fikra zetu na za watu wetu.
Na mbinu wanayoitumia watawala kuwacontrol watu ni kupitia Media.
Media zinaweza kushape mawazo ya jamii na kuicontrol wanavyotaka.

Watu wengi wanadhani wako 'free' lakini hawajui kuwa wako controlled na vile vinavyongia kichwani.
Uhuru tulio nao ni ule wa kuchagua kipi kiingie kichwani kipi kisiingie, ila kikishaingia hicho kitakucontrol na kitakuwa Master wako.

Mfano: Zamani kabla ya luninga na smartphone ilikuwa kumkuta mwanamke binti anadanga na ana wanaume 6,7,10 ilikuwa ni nadra. Mabikra walikuwa wengi.

ila baada ya miziki kuimba sana "sikuhizi hakuna mapenzi yale ya kupendana ni zama za kale", "All I need is one night stand" "Mapenzi pesa kuhongwa bana" na movies kuonyesha usaliti na umalaya. Social media kujaza page za wadangaji na kina gigy money.

Imeshakuwa ni kawaida kwa binti wa kitanzania kuwa na mabwana wengi na kuona mapenzi kama biashara ya kutafutia pesa.
 
Ingetungwa sheria ili uwe kiongozi lazima udhibitishe kwamba ni msomaji wa vitabu. Msoma vitabu ana maarifa mengi sana
Kutokuwa msomaji kunachochea mawazo mgando.

Ndiyo maana wengine, hasa Wazungu (sijui na wewe ni miongoni mwao!), huwajengea watoto wao tabia za usomaji tokea wakiwa tumboni.

Ndiyo maana ukipanda ndege yenye abiria kadhaa wa Kizungu, si rahisi umkose mwenye kitabu mkononi.
 
Na mbinu wanayoitumia watawala kuwacontrol watu ni kupitia Media.
Media zinaweza kushape mawazo ya jamii na kuicontrol wanavyotaka.

Watu wengi wanadhani wako 'free' lakini hawajui kuwa wako controlled na vile vinavyongia kichwani.
Uhuru tulio nao ni ule wa kuchagua kipi kiingie kichwani kipi kisiingie, ila kikishaingia hicho kitakucontrol na kitakuwa Master wako.

Mfano: Zamani kabla ya luninga na smartphone ilikuwa kumkuta mwanamke binti anadanga na ana wanaume 6,7,10 ilikuwa ni nadra. Mabikra walikuwa wengi.

ila baada ya miziki kuimba sana "sikuhizi hakuna mapenzi yale ya kupendana ni zama za kale", "All I need is one night stand" "Mapenzi pesa kuhongwa bana" na movies kuonyesha usaliti na umalaya. Social media kujaza page za wadangaji na kina gigy money.

Imeshakuwa ni kawaida kwa binti wa kitanzania kuwa na mabwana wengi na kuona mapenzi kama biashara ya kutafutia pesa.
Wanasema mihimili ya utawala ni mingapi vile? Mitatu? Hapana, kuna wa nne usio rasmi, na unaweza ukawa na nguvu hata kuizidi hiyo mingine mitatu, isipothibitiwa. Mhimili wenyewe ni MEDIA.
 
Nilichojifunza, ambacho hakijathibitishwa na TCU ni kuwa, kusoma Vitabu vya darasani, madhalani kwa mwanafunzi, kumtamsaidia kufaulu mitihani ya darasani. Na kujisomea Vitabu mbalimbali kwa lengo la kujiongezea maarifa ya kimaisha, vitakusaidia kupata majibu ya kimaisha, na hata kuboresha utumiaji wa vyeti ulivyopewa shuleni.

Kwa hiyo, kusoma kunapaswa kuwa sehemu ya maisha. Haina kustaafu.

Ndiyo maana bilionea wa Marekani, Warren Buffett, pamoja na kuwa na umri wa miaka 92 kwa sasa, bado anasoma Vitabu kila siku.

Alipokuwa kijana, alikuwa akisoma kurasa 1,000 kwa siku. Kwa sasa, anasoma alau kurasa 500.

Halafu kuna watu bado wanashangaa kwa nini Wazungu wanaendelea kuwazidi Waafrika kwa mafanikio? Sababu mojawapo inaweza ikawa ni hiyo, VITABU!!!
Point hapa ni hii!

Hapo juu ulionesha tofauti kati ya UBONGO na Akili.

Brain vsv Intelligence.

Sasa unapo discipline UBONGO wako kwa kupokea Positive Energies kupitia Maandishi yaliyosababishwa na Intellectual Intelligence moja kwa moja unapanua capacity ya Brain kumudu kupokea na kuchuja messages mbalimbali na hivo kupata majawabu yasiyokuwa na mashaka.

Vitabu ni Energies of Minds captured on the Paper....so unapitisha machapisho hayo kwenye Desk top ambayo ni UBONGO na kisha una transform tena kuwa Mind Energy into your own understanding.

Kusoma vitabu ni SIRI YA MAISHA KUPITIA UFAHAMU BORA KABISA.
 
Wao! Wonderful!!!

Sijutii kuwemo kwenye hili jukwaa, where mind sharpens mind!

Shukrani nyingi zikufikie hapo ulipo.
 
Hadithi za alfu ulela tu.

Baada ya kusoma hivyo vitabu, hali ya kiuchumi imeongezeka? Kama ni hapana, hapo tunachoshana bure tu.
Kwa mwaka huu umeshasoma Vitabu vingapi?

Ni vigumu kuifahamu ladha halisi ya asali ikiwa hujawahi kuilamba.

Maadam unajua kusoma na kuandika, chukua Vitabu kadhaa uvisome, ndipo utakapokuwa na uhalali wa kupinga au kuunga mkono.

Toafuti na hapo, msomaji wa Vitabu kubishana nawe itakuwa ni sawa na kukuonea. Atakuwa akiongelea anachokijua na wewe kujitutumua kujibu usichokijua.
 
Ni sahihi zamani nilipenda sana kusomaa vitabu tofaut hata vya dini ,,nilikua tofaut kuongea kufanyaa kazi na kujiamin hata Kuna wakati nilikua namua kuruhusu kuulizwaa swali lolote na kulijibu kwa ufahasa sio kwa sababu nilikua nimesomea vitu vingi hapana ni vile uwezo wa kufikir ulikua juu,,ukitaka kua kiongozi mzuri soma vitabu vingi.
 
Namfahamu Mtanzania mmoja, lakini simtaji jina. Alishawahi kusimulia kuwa siku chache baada ya kuajiriwa kama mhudumu wa afya kwenye Zahanati kama siyo kituo cha Afya cha Serikali, alisoma kitabu cha Napoleon Hill: THINK AND GROW RICH!
Matokeo yake? Kesho yake aliacha kazi. Kitabu alichokisoma kilibadili mwelekeo wa maisha yake. Sasa hivi ni miongoni mwa wafanyabiasha wazawa Tanzania, akimiliki makampuni ndani na nje ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom