Share hapa vitabu ulivyosoma
Mkuu, sina uhakika kama nimekuelewa ipasavyo, na sina uhakika pia kama nitakavyojibu ndivyo inavyohitajika.
Lakini kwa kuwa hili ni jukwaa la vichwa timamu, naamini, makosa nitakayoyafanya yatarekebishwa na hivyo kuwa na manufaa kwangu na kwa wengine wengi pia.
Nimevisoma both spiritual na visivyo spiritual, lakini hapa nitagusia non spiritual pekee. Hivi ni baadhi:
1. HOW YOU CAN GET RICHER QUICKER; By M. R. Kopmeyer
Ingawa sikubaliani na kila kitu kilichoandikwa na Kopmeyer, ambaye anajiita AMERICA'S SUCCESS COUNSELOR, kitabu chake hicho ni miongoni mwa vitabu ambavyo nimetokea kuvikubali sana. Nilichojifunza kwenye Vitabu vyake, hicho kikiwemo, kimenisaidia mimi binafsi na hata kuniwezesha kuwasaidia wengine.
Ni kwenye hicho kitabu nilikutana, kwa mara ya kwanza, na neno "SUBCONSCIOUS MIND".
Nilipofahamu kuwa taarifa yoyote utakayofanikiwa kuipenyezea subconscious mind kitakachofuatia ni utekelezaji, niliamua kufanya jaribio kwa mfanyakazi mwenzangu. Nilimwaminisha kuwa ana sifa ya kuweza kupandishwa cheo, na baada ya muda, alichukua hatua iliyompelekea kuwa hivyo.
2. FAILING FORWARD; by Dr. John C. Maxwell
Kinahamasisha kutokuhofua kufeli. Kinaaminisha kwamba FAILURE IS A BLESSING IN DISGUISE. Kutokufikia matokeo uliyoyakusudia, siyo kwamba umeshindwa, bali ni ujumbe kuwa kuna mabadiliko yanayohitajika. Kwa sababu hiyo, hupaswi kumlaumu mtu yeyote, au hata kitu chochote. Ukilaumu, utakuwa umeweka sahihi kuwa umeshashindwa.
Lakini kama utauruhusu mtazamo chanya kukutawala, utajiaminisha kuwa hujashindwa ila kuna marekebisho yanayohitajika. Kwamba, umegundua njia ambayo haitakufikisha unakotaka, hivyo inakulazimu kujaribu njia nyingine mpya, ambayo huenda ikakufanikisha.
Kati ya visa vilivyonifurahisha kwenye hicho kitabu, ni habari ya mtu mmoja aliyeishia kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa baada ya kufukuzwa kazi ya ulinzi.
Akiwa ameajiriwa na Kanisa la Anglikana kama mlinzi nchini Uingereza, ilibainika kuwa hakuwa akijua kusoma wala kuandika, na hivyo mwajiri wake akaishia kumfukuza kazi.
Hali hiyo ilimlazimu kufungua kaduka kadogo ili kupata hela ya kujikimu, lakini miaka michache baadaye, kaduka kake kalizaa maduka mengine mengi na kumfanya kuwa miongoni mwa matajiri mtaani kwao. Hakujua kusoma wala kuandika, lakini alikuwa tajiri na maarufu.
Siku moja alipoulizwa na mwandishi wa habari kuwa ingelikuwaje kama angekuwa anajua kusoma na kuandika; alijibu, "Ningekuwa mlinzi wa Kanisa la Anglikana".
Kufukuzwa kwake kazi kwa sababu ya kutokujua kusoma na kuandika kulimchochea kugundua uwezo wake wa kufanya biashara na kumfanya kuwa tajiri kumzidi aliyekuwa bosi wake. Kuachishwa kazi kuligeuka kuwa baraka kwake. Ndiyo maana wanasema, FAILURE IS NOTHING BUT A BLESSING IN DISGUISE!
3. AWAKEN THE GIANT WITHIN; By Anthony Robbins
Miongoni mwa mambo nilivyojifunza ni umuhimu wa kuweka Lengo na kuzielekeza fikra zako zote huko kwenye hilo lengo.
Hilo lengo, ikiwa limembatana na hisia kali sana, au umelitafakari kwa muda mrefu, huishia kuwa maelekezo kwenye subconscious mind. Bila kujali kama ni zuri au baya, subconscious mind itakutengenezea mazingira ya kuwa vivyo hivyo, sawa sawa na lengo lako.
4. SNOW BALL: WARREN BUFFETT AND THE BUSINESS OF LIFE
Kitabu chake kilinihamasisha kusoma vitabu zaidi. Alinitia wivu alivyoelezea jinsi alivyoanza kusoma vitabu akiwa na umri wa miaka saba. Alipofikisha miaka tisa, alianza kufanyia kazi alichokuwa akisoma.
Tabia yake ya usomaji ilimpelekea kuwa mwekezaji mkubwa sana ndani na nje ya Marekani.
5. THE LAWS OF SUCCESS; by Dr. Napoleon Hill
Kati ya mambo ambayo nayakumbuka, ni jinsi maneno mtu anayoyasikia yanavyoweza kuitawala akili yake kulingana na asili ya hayo maneno.
Kwa mbinu ijulikanyo kama SUGGESTION, mtu anaweza kutawala fikra za mtu mwingine, na kwa AUTOSUGGESTION, humsaidia kuzitawala fikra zake binafsi.
Ikitokea subconscious mind, kwa mfano, ikaaminishwa kuwa "huyu mtu anatakiwa kufa, "itakachofanya ni kuyasimaisha mapigo ya moyo na hatimaye lengo kufikiwa.
6. HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE; By Dale Carnegie
Kimenisaidia kuwaelewa watu wengine na kuniepusha na uwezekano wa kukasirika kirahisi pale ninapotendewa jambo la kukwaza. Kimenisaidia kufahamu kuwa kati ya hitaji kubwa sana kwa kila binadamu, ni shauku ya kutambuliwa.
Kwa hiyo, hata inapotokea wakati mwingine mtu akanikosoa kwa namna isiyo na staha, nakumbuka kuwa huenda nafsi yake ina njaa sana ya kutambuliwa. Yeye mwenyewe anayefanya hivyo hajui hilo, ila kwa mwelewa, atajua kuwa hicho ni kilio cha ndani kinachotaka mhusika naye apewe attention! Kwa hiyo, badala ya kujibu kwa hasira, nitatenda kulingana na nitakavyoona inafaa.
7. THE RICHEST MAN IN BABYLON, By Samuel G. Classon
Huwezi kujisomea hicho kitabu na usione umuhimu wa kuweka akiba (savings)
8. STAY LOCAL AND GOING GLOBAL
Silikumbuki jina la mwandishi, ila ni Mnigeria. Ndicho kitabu cha kwanza kujifunza umuhimu wa SYSTEM (mfumo) kwenye kazi/biashara. Kwamba, kama utaanzisha biashara ambayo hutaki ubanwe na uendeshaji wake, yakupasa kutengeneza mfumo utakaoweza kumtawala kila mtu atakayekuwa akifanya kazi humo.
9. CASHFLOW QUADRANT; By Robert Kiyosaki
Kimeelezea vyanzo Vikuu 4 vya fedha/ utajiri na umuhimu wa kilia kimoja: EMPLOYMENT, SELF EMPLOYEE, BUSINESS & INVESTMENT.
The quickest of all, in most cases, katika kufikia utajiri wa haraka, ni BUSINESS. Lakini ambayo haina stress ni INVESTMENT. Ukiwekeza, fedha yako itakuwa ikifanya kazi kwa niaba yako
10. THOUGHTS TO BUILD ON; By M. R. Kopmeyer
Wazo aliwazalo mtu muda mrefu, hatimaye huishia kulitenda. Kwa hiyo, maisha ya mtu ni jumla ya mawazo aliyowahi kuwaza.
11. HOW TO START A MULTIBILLION BUSINESS IN AFRICA FROM THE SCRATCH; By Strive Masiyiwa.
Bilionea huyu mwenye uraia wa Zimbabwe na Uingereza, ameelezea jinsi MANAGEMENT ilivyo ya muhimu sana kwenye biashara. Ndiyo uti wa wa mgongo wa biashara yoyote ile.
Humo utakutana na masuala ya:
(A). Financial Management
(B). Human Resources Management,
E.t.c.
12. WHO WILL CRY WHEN YOU DIE; By Robbins Sharma
Kati ya vitu nilivyojifunza ni umuhimu wa kuwa na kauli ya kujisemesha mara kwa mara kwa lengo la kutawala fikra zako. Kwa mfano, kama unaenda kufanya presentation mbele ya watu ambao hujazoeana nao, na ukawa unahofu kuwa huenda utakosa ujasiri wa kuzungumza mbele yao, unaweza ukaamua kujisemea mara kwa mara, "KUONGEA MBELE YA UMATI WA WATU NI JAMBO RAHISI SANA". Kwa kufanya hivyo, kila seli ilyopo kwenye mwili wako itaelekezwa kukufanya ujisikie hivyo na kutenda hivyo.
Nilipompatia hicho kitabu rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa Mwalimu wa Sekondari, aliishia kuacha ajira ya ualimu baada ya kukisoma.
Nilipokutana naye baadaye, alinieleza kuwa hicho kitabu kilimfanya afahamu kuwa alichokuwa anakifanya(ualimu wa Sekondari) sicho alichoumbiwa kufanya.
Aliacha kazi ya ualimu na kuanzisha shughuli zake binafsi.
Jamani ee, nimejaribu kwa kadiri ya ufahamu wangu, ila mpaka sasa, sijui kama ndicho kilichokuwa kinahitajika.