Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Kwel kabisa ,kuna kipind nilikua nimekataa tamaa ya maisha ,sababu ya kero za mimba changa,yaan ile tapikatapika ,kukerwa na harufu za za karibu kila kitu iwe chakula,mafuta n.k.nikapata kwa rafik yangu kitabu kinaitwa"how to stop worries and start and start living" nikakisoma kwa utulivu mkubwa sana,aisee kilinibadilisha mind set nikapona kabisa,mate nkaacha kutema ,nkaanza kula kila kitu,nakurejea na majukumu yangu nikiwa imara kabisa.mpaka leo huwa sikisahau kuna vitu naviapply kwny maisha yng kupitia kile kitabu na majib ni mazur ,
Mkuu naomba soft yake[emoji120]
 
Nafikiri ni tabia ya Waafrika wengi. Ndiyo maana wengi wakishahitimu masomo wanaagana na vitabu.

Kwa Wazungu wengi, ni jambo la kawaida kujiwekea bajeti ya Vitabu kila mwaka.

Lakini kwa Watanzania, ni wachache sana wanaofanya hivyo.
nakubaliana na wewe
 
Hadithi za alfu ulela tu.


Baada ya kusoma hivyo vitabu, hali ya kiuchumi imeongezeka? Kama ni hapana, hapo tunachoshana bure tu.
Mimi nilikuwa sijiamini kupanga statement hata kwenye vikao au waandishi wa habari wakija si ndo nikafunguka kwa jamaa yangu ambae yeye mzuri wa presentation akaniambia angalia movies na soma na vitabu sana leo hii kwenye kikao nondo nazotoa mpaka mi mwenyewe huwa najipigia makofi kichwani mwangu.Umetoa mfano wa vitabu vya alufu lela ulela ndio unaweza ukavidharau ila ni moja vitabu maarufu sana vya zamani ambavyo vimejaa fiction za majini ambapo nia ya vitabu ni KUELIMISHA,KUBURUDISHA NA KUFIKILISHA.
 
IMG_2032.png

Now on to this one “Economics in one Lesson” … Mwandishi wa hiki kitabu aende direct mbinguni. Ideas kibao jamaa kazifanya simple sana
 
Kwamfano mimi sijawahi kusoma ata kitabu kimoja.

Naanzaje? Nipe tips nianze mdogo mdogo.

Je, ata kusoma vitabu vya story ni msosi wa Medulla oblongata? Au lazima viwe vitabu vya "How to become Wiseman"? "You was born to win"?
Anza mdogo mdogo
Ili mradi ujijengee mazoea ya kusoma Soma baadae ukizoea hutaona uvivu kusoma Kuna kitabu nilikisoma masaa 12 non stop
 
Ndiyo, kama ni story nzuri za kujenga. Lakini Mimi binafsi, kwa upande wangu, non fiction vinaweza vikawa ni vizuri zaidi.

Vitabu siyo chakula cha ubongo bali akili. Mimi siyo mtaalam wa Saikolojia lakini nafahamu kuwa ubongo siyo akili na akili siyo ubongo.

Ubongo ni kama hardware na akili ni software.

Unaposoma, yale maneno yanayoingia kwenye akili yako huweza kuathiri na utendaji kazi wa ubongo wako.

Ndiyo, maneno huweza hata kumwua mtu, ikiwa hayo maneno yataielekeza akili kufanya hivyo. Akili itakachofanya ni kuiamuru ubongo kusitisha utendaji kazi wake, na ubongo ukiacha kufanya kazi matokeo yake yanafahamika, kifo.

Lakini yakiwa chanya, yanaweza kumletea mtu manufaa makubwa sana.

Ndiyo maana ni muhimu sana kuwa makini na unachokidoma. Kitakubadilisha bila wewe kujua, sana sana ni watu wanaokufahamu ndiyo watakaobaini mabadiliko yako.

I tell you the truth, vitabu vinaweza kuathiri hata mwonekano wako wa nje. I know what I am talking about. Sijasimuliwa. Nimeiona kwa macho yangu.

Maneno humjengea mtu taswira fulani akilini mwake, na hiyo taswira hutawala matendo yake.

Maneno yanayoingia kwa wingi kwenye ufahamu wako hatimaye yatatafuta jinsi ya kujithihirisha kwa vitendo.
Naye NENO akafanyika Mwili akakaa kwetu...........Yohana 1:14a neno analosoma mtu linaweza kumbadilisha na kumfanya afanane na Mawazo ya mwandishi wa kitabu...
 
400? Too much, vya subject hiyo hiyo
400 ni vitabu vingi, tena kwa miaka zaidi ya kumi?

Ikiwa kwa mwaka utavisoma alau vitabu hamsini tu, kwa miaka kumi utakuwa umesoma vingapi?

Nilivyovisoma mpaka sasa ni zaidi ya 400, na ni zaidi ya 500 pia.

Mpaka 2020, nilikuwa nimeshavuka 400, hivyo kwa sasa ni zaidi ya 500.

Lakini, pamoja na hayo, siwezi kusema kuwa nami nimesoma vitabu vingi. Hata hapa Tanzania tu, kuna watu ni wasomaji sana.

Nilipoanza kusoma vitabu kwa "ulafi", nilifikiri ni mimi peke yangu ndiye msomaji sana wa vitabu Tanzania, lakini nilipokutana na wasomaji wengine, nilibadili mtazamo. Nilifahamu Tanzania ina wasomaji ambao kama tungeshindanishwa, mimi ningeweza kuonekana ningali level ya chekechea.

Ni kweli ninasoma soma Vitabu, lakini simo kwenye kundi la wanaosoma sana vitabu duniani wala Tanzania.

Hata hapa Tanzania tu, kuna wasomaji ambao mimi binafsi nawakubali kuwa ni wasomaji walio serious. Wanatembea na hii kauli mbiu: MISS YOUR MEAL BUT NOT YOUR READING!

Kwa kipindi cha miaka kumi, ilipaswa niwe kwenye Vitabu zaidi ya elfu moja na siyo mamia.

Miaka ya nyuma, Profesa Kitila Mkumbo alitoa makala kwenye Gazeti la Uraia Mwema iliyohusiana na usomaji vitabu. Aiweka na idadi ya Vitabu vilivyosomwa na viongozi kadhaa wa Marekani. Mfano, Bill Clinton, alipofikisha umri wa miaka thelathini, alikuwa ameshasoma jumla ya vitabu elfu thelathini(30,000).

Kusoma Vitabu 400 kwa kipindi cha miaka kumi ni "uzembe"
 
Yaani mimi nikiamua nikae nishike kitabu nisome ni 30 seconds tu hamu ya kusoma inaisha hivyo ni kujilazimisha na nikilazimisha utamu siupati vizuri....


Nifanyeje?
Relax! Usitumie nguvu nyingi kukielewa, just read for leisure. Ukitulia nacho kwa muda kama nusu saa hivi, akili yako itajua umedhamiria kukisoma, itaanza kukupa ushirikiano na kujikuta unaanza kukielewa na hata kukipenda.

Tatizo linaweza likawa unasoma huku unawaza mambo mengi hivyo akili inadhindwa kutulia kwenye usomaji.

Kama ndivyo, unapaswa kusoma kwa kasi kubwa sana ili mawazo yako yawe busy kwenye jambo moja tu, up nachokisoma.

Ukiona na hilo halijasaidia, badilisha mbinu. Soma kwa sauti. Kwa kawaida, si rahisi kuwaza na kuongea vitu viwili tofauti kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom