Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Shukurani sana mkuu. Ngoja nianze kupakua kimoja baada ya kingine na kuvisoma. Nitakavyoshindwa kuvipata nitakuomba tena utusaidie namna rahisi ya kuvipata.
Karibu.
 
Hii ni kweli kabisa, Mimi binafsi nimejitahidi Sana kusoma vitabu Ila nimeshindwa na cjajua shida ni nini, Ila nilisema ntahakikisha mtoto wangu atapenda kusoma vitabu, na namshukuru Mungu kwa Hilo mwanangu ana umri wa miaka 8 tayari anasoma chapter book. Na baba yake kwa kuwa ni msomaji Sana wanaulizana maswali na tumekuja kuona faida yake yaani yuko year 4 Ila anaandika story ambayo hata Mimi nabaki nimeshangaa. Na siku zote anaongoza English kwenye darasa lake. So Mimi kazi yangu ni kuzunguka kutafuta vitabu baba yake kazi yake ni kusoma nae. Kama Sisi tumeshindwa basi tuwekeze kwa watoto.
 
Haujashindwa, bali hujaamua. Lakini hongera kwa uwekezaji bora unaoufanya kwa mwanao.
 
Hahahahah! babu kubwa ni kusoma kwa sauti kubwa tu
 
Dhamini Vitabu kuliko unavyoldhamini chakula cha kawaida..... Mkuu uko vizuri na Vitabu vyako
 
Tumia akili zako ili kurutubisha na kujenga zaidi akili na hatimaye zikupatie matokeo.
Kama haunazo, au akili zako ni dhoofu, basi soma vitabu ili uweze kuziimarisha.
Akili zinakua unapozishughulisha kwa kufanya jambo. Siyo kwa kusomasoma tu vitabu.
 
Dhamini Vitabu kuliko unavyoldhamini chakula cha kawaida..... Mkuu uko vizuri na Vitabu vyako
Nashukuru mkuu, ila mpaka sasa vitabu ninavyovisoma ni vilivyoandikwa na wengine. Siyo vyangu kiongozi. Ila niko mbioni na mimi kuandika.
 
Tumia akili zako ili kurutubisha na kujenga zaidi akili na hatimaye zikupatie matokeo.
Kama haunazo, au akili zako ni dhoofu, basi soma vitabu ili uweze kuziimarisha.
Akili zinakua unapozishulisha kwa kufanya jambo. Siyo kwa kusomasoma tu vitabu
Samahani mkuu, unaweza ukafafanua tena kidogo? Kuna point sijaipata vizuri.
 
Wao! Kitabu kizuri sana: HOW TO STOP WORRYING AND START LIVING by Dale Carnegie.

Asante kwa huo ushuhuda. Usomaji vitabu unalipa sana!
Thanks mkuu,umekiandika correct kabisa,[emoji106][emoji106]kuna mdau hapo anaomba umsaidie softcopy yake,km hutojali mkuu
 
Thanks mkuu,umekiandika correct kabisa,[emoji106][emoji106]kuna mdau hapo anaomba umsaidie softcopy yake,km hutojali mkuu
Ni problem mkuu! Nikipata nafasi nitaingia kwenye "ghala" langu la soft copy books nione kama kipo. Nikikikuta nitakiweka. Nitacheki baadaye.
 
Naunga mkono hoja✍️✍️
 
Swadakta ndicho chenyewe, swali langu vitabu vinapatikanaje kiurahisi?
 
SIku hizi kuna aodio book za kila kitabu hivyo hata kama mtu mvivu kusona asikilize tu.
Kitabu cha mwisho mimi kukisoma kiundani ni kitabu cha dr wilson ambacho ni hotuba ilowekwa ktk maandishi.
Capitlist Nigger.
Nilichokipenda ktk kitabu kile ni kushawishi watu weusi kusoma vitabu.
Hii ina naana tusome kila kitabu kilichopo duniani.
Kwa mujibu wa dr wilson tutaweza kufanya na kuwazidi waliotupita.
Dr wilson anasema tutaweza kutengebeza kila kilchopo ambacho hatujui siri yake.
Bahati mbaya sana waafrika wengi tumeendelea kukataa rabia ta kusona vitabu.
Wenzetu wamarekani wameteua 100 books, a must read boojs ikiwemo koran na bible.
 
Please, tafadhali sana mkuu! Niambie pa kukipata hicho kitabu.
 
Kupitia google siku hizi unasoma na kupata tu Yale maarifa uyatakayo
 
Swadakta ndicho chenyewe, swali langu vitabu vinapatikanaje kiurahisi?
Hard copy waweza pata madukani.

Soft copy vipi vinavyouzwa na kuna vinavyopatikana free of charge, ni bundle lako tu

Ingia mtandaoni ujaribu kuvidownload.

Ninatarajia kuviweka vichache humu ila namna ya kuviweka ndiyo bado kunanisumbua. Nikifahamu jinsi ya kufanya nitaviweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…