Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Unadaiwa ada za watoto, pesa ya kujikimu huo muda wa kuupa ubongo chakula unapata wapiii?
Ikiwa unapata muda wa kula "ugali" ili usife, na inapata muda wa kulala kwa sababu ni hitaji la lazima, huwezi kukosa muda wa kusoma ukishaufshamu umuhimu wake.

Hata hayo uliyoyataja: ada ya watoto na pesa ya kujikimu, unaweza kupata ufumbuzi wake endapo utasoma vitabu sahihi na kufanyia kazi maelekezo yake.
 
Embu tuwe realistic. Huna hata pesa y nauli ya daladala kitabu cha 50000 utanunua ukianzia wapi?
Si lazima ununue cha elfu hamsini! Inategemeana na kitabu unachokitaka. Vipo mpaka vya sh 500/=, na sehemu zingine unaweza kupata hata vya bure.

Si lazima ununue cha elfu hamsini, unaweza kuazima.

Kwa sababu huna nauli, mwanao akiugua ghafla, utamwacha aendelee kuteseka ndani kisa huna hata nauli?

"Why" ina nguvu zaidi ya "How".

Ukishakuwa na sababu kubwa kuzidi uhalisia unaokikabili, hatimaye utapata namna ya kufikia lengo.

Hata Vitabu, vikishakuwa ni vya muhimu sana kuzidi chakula cha mwili, utavipata na kuvisoma hata kama huna senti.
 
Kwamfano mimi sijawahi kusoma ata kitabu kimoja.

Naanzaje? Nipe tips nianze mdogo mdogo.

Je, ata kusoma vitabu vya story ni msosi wa Medulla oblongata? Au lazima viwe vitabu vya "How to become Wiseman"? "You was born to win"?
anza kusoma vitabu vyenye kurasa chache,polepole utazoea
 
Si lazima ununue cha elfu hamsini! Inategemeana na kitabu unachokitaka. Vipo mpaka vya sh 500/=, na sehemu zingine unaweza kupata hata vya bure.

Si lazima ununue cha elfu hamsini, unaweza kuazima.

Kwa sababu huna nauli, mwanao akiugua ghafla, utamwacha aendelee kuteseka ndani kisa huna hata nauli?

"Why" ina nguvu zaidi ya "How".

Ukishakuwa na sababu kubwa kuzidi uhalisia unaokikabili, hatimaye utapata namna ya kufikia lengo.

Hata Vitabu, vikishakuwa ni vya muhimu sana kuzidi chakula cha mwili, utavipata na kuvisoma hata kama huna senti.

Mkuu unapoteza muda na hawa watu mtabishana mpaka kesho .. Uzi wa wasoma vitabu Kama mtu hataki unamuacha tu ipo siku ataelewa.
 
Daah kuna sisi wengne vitabu tunavyo vingi kwenye simu ila kusoma ndo wavivu

Au wenzangu mliwezaje kuzoea kusoma mana binafsi natamani niwe nasoma sana ila nikisoma page 2 au 3 naanza kuona michosho tu naamua kuhairisha
 
Hata hizo page 3 ni hatua. Unaweza kujiboresha zaidi.

Labda nikuulize! Vipi ikitokea ukapata "ofa" ya kulipwa shilingi laki Moja kwa kila ukurasa utakaousoma, kwa siku ungesoma kurasa ngapi? Kumbuka una majukumu mengine ambayo ni lazima uyatekeleze ama nyumbani au kazini, n.k. Ungesoma kurasa ngapi kwa siku?
 
Ukiwa na stress ni sahihi kufa njaa?

Kama hata mtu akiwa na stress bado anahitajika kula, ndivyo ilivyo pia na usomaji.

Ukiwa na stress, unaweza usiwe na muda wa kula na kunywa kwa anasa, lakini lazima kula chakula na kunywa maji kwa ajili ya kuendelea kuishi.

Ndivyo ilivyo na vitabu. Ni sehemu ya maisha ya akili yako. Isitoshe, stress inaweza kuchangiwa na upungufu wa lishe sahihi kichwani.

Kusoma Vitabu sahihi kutakusaidia ama kuepuka stress, kuishinda, au kuimanage.
Hapo kwenye vitabu sahihi.

Vitabu vya wakina Singano Jr sio sahihi?
 
Embu tuwe realistic. Huna hata pesa y nauli ya daladala kitabu cha 50000 utanunua ukianzia wapi?
Kama tu walivyo walafi wa ngono wanaweza kulipa lodge kwa ajili hiyo au walevi kuteketeza laki na point kwenye pombe , ndivyo ilivyo pia kwa wanaopenda vitabu.... Binafsi pale elite bookshop , shoppers plaza Dodoma na mpango wa kwenda kuvuta kitabu Fulani hivi Cha 86,000 , nangoja tu pesa inikalie vizuri .[emoji108][emoji108]
 
nimegundua kitabu cha 48laws kinatengeneza machawa au sijaelewa
Hapana , nakataa , wewe ni kitabu kipi unasoma? Zile sheria sio kwamba zitakuwa applied kwa kila mazingira. Kwa mfano kama una kitabu kile alichoandika Robert Greene, kila law imefafanuliwa vizuri kabisa kwenye kipengele kinaitwa keys to power.
Mfano huu hapa[emoji116].
IMG_20230606_144942_529.jpg

IMG_20230606_145007_956.jpg
 
nimegundua kitabu cha 48laws kinatengeneza machawa au sijaelewa

Zile laws ndo Hali halisi ya uongozi ulivyo, Kimeiba ideas kutoka viongozi mbali mbali yan kinaonesha tabia halisi za kiongozi vs tabia ya kuonekana kwenye Jamii . Fuatilia uongozi wa mtu Kama Hitler au hata Maraisi mbali mbali au Baba nyumbani zile laws ndo zenyewe .

Mfano nilivyokuwa nasoma chuo nilidhani kiongozi mzuri ni Yule Mkweli , ila sasa naona halisi ukiwa kiongozi mkweli umeisha, Kiongozi mzuri lazima uwe muongo muongo changanya na ukweli ila hakikisha unaaminika , hii nimeijua kutokana na uzoefu wa muda sasa ila chuo tunafundishwa tofauti kabisa.
 
Kwamfano mimi sijawahi kusoma ata kitabu kimoja.

Naanzaje? Nipe tips nianze mdogo mdogo.

Je, ata kusoma vitabu vya story ni msosi wa Medulla oblongata? Au lazima viwe vitabu vya "How to become Wiseman"? "You was born to win"?
Naomba kuongezea kwa waliochangia mambo mazuri hapo mwanzoni. Kitabu ni chemichemi ya maarifa. Inategemea unahitaji kuongeza maarifa upande upi wa maisha yako. Mfano kuna kitabu cha 100 rules for entreprenuers kinachouzawa na Sambazah.co kinagusia mambo ya ujasiriamali tu ambacho kitamfaa mfanyabishara na jinsi ipi ataelewa njia sahihi za ujasiriamali. Kuna vya self help, finance na zaidi. Ila swali linarudi kwako, je ungependa kukua katika sehemu ipi ya maisha yako?
 
Sijasoma vitabu vingi sana, lakini alau nimevisoma soma kidogo.

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, nimeweza kusoma Vitabu vichache, vikubwa kwa vidogo, vinavyozidi mia nne.

Nimeiona faida yake. Kuna faida sana. Ni CHAKULA muhimu sana cha akili, hakika!.

Mara tu baada ya kuianza hiyo tabia, nilijaribu kuwashawishi baadhi ya watu, hasa wasomi, kuiga hiyo tabia. Kuna siku, nafikiri nilikosea, nikaenda kumshawishi mtu aliyenizidi kitaaluma naye awe msomaji. Alichonijibu kilinifanya nisirudi kwake tena kwa sulala hilo. Niliamini, usomaji wa Vitabu ungweza kumwongezea mawazo ya kuboresha shughuli alizokuwa akizifanya.

Siku ya kwanza, pengine alinivumilia, hakunijibu chochote.

Nilipoamua kumpelekea orodha ya vitabu nilivyoamini kuwa vingemfaa, aliishia kunijibu, "hivyo Vitabu havifanyi kazi Tanzania"

Havifanyi kazi Tanzania? How? Kisa tu vilikuwa vimeandikwa na Wazungu? Iweje visifanye kazi Tanzania, wakati vingi ya Vitabu alivyovitumia Chuo Kikuu vilitoka kwa Wazungu?

Namshukuru Mungu sikutetereshwa na kauli yake, ila na mimi sikurudia kumshawishi katika hilo. Niliendelea kujisomea, na sasa imeshakuwa ni tabia yangu.

Nahisi, maarifa niliyoyapata kwa kujisomea mwenyewe vitabu nilivyojichagulia, yamenisaidia zaidia kuzidi maarifa niliyoyapata chuo kikuu.

Vitabu, hasa Vitabu vizuri, haviwezi kukuacha kama ulivyokuwa. Ila ukivisoma "visivyo" salama kwa akili, utakuwa hatarini pia.

Soma vitabu vizuri, hutajutia.

Wanasema, LEADERS ARE READERS!

Soma VITABU, Vitabu vizuri! Vina faidi tele!

Dhamini Vitabu kuliko unavyoldhamini chakula cha kawaida, ni CHAKULA muhimu sana cha akili yako.
Naomba tukushukuru na kusapoti usomaji wako wa vitabu kwa kukupa discount ya 10% kwa kitabu chochote utakachokua kwenye Sambazah.co .
 
Back
Top Bottom