Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Kilimanjaro- Kilimakyaro wazungu walikuwa wakishindwa kusema Kilimakyaro wakasema Kilimanjaro.
 
Banana bar= ukonga banana, ukonga mombasa- mombasa bar, 'Kimara stop over-stopover bar, kimara matangini- matanki ya maji, kimara baruti- ghala la baruti, magomeni mapipa- hifadhi ya mapipa ya lami wakati wa ujenzi wa morogoro rd. Temeke aziz ali- makao ya RPC wa kwanza wa dsm Aizi ali
 
Kongowe: Jina la Mzee wa Kizaramo mwenyeji wa eneo lile. Alikuwa na wake wawili, mmoja akiishi Kongowe ya Mbagala na mwingine Kongowe ya Kibaha.
 
Shekilango -Sheikh kilango alkw shkh maarufu,Bububu zanzibar-mlio wa treni bububu za makaa ya mawe enzi hizo treni ilikuwa inakuja dar,Bagamoyo-Bwagamoyo,sinza kwa remy-mwnmzk remy ongala alkw anaishi,Kamanyola-mzee kamanyola aliishi nyumba barabarani,nyama ya kitimoto-baa ya kwanza maeneo ya mwenge jirani na maghorofa ya customs ilikuwa imeandkw getini kitimoto ndo jina lilipoanzia hapo masheikh ubwabwa waliijia juu baa kuwepo mtaani kwao ikahamishwa!
 
Mnyamani-Mwinyi Amani, Vingunguti- vingungu kwa kizaramo ni vizee, na tii na kutia timu(kufika) sasa hivi vizee vilikuwa vinauza maeneo kariakoo na kuhamia vingunguti kwa wingi sana.. Ndo maana pakaitwa vingungu-tii.,yaani vizee vimetia timu! ubungo-kulikuwa na mbungo mengi.
 
Ubungo- limetona na ukweli kuwa eneo hilo palikuwa na pori kubwa na miti mingi na mikubwa ya mibungo, ndio mpaka leo pakaitwa hivyo.
Msasani- pale kulikuwa na wamakonde kwa wingi sana, na bahati mbaya palikuwa na mzee mmoja maharufu sana aliyekuwa akiitwa MUSA HASSAN, wamakonde walishindwa kulitamka hilo jina kuita msasani, na ndio mwanzo wa eneo hilo kuitwa hivyo.
 
Kurasini Mivinjeni, kulikuwa na miti ya mivinje mingi sana kando ya barabara ya kilwa road.
Kurasini Shimo la Udongo, walikuwa wanachimba mchanga wa kujengea nyumba. Yale mashimo kwa sasa wameyafanya mabwawa ya maji taka.
Ukonga mwembe madafu, kulikuwa na mwembe ambao wanauzia madafu.
Majumba Sita, kulikuwa na nyumba sita za jeshi kikosi cha anga zinafanana jirani na eneo hilo. Kwa sasa wamezungusha ukuta sijui kama bado zipo.
Ukonga Mzambarauni, kulikuwa na mti wa mzambarau.
Gongo la Mboto mwisho wa lami, zamani lami ndo ilikuwa inaishia hapo.
Ubungo External, kulikuwa na mitambo ya kurusha matangazo ya radio kwa lugha ya kingereza, external service.
Ubungo River Side, kuna baa moja kubwa ya mzee Mrema inaitwa river side.
Dodoma, tembo alipita sehemu fulani ya udongo laini akadidimia. Wagogo wakasema Ididimiya mzungu akashindwa ikabidi aseme dodoma. Inasemekana ardhi ya Dodoma ni laini sana. Inasemekana walipiga marufuku kujenga zaidi ya ghorofa nne.
 
Sinza kwa remmy, muimbaji remmy ongara, sinza makaburini kuna makaburi, sinza vatikani kuna bar, sinza kijiweni kulikuaaga na kijiwe, sinza madukan inajieleza yenyewe
 
I stand to be corrected, Kariakoo inatokana na neno Carrier Corps. Hii ilitokana na jinsi walivyokuwa wakiitwa askari wa Kibantu ambao walipigana vita vya pili vya dunia kwa upande wa mwingereza. Hilo eneo lilianzishwa baada ya wao kurudi kutoka vitani

Why "carrier corps"? Kwa nini wasingeitwa "makuli" au "coolies" ambalo ndilo lilikuwa jina maarufu kwa wabeba mizigo wa wakati huo?
 
Kijitonyama Sayansi= Uwepo wa jengo la sayansi na teknolojia
 
Kariakoo-Career Call sehemu ya makuli kupata ajira
Msasani-Kulikuwa na mwarabu akiitwa Mussa Hasan aliyekuwa na duka pekee hapo kijijini
Mwana nyamala-Kizaramo mtoto nyamaza,ambapo mama alikuwa anambembeleza mtotot katikati ya msitu uliokuwa na Simba hapo ilio mwananyamala leo.
Mikocheni-kulikuwa na miti mingi sana ya Mikoche ambayo hufanana na minazi

Carrier corp = Kariakoo
 
Shekilango -Sheikh kilango alkw shkh maarufu,Bububu zanzibar-mlio wa treni bububu za makaa ya mawe enzi hizo treni ilikuwa inakuja dar,Bagamoyo-Bwagamoyo,sinza kwa remy-mwnmzk remy ongala alkw anaishi,Kamanyola-mzee kamanyola aliishi nyumba barabarani,nyama ya kitimoto-baa ya kwanza maeneo ya mwenge jirani na maghorofa ya customs ilikuwa imeandkw getini kitimoto ndo jina lilipoanzia hapo masheikh ubwabwa waliijia juu baa kuwepo mtaani kwao ikahamishwa!

Shekilango nakumbuka alikuwa balozi wetu kule Uganda. Alifariki kwenye ajali ya ndege kule Monduli. Sinzo ndiyo ilikuwa inajengwa na barabara iliyokata katikati ya Sinza ilipewa jina la Shekilango kama kumbukumbu yake.
 
Banana bar= ukonga banana, ukonga mombasa- mombasa bar, 'Kimara stop over-stopover bar, kimara matangini- matanki ya maji, kimara baruti- ghala la baruti, magomeni mapipa- hifadhi ya mapipa ya lami wakati wa ujenzi wa morogoro rd. Temeke aziz ali- makao ya RPC wa kwanza wa dsm Aizi ali
Buguruni kwa mnyamani.
Mnyamani=Mwinyi Amani.
Huyu mzee alikuepo maeneo hayo....
 
Kinondoni kulikuwa na kipisi cha nondo barabarani, ukipita kwa miguu lazima ujikwae, ukipita na gari pancha
Mkuu hii kama umejitungia!!!kinondoni kwa manyanya!manyanya alikuwa mzee maarufu sana alifungua bar maeneo hayo!cha kushangaza bar hiyo iliandikwa kinondoni bar ila wateja bila kulazimishwa waliita kwa manyanya!!ilikuwa pembeni ya mwanamboka petrol station karibu na casablanca bar siku hizi!....
 
Habari wana JF,mwenye uelewa na chanzo,vyanzo vya majina ya sehem mbalmbal hapa dar anieahamishe kama k'koo,kinondon,mikochen,msasan,mbagala,bugurun nk. Si mbaya ukieleza hata maeneo ya mikoan.
Nawasilisha ....
upo uzi humu ndani utafute kwa bidii, unaweza kunitafuta kwa ku-pm but at a fee
 
Kama kichwa cha thiled kinavyojieleza....
kuna mbuga inaitwa saadani,asili ya jina hili inasemekana kipindi hiko kulikuwa na mzee mmoja wa kiarabu hapo mbugani,sasa wananchi wa karibu na eneo ilo walikuwa wakipita kutoka shambani na walipofika kwa huyo mzee wa kiarabu na kwa yeye alikuwa na duka na dukani pale aliweka saa ya ukitani.Basi watu kila wakipita wanamuuliza mzee saa ngapi? Mwanzoni alikuwa anawatajia lakini baada ya kuona kero akaamua kuweka saa yake ndani,sasa watu wakipita wanamuuliza mzee saa ngapi? Yeye anajibu SAADAN.......na huo ndio ukawa mwanzo wa jina la saadan.


Karibuni wakuu.
 
Back
Top Bottom