Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo kafumaniwa katika kujiokoa ndo likatokea la kutokea ila sio hii story wanayosema hapa.
Kuna dalili za Framework, hai make sense askari mtu mzima kufanya aliyoyafanya. Wazee wa CUBA tumeshajiongeza
Alionekana anaingia na mwanamke ila wakati wa kutoka anatoka mwenyewe kwa kuruka ukuta ,huko nikutoroka, tena na simu ya malayer
Alitaka kumdhurumu mwanamke wa watu....ona sasa!!........na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili
Ndio aruke getiHakuna sheria ya guest house inayomzuia mteja asiondoke mwenyewe hata kama aliingia na mwenza
Pia huyu ni Poti, walivyo watemi watemi angepita pale getini bila kubughudhiwa na yeyote
Hapa suala sio kumkimbia mwanamke, huyu ni mwizi.Yaani mafunzo yote ya medani anakimbia mwanamke? Angetumia zile mbinu wanazitumia kuwadunda Chadema na vibaka.
Yaani huyu alikula ugali wa chuo Cha polisi bure
[emoji3581][emoji12]Yaani mafunzo yote ya medani anakimbia mwanamke? Angetumia zile mbinu wanazitumia kuwadunda Chadema na vibaka.
Yaani huyu alikula ugali wa chuo Cha polisi bure
One Soldier DownAskari Polisi jijini Arusha amefariki dunia katika mazingira ya utata katika nyumba ya kulala wageni ya Mrina shine iliyopo makao mapya jijini hapa.
Taarifa za awali kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina Lake lihifadhiwe zimedai kuwa, Saiba aliingia katika nyumba hiyo majira ya saa sita usiku akiwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake hakufahamka mara moja .
Aliieleza kuwa marehemu aliandikisha katika kitabu cha wageni na kupewa chumba namba tano na kisha kuingia katika chumba hicho akiwa na mwanamke huyo, kibegi kidogo cha mgongoni na radio ya mawasiliano aliyokuwa ameshika mkononi.
Alisema majira ya saa 9 usiku askari huyo alitoka ndani ya chumba hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa amelala fofofo. Aliendelea kudai kuwa marehemu alikwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuruka geti la nyumba hiyo akiwa na lengo la kumtoroka mwanamke huyo, ndipo alipoangukia kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Taarifa zinadai kwamba baada ya mlinzi kusikia kishindo alienda katika geti hilo na kumkuta askari huyo akiwa ameanguka chini akivuja damu nyingi kwenye paji la uso na kutoa taarifa polisi ambapo majira ya alfajiri polisi wenzake walifika na kukuta amepotez maisha.
Hata hivyo baada ya askari polisi kufika walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa ,Justin Masejo ili kuzungumzia tukio hilo ziligonga mwamba mara baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kutopokelewa.
Mwili wa marehemu Stewart unatarajiwa kusafirishwa kwenda kwao Bukoba kwa ajili ya maziko, baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Mwenyezi mungu alilaze mahala pema peponi roho ya marehemu Stewart, Amen!
Aaamyn, sasa hiyo aibu imagine mbele ya mola wake, hivi naenda kusemaje kwa mfano? dah haya mambo yanaumiza sana.Allah atuongoze wallah ni mtihani mno, nawaza hata aibu ya wazazi wa marehemu
Mkuu ukiona hujui sehemu ya kupata chakula ujue hujaalikwa.Mapokezi ya wapi?! Au unadhani kufa ni Sawa na safari ya kwenda kwenu rombo
Najiuliza wamejuaje kwamba alikuwa anamtoroka mwanamke!??
Je huyu marehemu alimwambia mtu kuwa nipo na demu nakula show, ila nikimalizana nae nitamtoroka!??
Pia kwa maaskari wetu walivyo wababe sidhani kama angehitajika kuruka geti, pale ilikuwa anakwenda kumface mlinzi na kumuamuru amfungulie hata ikibidi angejitambulisha,, mlinzi asingegoma asilani
Kuna utata ktk hili
Kama alinunua chips kwann hawakuila mpaka anarudi nayo?
Kama bia aliingia nayo kwann hakuinywa au kumpa mwenzie mpaka anaamua kurudi nayo?
Kama mchezo umepewa mpaka mtu kalala fofo na wakati umeingia wahudumu walijua lazima utakuwa n Askari sababu ya rediokol sasa kulikuwa na ulazima gani aruke ukuta?
Kwa mazingira yale Kama alifanikiwa kumwacha Mwanamke akiwa amelala fofofo na kumchukulia simu yake huku chakula na bia akiwa navyo mkononi pamona na kutambulika kuwa n Askari sidhan Kama alishindwa kupitia njia ya mlangoni.
Hapa kuna shida nyingine zaidi ya hili mnalojadili humu.
Nataka hilo faili litoke polisi walikete ofisini kwangu kwa uchunguzi zaid
Kakimbia bill, kaiba simu ya demu na chips yai. Maisha haya.
Hali ni ngumu Mkuu...Usione tu watu wamevaa wamependeza wanatembea.....Ukiona au kuambiwa mambo wanayoyafanya, hauwezi kuamini. Na utakuta ilikuwa ni Chips Kavu (ya Tshs 1,500) au Chips Mayai ya Tshs 3,000 tu - askari alikuwa ametoka nayo mbio. Mpaka ikamponza aangukie kitu chenye ncha kali.
Simu mbili Pamoja ..... ya huyo mwanamke.......walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine...
Sasa Arusha imeifunika Dar. Poleni wafiwaPoti ana maisha duni sana😂 kukimbia na chips kweli