Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Yah upo sahihi kabisa kuna watu wana elimu nzuri na kuna vyuo huwa wanafundisha kwa muda tu.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".[emoji3064][emoji3064][emoji3064]
 
Lugha za kijeshi hizo hata samia ana jina la mnyama, wapo faru, tembo, poongo na huyo dogo mjeshi ni paka anampa mkwara panya!

Niutovu wa nidham constebo wa polisi kumzingua jwtz.
Naomba popote ukiona jwtz muwanunulie bia
Constebo wa polisi awapo kazini anaweza kumhoji mtu yeyote hata kama ana cheo kikubwa kuliko yeye, isipokuwa awe na heshima katika kufanya hivyo. Tunaposema hakuna aliye juu ya sheria hiyo ndiyo maana yake halisi. Hata mkuu wa majeshi anaweza kuhojiwa na polisi wa cheo cha chini kama yuko katika kutimiza kazi yake. Nafikiri wanaodhani kuwa mwanajeshi au mwenye cheo cha juu hahojiwi ni wale ambao hawajapitia kazi ya uaskari kama vile JKT.
 
Sasa umeridhika mwenzako kupoteza kazi.Huyo alilewa tu.Sasa subiri aanze kutumia taaluma ya kijeshi kutafuta Pesa atajuta kwanini hamkuvumilia Matusi
Awaachie nafasi na wengine wakalewe
 
Hivi kati ya JWTZ na Polisi kina nani wanafanya kazi kubwa hapa nchini?
Nchi hii kila mtu au mfanya kazi ana umuhimu wake. Polisi ni muhimu, mwanajeshi ni muhimu, watumishi wa afya ni muhimu, magereza ni muhimu, wasafishaji wa barabara, choo, majumba n.k. ni muhimuwalimu ni muhimu. Kwa kifupi kazi zote za taaluma ni zisizo za taaluma ni muhimu kwa sababu tunategemeana ili kila mfanya kazi kutimiza wajibu wake.
 
hujui walianzia wapi hii video ni fupi! kwanza TRAFIKI anakosa adabu kibishana na mtu aliyemzidi cheo mbele ya RAIA
Kwenye makosa cheo weka pembeni. Ndiyo nimyi mnadhania dereva wa gari la mkubwa au mkubwa mwenyewe hatakiwi kupewa tiketi au kusimamishwa akikosea. Sijui katika kutenda hayo makosa ataua utamuachia kwa sababu ana cheo cha juu. Kuwa mwanajeshi au mkubwa siyo kinga yas kutpofuata sheria, ama sivyo TZ itakuwa nchi ya "man eat man".
 
Leo asbh nilikuwa natoka Mazoezi, nimefika mahala traffic amesimamisha Daladala lkn hapo hapo akawa ameenda upande mwingine kusimamisha Lorry, yule Konda wa Daladala akawa anamfuata upande wa Lorry akamfikia akamshikisha buku 2 wakaachana Konda akarudi kwenye gar Daladala ikasepa..... hebu hapo jiulize alisimamisha Daladala ya nn maana hata kukagua hajakagua usipokuwa kupewa buku mbili na daladala kuondoka.... amepoteza muda wa watu wangapi hapo, amesumbua watu wangapi hapo....Police kwa ujumla wake inahitaji reform wao wametanguliza Rushwa mbele kuliko kazi yao ya msingi ya kusimamia usalama wa raia/usalama wa barabarani, sometime wanahitaji such rude treatment!!
 
Sasa umeridhika mwenzako kupoteza kazi.Huyo alilewa tu.Sasa subiri aanze kutumia taaluma ya kijeshi kutafuta Pesa atajuta kwanini hamkuvumilia Matusi
Yaani umvumilie kwa sababu akifukuzwa atakuwa mwizi. Utavumilia wangapi? Kama kuna kazi inataka nidhamu ya hali ya juu kuliko zote jeshi ni mojawapo. Ndiyo maana mwajajeshi anaambiwa tii amri kwanza maswali baadaye. Kumbuka kosa dogo la nidhamu linaweza kuletelezakufagiwa kikosi kizima au hata kuleteleza nchi ikatekwa kwa sababu ya ya mjinga mmoja asiye na nidhamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…