PreGE2025 Askari waliofunika sura zao wanadaiwa kumfuatilia John Heche huko Mwanza, yadaiwa wanataka kumkamata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wewe ya kwako mazuri au maisha yako magumu yanakuganya uhisi Serikali ndio imekusababishia?
 
Kama Tanzania bado hakuna amri ya mahakama ya kuzuia policcm kuvaa mask inafaa wadau wafungue kesi kwa dharura ili kupata hiyo court order.

Polisi mwenye nia njema hana sababu ya kuficha sura.

Ukute wanataka wakitekeleza tukio la uhalifu wasijulikane kama yule afande Shabani wa Mbeya
 
Asante sana mpiga picha kwa hii picha. Imenikumbusha picha za Gestapo wa Adolph Hitler walipokuwa wakipita usiku katika nyumba za watu na kuwakamata...kweli tumefika huku!View attachment 3331773
Kutakuwa na tatizo kubwa ndani ya serikali hii. Inaonyesha kama iko 'devolved' kiaina.

Inspector General wa Polisi ni kama yupo pembeni kabisa hakuna anachojuwa kinaendelea ndani ya jeshi lake. Kila eneo linajitosheleza lenyewe.
Muliro, kwa vile yupo kwenye kitovu, na kusikika kila siku kwenye vyombo vya habari, utafikiri ndiye mkuu wa jeshi. CHADEMA wakienda Mbeya, au kukitokea vurumai ya Mdude, unamsikia RCO wa huko au RC; wakitolea maelezo tukio ambalo ni mojatu kati ya mengi yanayotokea kila sehemu nchini.

Kuna aina ya 'disconnection' mahala. Hii siyo bure!

Rais mwenyewe amebaki kuwa mtu wa masherehe ya sanaa, michezo, vifo vya waheshimiwa wenzake, na kutoa pesa nyingi kwa machawa!
 
Kumbe inadaiwa, anaedai ni nani?
Hata huku Arusha nimeona wamevaa hivyo au ndo wapo pamoja na hao wa mwanza wanamtafuta Heche
 
Kumbe inadaiwa, anaedai ni nani?
Hata huku Arusha nimeona wamevaa hivyo au ndo wapo pamoja na hao wa mwanza wanamtafuta Heche
ni walewale special task
 
Wanawatisha wananchi. Haya ni mambo ya siasa za 2005-2010. Miaka fulani yalikatazwa kwenye kanuni za maadili ya uchaguzi na sheria sijui kwasasa hasa mwaka huu
Huku zanzibar kawaida mambo haya tushayazoea. Hivi sasa tu tayari tushaanza kuwaona hao tunawaita mazombie. Wengine hutumia mwanya huohuo wa uaskari kwa kuiba na kupora haki za watu dhaifu wasoweza hata kujitetea
 
Hao walioficha nyuso zao watakuwa wastaafu sasa wameongezewa muda kidogo mwaka 1-2 ili uchaguzi upite, baada ya hapo watupwe huko wakaangaike na uaskari sugu
 
Mmmmhh.. nani kaambiwa na polisi kuwa wanamtafuta Heche? Heche si anapigiwa simu na kwenda Polisi kama anahitajika, nina mashaka na taarifa hii
 
Mmmmhh.. nani kaambiwa na polisi kuwa wanamtafuta Heche? Heche si anapigiwa simu na kwenda Polisi kama anahitajika, nina mashaka na taarifa hii

Ungekuwa na mashaka na HAMAS wafunika nyuso ingependeza zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…