SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 50,104
- 75,552
Wacha uongo wewe.Katika mazingira hayo Askofu ina maana nchi yetu mfumo wa ulinzi hakuna Amiri Jeshi Mkuu, nafikiri tafsiri ya Jeshi la Wananchi inatafsiriwa kiholela na kupotosha umma, nchi zilizoendelea Sana Zina mifumo mingi ya usalama kabla ya Majeshi ya ulinzi.
Chukulia mfano wa matatizo ya Kibiti Jeshi la Polisi lilizidiwa na raia waliojihami kwa silaha wakiendesha ugaidi, Serikali iliongeza kasi kwa kutuma jeshi la ulinzi na likadhibiti, wakati mwingine nchi zetu Zina wasaliti wanaopanga njama sophisticated ambazo zinazidi uwezo wa Jeshi la Polisi,Serikali makini itachukua hatua mara moja bila ya kuangalia sura ya mtu au cheo chake au Chama.
Gunga
Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa ni nini mkuu? Kwangu siasa ni maisha. Bila siasa askofu atahubiri kwa nani?Binafsi sipendi sana Maaskofu kuingilia mambo ya siasa pia.. Hii ni kumbukumbu nzuri ila naye Askofu sio kazi yake kuingilia ingilia siasa, kazi yake kuu ni kanisani na kuhubiri injili, ila hii nakubali ni reminder bora kwa viongozi wote, kama Sudan jeshi lilivyoaungana na wananchi, kwani jeshi ni la wananchi..!! Ila Baba Askofu, si kila kazi ya siasa unataka kufanya..!! Ila wamekusikia, niongezee kidogo, nachojua Jeshi la wananchi kazi yao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi, tusivamiwe kutoka nje, mambo ya ndani ya nchi, najua ni Jeshi la polisi, sasa naona kama jukumu kuu linasahaulika kidogo kidogo
Chakubanga huna hoja hapo.Aisee, kwahiyo yeye kama mkuu wa jeshi mlitarajia angeongela vita wakati hatuna vita, au majukumu ya jeshi wakati wa amani yamebadilika!!!
Asiwasakame waTz wenye mawazo na itikadi tofauti na watawala.Kivipi mkuu!!! Nyinyi mlitaka amkabe na kisu au mnatakaje makamanda!!!
Sawa ili iwe hoja si mpaka iwe ni kumnanga magu na mkuu wa jeshi!!!!
Mwanajeshi hajui uchochezi!!!! Hivi mnajua hata jeshi linafanya kazi gani jaman!!!Asiwasakame waTz wenye mawazo na itikadi tofauti na watawala.
Mwanajeshi anajuwa wapi uchochezi ??!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi sipendi sana Maaskofu kuingilia mambo ya siasa pia.. Hii ni kumbukumbu nzuri ila naye Askofu sio kazi yake kuingilia ingilia siasa, kazi yake kuu ni kanisani na kuhubiri injili, ila hii nakubali ni reminder bora kwa viongozi wote, kama Sudan jeshi lilivyoaungana na wananchi, kwani jeshi ni la wananchi..!! Ila Baba Askofu, si kila kazi ya siasa unataka kufanya..!! Ila wamekusikia, niongezee kidogo, nachojua Jeshi la wananchi kazi yao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi, tusivamiwe kutoka nje, mambo ya ndani ya nchi, najua ni Jeshi la polisi, sasa naona kama jukumu kuu linasahaulika kidogo kidogo
Hakuna anayetishia utulivu wa nchi zaidi ya anayevunja Katiba ya nchi.Jaman kwani mnamjua anayetishia utulivu wa nchi??!! Maana mkuu katupa jiwe gizani.
Mkuu hicho ni klie kibabu kijana aka chakubangaKwani ilikuwa lazima yeye aongee. Hata kama ni wakati wa amani ndio aongee vile kwa kuchimba mkwala. Wapi uliona hiyo! Umeongea kitoto, sorry kama nimekukwaza upo form gani?
Angalia hizo kesi uchwara za uchochezi ktk mahakama zetu zimewalenga kina nani !! Ndiyo uibariki jwtz kujihusisha nazo . Jeshi letu libaki kuwa mali wananchi na taifa bila kubagua. Libaki kuwa kimbilio ya wananchiMwanajeshi hajui uchochezi!!!! Hivi mnajua hata jeshi linafanya kazi gani jaman!!!
Swadaktaaaaa!!!!!Huku umri wa mtu unapimwa kwa hoja zake. Ukija na hoja za kitoto hata kama una karne 4 unaonekana mpuuzi tu.
Wewe hujui ndiyo maana unashabikia upuuzi.Mwanajeshi hajui uchochezi!!!! Hivi mnajua hata jeshi linafanya kazi gani jaman!!!
Mmeshasahau ya CAG sasa mko na kauli ya CDF, mkija kushtuka mna mbili mkononi wenzenu wana 15.[emoji16][emoji16][emoji16]
Kauli ya jana ya cdf inaonyesha kuwa sio jeshi la wananchi tena bali la CCM na wasukuma wa awamu ya tanoHAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.
Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.
Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.
Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.
Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.
Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.
Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".
Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.
Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.
Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.
Utaendelea kuishi Mwalimu.
Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.
Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)
Hakupinduliwa, wanajeshi walikuwa wanataka manadiliko kwenye uongozi wa jeshi, ndiyo sababu hawakuenda ikulu.Hapo ndio ujiulize kama Baba wa Taifa pamoja na kuwa mzalendo wa kweli kwenye nchi yake alipinduliwa ije iwe kwa awa wavunja katiba,sheria, kuminya uhuru wa kujieleza ? Haichukui hata dakika moja kuwekwa chini ya ulinzi na sijui kama Rwanda anaweza Saidia chochote.
Sijui unaenda tena kwa unaowaita mabeberu kuwaomba msaada? !!
Kauli ya jana ya cdf inaonyesha kuwa sio jeshi la wananchi tena bali la CCM na wasukuma wa awamu ya tano