Askofu Bagoza: Ukisomeshwa na Kanisa halafu ukahamia Serikalini nani ataifungia Serikali?

Na wasioajiriwa walipiwe na wazazi wao

Na mkataba wa kupewa mkopo una sharti,kuwa ni lazma ufanye kazi serikalini

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Unafikili hiyo Dr.ana njaa Kama yako.
 
Kwani kulipa mkopo ni lazima ufanye kazi serikalini? Na usipokuwa na kazi basi mkopo unasemehewa? Ninavyojua mimi wakopeshaji wanakupa masharti ya namna ya kulipa na hawajali uwezo wako wa kulipa au status yako ya ajira. Serikali kama wanaona wanawahitaji sana hawa madaktari wangewasamehe deni lao kwa masharti ya kuhudumia katika hospitali za serikali kwa muda fulani. Au wangeingiza kipengele cha kuwa daktari atakaechukua mkopo ajue atawajibika kufanya kazi serikalini maisha yake yote na kupiga marufuku hospitali binafsi na za taasisi nyingine kuajiri madaktari waliokuwa na deni la mkopo bila kibali cha mkopeshaji, hata kama Serikali haina nafasi za ajira.

Amandla...
 
Serikali inahusika na elimu ya mtu kwa namna moja au nyingine.
Kwani ulipokuwa primary school ulisomeshwa na kanisa? , au tunafikiri elimu ni ile ya juu peke yake?
Ni jukumu la msingi la serikali yoyote duniani kuwapa elimu bora watu wake kwa maendeleo ya nchi husika.ila kuwapa elimu haimanishi wote wakafanye kazi serikalini,wachache watafanya kazi serikali,wengine wataanzisha makampuni yao,wengine wataanzisha hospital zao na wengine wataamua kuwa wakulima.lakini wote hao wanajenga nchi .Ile kauli niya hovyo iliyotolewa na mtu ambaye hakutaka kushughulisha akili yakevizuri
 
Mkuu mkopo unalipa ukiwa popote pale,may be simple question.huko hospital binafsi wanahudumia watu wa nchi gani?
 
Kwani ukienda Sekta binafsi mkopo hatulipwi?Je waliosomeshwa na taasisi za dini wanapoenda serikalini nani analipa gharama?Na je wanaosomeshwa na serikali na hawafanyi kazi serikalini na wako nje ya nchi nao je.Kwenye mkataba wa mkopo kuna kipengele Cha mkopaji kufanya kazi serikalini?Huko si kuua Sekta binafsi ambazo Zina mchango mkubwa kwa wananchi na serikali yenyewe?Naamini Sasa tunapoteza mwelekeo kabisa Kama nchi.serikali yenyewe haina ajira na ukipata ajira mishahara kiduchu kwa nn watu wasiende sekta binafsi na Kama serikali inawataka si waongeze mishahara?wafanyakazi wamechoka kunyonya waachwe watafute greener pastures.
 
mimi nahitaji madaktari waanze kupigishwa interview wanapoomba kazi za serikali watakua na heshima tu na kazi zao. Na sio kuwapeleka tu bila hata kuwahoji kwenye interview ndio maana wanakosa nidhamu.
Interview ya Nini serikali ijitathimini inapoangukia usitafute mchawi wakati mchawi ni serikali yenyewe inayonyonya wafanyakazi.iwalipe haki yao na si kunyonya jasho Lao.
 
Magu yuko sahihi ukitaka vya bure ukubali masharti ya bosi ni ukipewa friji la Coca-Cola bure uache kuweka bidha zao uwekage Pepsi
Serikali ndo inataka vya bure iache kulia Lia Kama mtoto iwalipe mishahara mizuri si kuwabinya jasho lao.
 
Dokta ataucheza wimbo wao " wacha waisome namba eheee... UHUJUMU MAGUFULI..!
MBEBA MAONO aliyaona haya na kutukumbusha,lakini unafiki na ubinafsi tulio nao Watanganyika umetugawa na kumwacha CHIZI atambe na kutuumiza atakavyo.
 
Yaaani unajifanya unajua kumbe hujui,mkopo wa serikali mtumishi analipa kwa hata kama alihama deni liliendelea kulipwa sio kwamba ukihama unaacha kulipa
Analipia tena kwa gharama kubwa mno na pretension fee juu
 
Kwani kanisa linasomesha kisha linadai ghalama ziludi au inasomesha bure? Maana serikari inakopesha na ndio maana inahitaji ilipwe
Naomba bagonza akiri inaanza kupungua hata kufikiri nini kilinganishwe.

Magufuri kauliza kwa nini huyo dakitari aliomba serikarini na kuchukua kianzio wakati anajua kuna malipo sehemu nyingine ni mkubwa na kuzuia nafasi ya wengine kupata akira?
Hilo linatakiwa lijibiwe na Bagonza kwanza.

Kwa nini aliomba serikarini wakati anajua binafsi zipo na kuchukua pesa ya kianzio na kukimbia?
 
Tulizana ndugu dimatteo! Ebu rudia tena kusoma ulichoandika na ulingalishe na nilichoandika kimanti. Kisha jipime unastahili kuwekwa kundi gani!
 
Vipi Bagonza hafungi makanisa kwenye dayosisi yake tena?
 
Interview ya Nini serikali ijitathimini inapoangukia usitafute mchawi wakati mchawi ni serikali yenyewe inayonyonya wafanyakazi.iwalipe haki yao na si kunyonya jasho Lao.
Kama walijua serikalini kuna unyonyaji kwanini hawakuomba hizo kazi kwenye hospitali za private kabla ya kuajiriwa na serikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…